Kama kuna mafanikio mbona kuzuia watu wasitoe dukuduku lao? Mbona kuzuia wakosoaji wake wote wasiseme alikoharibu? Uharibifu ni mwingi sana kuliko mafanikio. Katika kipindi hichi cha Magufuli ndio kipindi deni la Taifa limepaa kuliko nyakati nyingine zote tena wizi na rushwa vimepamba moto, miladi mingi yenye mikataba ya kifisadi imefanyika chini ya Magufuli uku uchumi wa nchi ukisinyaa, uchumi wa mtu mmoja mmoja ukishuka kwa kasi ya ajabu uku haki za kirahia zikiendelea kuporwa.
 
Uislamu na Ukristo ni dini mbili tofauti, zenye mitazamo tofauti kiimani.

Katika Uislamu, msikiti ni nyumba takatifu ya kiibada. Kuanzia kujengwa, kutumiwa na kutunzwa kwa msikiti kumewekwa taratibu na sheria katika uislamu. Sio jambo la holela holela.

Kitendo cha mtu mmoja (pasipo kutumwa na waislamu) kwenda kukusanya sadaka za waumini wa kikristo kanisani (mahali ambapo waislamu wanaamini 'makafir' hukusanyika kumwabudu Yesu kama Mungu wao na 'makafir' hao kufundishana namna ya kukabiliana kiimani dhidi ya uislamu) kwa lengo la kupata pesa za kwenda kujenga msikiti wa waislamu kumeleta mjadala mkubwa na mpana katika jamii.

Wapo ambao wanasema hicho ni kitendo cha utu, ujirani mwema na upendo baina ya dini mbili tofauti zenye kukinzani kiasili.

Lakini wapo wanaoamini kuwa hicho ni kitendo cha dhihaka ya kiimani dhidi ya uislamu, kuudhalilisha utu wa kiimani wa muislamu mbele ya mkristo na kunajisi imani ya takatifu ya kiislamu.

Karibuni tujadili kwa kina, hekima na staha, ili kujua kama jambo hilo ni jema (ili tujenge utamaduni wa kuliendeleza) au kama ni jambo baya (tulikemee na kulifuta katika jamii yetu).
 
Rais ashauriwe haya ya kiimani awachie wenyewe yeye afanye kwa nafasi yake kama muumini au mdau kimya kimya kama ambavyo baba wa taifa alifanya,Mzee Mwinyi,Mzee Ben na Mzee JK
 
Ndiyo maana mnahusishwa na ukorofi wa wa kujitoa muhanga bila sababu,hii ni kweli mko hivyo na yale mauaji ya IS au Al Shaabab ndiyo imani

Hapa hakuna cha ajabu zaidi ya kutafuta kuhitilafiana na kujikweza kua mngeweza,hamjiongezi kua yule ni Rais wa watu wote na hakufanya kwa ubaya bali ninkuweka maelewano mema tu kiimani na kindugu moja kama waTanzania

Angefanya hivyo msikitini kwa ajili ya waKristo wala usingesikia chochote wakisema maana Christian ni amani kwa watu wote,lakini binafsi hapa nilijua tu mtalipuka

NB: I'am a Rastaman
 
Ingependeza Kama hiyo harambee ingeitishwa na waislamu wenyewe msikitini , na mheshimiwa angeenda Kama mwalikwa kufanya huo uhamaeishaji.
 
Bakwata si ya Waislam
1660090_FB_IMG_1514731600839.jpg
 
Bakwata ni sehemu ya CCM. Kilichofanyika ni sahihi, jengeni msikiti huo wa msaada.
 
Huko uarabuni waislamu wamepewa jengo la kanisa Katoliki walitumie kama msikiti na wamelipokea kwa Upendo na maisha yanaendelea!
 
Halafu just imagine ni msikiti wa ndani ya Ikulu Ya Dodoma

Huo msikiti miaka ijayo utaleta masimango makubwa dhidi ya waislamu kuwa umejengwa kwa sadaka za kanisani na pia utatumika kama kichaka cha kuficha udini mkali wa kimfumo dhidi ya waislamu, maana kila itakapotokea waislamu kupaza sauti kutaka fairness wataambiwa nchini hakuna ubaguzi ndiyo maana mlijengewa msikiti wenu wa Ikulu ya Chamwino kwa sadaka za kanisani!

Nashauri waislamu wajenge msikiti wao wenyewe kwa fedha zao wenyewe, hizo pesa walizochangiwa za kanisani wazipeleke kusaidia watoto yatima
 
Halafu msikiti wa ndani ya Ikulu Ya Dodoma

Huo msikiti utaleta masimango makubwa dhidi ya waislamu kuwa umejengwa kwa sadaka za kanisani

Nashauri waislamu wajenge msikiti wao wenyewe kwa fedha zao wenyewe, hizo pesa walizochangiwa za kanisani wazipeleke kusaidia watoto yatima
Acha tuwajengee msikiti ili mutuite makafiri vizuri...!!
 
Kama ni dhihaka ya kiimani basi dhihaka kubwa duniani lipo kwa Rais wa Uturuki (Turkey) Erdogan kutaifisha Kanisa kubwa kuliko yote duniani Hagia Sophia na kuligeuza kuwa msikiti!! Kanisa lilijengwa karne ya tano yaani circa mwaka 400 A.D.!!! Msikiti na Kanisa yote ni sehemu za ibada, sioni tatizo hata kama ni atheists(ambao hawaamini kuwepo kwa Mungu).
 
Gadafi alijenga msikiti kule dodoma hiyo haikuwa dhihaka na hapo kabla wakati wa Vita ya kagera iliyohusisha Tanzania na uganda.. aliipa ufadhiri Uganda kwa kuwapa siraha na baadhi ya wanajeshi kutoka Libya na wengine majeshi yetu yaliwateja wanajeshi wa gadafi!!.. kama huo msikiti haukuwa dhihaka kwa mtu aliekuwa upande wa adui yetu je, unafikiri itakuwa dhihaka kivipi kwa watu tunaoishinao mitaani kwetu,tunafanya nao kazi,tunakula nao,tunashea historia moja ya nchi yetu n.k..

Kiongozi imara ni yule anaeonyesha uimara wa muunganiko wa watu wake,umoja na mshikamano Kama ilivyoainishwa kwenye ngao ya nchi yetu!.
Sioni dhihaka hapo bali naona taifa linalojitambua kuwa linawatu mbalimbali wenye utofauti wa kidini n.k ila bado linajali utu na mshikamano uliomarishwa na umoja imara.. taifa linalojua umuhimu wa kuabudu hata kama wewe si wa dini fulani lkn misingi yako bado ni imara!..

Wachache wenye ulimbukeni wataona kama jambo la ajabu lkn binafsi sioni utofauti kwa swala hilo.. kwani tukumbuke Kodi zetu za waislamu ma wakristo n.k ndizo hizohizo zinazolipa haohao mishahara waislamu na wakristo.. so ni kitu Cha kawaida sana ukiangalia kwa jicho pana.
 
Back
Top Bottom