10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...

Pia soma;


Baba laoooo
 
Tutazungumzia maendeleo pale ambapo wananchi wa kawaida wana haki na utawala bora. Leo haki za binadamu zinavunjwa . wananchi wa kawaida wana lalamika maisha yamezidi kuwa magumu. bei za bidhaa zimepanda.

Ukiongea unapotezwa. Upinzani na demokrasia katika nchi zimelala chali, Vipi tutamsifia Magufuli?. Biashara ndogo ndogo zimepigwa na chini. TRA inakufuata hata njugu karanga zinatushinda kuuza. Vipi tumsifie Magufuli?.
 
Pamoja na misemo mingi kama hii iliyopo, hakika hakuna ubishi kuwa huwakirisha mtu aliyepitia

1. Misuko suko hatimae mafanikio
2. Shida, hujuma, na majaribu lakini hakukata tamaa.

Kibwagizo kikubwa huwa nikwamba, pamoja nayote hayo alipata mafanikio, nahuyo anaitwa mshindi

Ila kama asingeyapata mafanikio lkn alivuka yte hayo, ataitwa Mpambanaji.

JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, eye ni MSHINDI.

Kwanini JPM ni mshindi

Mh Rais john p. Magufuri a.k.a brudoser. Mara tu baada yakuchaguliwa kuwa Rais wa JMT akakumbana na yafuatayo:

1. Account nyeupe, malipo hewa yaliyoandaliwa kukomba fedha, mzee akaziwahi na akapiga chini Gavana wa BOT
2. Darali wa mabeberu akatangaza ugonjwa wa dhika! Mzee akaiona akaipangua akampa za uso mwele malesera.
3. Ikatangazwa njaa kila kona ya nchi! Mzee akaikwepa akawakoswa koswa waliotangaza akawapa nyo. Ikawa shwari
4. wakataka kufungulia maji ya mabwawa ya umeme! Mzee akaisoma akawapiga bit ngoma ikatulia.
5. wakaanza kuhujum ndege, mzee akaisoma akalala nao mbele kwa mbele! Wakahama nchi na wakawa vilema
6. wakasitisha misaada ya Rea mzee akatoa fungu na umeme uko kila kona.
7. Kari ya mwaka sasa, WAKALETA COVID-19 aaaah!! Mze akashtuka akawaeudishia za mdomo, mpaka leo wanatema dam.
Rais magufuli haya yote kayafanya kwakuwa tu , mungu alimleta atuokoe watanzania, hata yesu aliwaambia wanafunzi wa yohana kuwa! Anauliza kama mimi ndie masiha?? Wakasema ndiyo.

Yesu akawaambia nendeni mkamwambie viwete wanatembea na vipofu wanaona!

Kwa asiye mkubari JPM mwambieni.. Barick wamelipa na kukubari kuunda nao kampuni

Mwambieni .. standard guage iko moro to mza , Bwawa la umeme la nyerere hydropower iko 75%
Mwambieni.. hospitali aliyoiacha mwl ile ya msoma na vituo vya afya , zahanati, hosp za rufaa zimejengwa.

.haki mahakamani iliyopotea sasa imerudi,
Habari ya unanijua mimi sasa haipo.
Lakini msisahau nayale mnayoyaona kwa macho yenu.

October 2020 tumpe kura kwa wingi atuingize kanaani.
Enzi na Enzi
Dar es salaam.
 
Miradi ya magufuli ni upotevu tu wa pesa za walipaa kodi maana haitakamilika.. unaua biashara na vyanzo vya mapato , alafu ndio unaanzisha miradi mikubwa,!
 
Ameifanya Chato ifanane na Gbadolite ya mobutu sese seko kwa maana anajenga/ amejenga
Taaa za kuongoza magari( bila magari?
Uwanja wa ndege wa kimataifa (bila ndege za kimataifa kutua) sana Sana popo na bundi wanakaa
Amejenga uwanja wa michezo wa watu nusu lakin bila kuwa na team league kuu au hata iwezekano wa uwanja kujaa kwa miaka50 ijayo
Hospital ya rufaa
Haya Mambo aliefanya Mobutu kule Gbadolite
 
Nina mkubali Magufuli lakini watendaji wake wanamuogopa ndio maana hadi leo wastaafu wa ATCL bado wanahangaikia mapunjo ya PPF/PSSSF zao bila kulipwa japo mahakama iliagiza walipwe. Wizara UUM inasema mlipaji ni Wizara ya Fedha Katibi Mkuu Kiongozi kaelekeza wizara ya UUM kuwalipa wastaafu hapo ndio unapo ona danganya kwa wazee. Raisi anasema kalipa madai yote ya PSSSF ya wastaafu.PSSSF wanasema hawaja pokea malipo kwa ajili ya wastaafu wa ATCL. Inshaallah ipo siku Mungu atamuelekeza Magufuli awalipe wastaafu wa ATCL kama alivyoagiza walimu walipwe.
 
Back
Top Bottom