Ilani ya CCM imeendelea kutekelezwa kwa umakini mkubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo maendeleo ya jamii na vijana.

Leo Salim Kikeke wa BBC amehabarisha juu ya nahodha wa Taifa stars mh Mbwana Samatta kufanyiwa vipimo tayari kabisa kusajiliwa na timu ya Aston Villa ya England inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

CCM hoyeeee.........Taifa stars hoyeeeee.........!

Maendeleo hayana vyama!
Acheni kuwaudhi wapiga kura kwa kuingiza mizaha Kumbe ilani ilisema 2015-2020 ccm itamtafutia Samatta klabu Uingereza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilani ya CCM imeendelea kutekelezwa kwa umakini mkubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo maendeleo ya jamii na vijana.

Leo Salim Kikeke wa BBC amehabarisha juu ya nahodha wa Taifa Stars Mh. Mbwana Samatta kufanyiwa vipimo tayari kabisa kusajiliwa na timu ya Aston Villa ya England inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

CCM hoyeeee. Taifa stars hoyeeee!

Maendeleo hayana vyama!
Huu unafiki uliondika hapa hata enzi hizo za kina Yuda walikuwepo na Yesu aliwakataa sasa hapa juhudi za mtu binafsi na uhusiano wa ccm wapi na wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli akijitahidi isishuke itakuwa bingo kwake.

Dream yake ni kucheza EPL , hata kama hali ya timu sio nzuri lakin kule anaweza kuonekana na klabu nyingine kubwa kwa urahisi.

Ni lazima awahi mapema kwa maana wazungu wapo very sensitive na mambo ya age. Mbwana now is 27, ni mkubwa kwa mpira wa Ulaya.






Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Dream yake ni kucheza EPL , hata kama hali ya timu sio nzuri lakin kule anaweza kuonekana na klabu nyingine kubwa kwa urahisi.

Ni lazima awahi mapema kwa maana wazungu wapo very sensitive na mambo ya age. Mbwana now is 27, ni mkubwa kwa mpira wa Ulaya.






Sent from my iPhone using JamiiForums

Akifanya vizuri atakuwa marketable zaidi mkuu. Yote kwa yote katutoa kimasomaso au vipi.
 
Na Kasambula Theonest, Kigoma.

Tanzania leo inaungana na mataifa mengine duniani kuuaga mwaka 2019. Kuna mengi mazuri ya kuusemea huu mwaka lakini makala hii inaongelea kazi nzuri aliyofanya Rais John Magufuli wa Tanzania katika mwaka huu wa 2019 na inayoendelea mwaka 2020.

Kwanza nikiri kwanza kwamba Rais Magufuli amefanya mengi katika mwaka 2019 katika kuwaletea watanzania maendeleo. Kwa wingi huu naomba nikiri kuwa siwezi kuandika yote maana komputa mpakato itavunjika. Nitaandika machache kwa leo mengine nitayandika siku za usoni kwani kazi ndo imeanza.

Ujenzi wa bwawa kubwa la umeme katika Afrika Mashariki na la nne kwa ukubwa Afrika ( Mwalimu Nyerere Hydropower Project)
Katika mwaka 2019, Rais Magufuli ameweza kusimamia wazo la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere la kujenga bwawa kubwa la umeme litakalozalisha megawati 2,115 litakalo kamilika mwaka 2022 katika mto Rufiji.

Haikuwa kazi rahisi kwa sababu ya kelele za wapinga maendeleo wa ndani na nje ya nchi waliotaka kukwamisha kazi hii lakini Rais alisimama kidete na kuhakikisha mradi unatekelezwa.

Mradi huu unaojengwa kwa kodi za wananchi kwa zaidi ya shilingi tirioni sita za kitanzania ukikamilika utaweza kuifanya Tanzania kuwa msambazaji mkubwa wa umeme katika nchi za Afrika mashariki na kati.

Usafiri wa Anga
Ni vigumu kuamini lakini ndo ukweli kuwa tunamaliza mwaka 2019 Rais Magufuli akiwa amenunua ndege nane katika 11 ambapo tatu zinatarajiwa mwakani. Shirika la ndege lilishafirisiwa na mafisadi na kulikuwa na ndege moja tu wakati Magufuli anaingia madarakani. Sasa Magufuli amerudisha heshima ya Tanzania.

Ukiwa Afrika Kusini, Zambia, Malawi, DRC, Mumbai- India na muda si mrefu Guangzhou utaona twiga wetu akikuambia Tanzania tupo laivu kazini. Tunaambiwa baada ya ndege za abiria sasa madege ya mizigo yanafuata. Huyo ndo Magufuli Rais wa Watanzania, mchapa kazi na asiyependa nchi kuitwa maskini wakati ina rasilimali nyingi.

Umeme Vijijini
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tangu tupate uhuru, Rais Magufuli anaifanya nchi kuingia katika mwaka mpya wa 2020 huku vijiji 9000 kati ya 12,000 vikiwa vimeunganishwa na umeme. Asante sana Rais Magufuli kwa kuona shida za watanzania wanyonge na kuwaunganisha na gridi ya Taifa ili wapate maendeleo.
Ikumbukwe pia kuwa bila umeme hamna maendeleo.

Huyo ndo Rais Magufuli ambaye ameamua pia kila mwaka bilioni 200 za kitanzania zitolewe kupitia mradi wa umeme vijijini ( REA) ili kujenga mifumo ya umeme vijijini na kununua miundo mbinu yake. Naweza Kusema hongera wana vijiji wa kitanzania hayo ndo matunda mliyochuma mlipomchagua Maguguli kuwa rais wenu mwaka 2015.
Upatikanaji wa maji safi na salama vijijini.

Katika moto uleule wa kuwajali watu maskini na watanzania kwa ujumla, Rais Mafuguli anaifanya Tanzania kuingia mwaka 2020 huku asilimia 67 za wananchi wanaoishi vijijini wakiwa wameunganishiwa maji safi na salama kutokana na miradi 1600 iliyoanzisha na serikali ya awamu ya tano.

Raisi Magufuli anatuambia kuwa mpaka mwaka 2025 kila kijiji kitakuwa kimeunganishiwa maji. Kwa wale tunaoishi tunaona kuwa upatikanaji wa maji umeongezekeza.

Takwimu zinasema zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanaoishi mjini wameunganushiwa maji na yanatoka kila siku. Haya ndo matunda ya uhuru, tuendelee kumuunga mkono jemedali wetu Rais Magufuli.

Sekta ya utalii
Kwa mara ya kwanza tangu nchi hii ipate uhuru, Rais Magufuli ameongoza jitihada za kungeza watalii ili kuinua pato la Taifa ambapo sekta ya utalii ni ya pili katika kuchangia pato la Taifa.

Pamoja na kelele za mabeberu na wanasiasa wa upinzani kuizushia Tanzania kuwa ina ebola ili watalii wasitemebelee nchi mwaka 2019, nchi imeendelea kupata watalii zaidi ya 10,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwamo ulaya, Asia…
We muongo sana kwenye kipengele cha REA yaani suala la umeme vijijini umedanganya sana, kwa kuwa umedanganya hili suala ninalo lijua kinaga ubaga basi huenda na hayo uliyoyaeleza nisiyo yajua utakuwa umechanganya uongo pia. Uongo si kitu kizuri ukitaka data kamili za REA utaniambia nikaupatie ujue kuwa suala la umeme vijijini bado sana bali ni wananchi wachache sana walionufaika na huduma ya REA na walio wengi ni wale waliopata huduma hii kipindi cha serikali ya hawamu ya 4, hawamu hii ya 5 ni wanavijiji wachache sana ambao wamefikiwa na huduma hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kiswahili cha mjini ninaweza kusema nimechizika, kinoma kwa Yale anayoyafanya JPM. Ametafuna mifupa ambayo watangulizi wake hata kujaribu, kwangu Mimi achana na vituo vya Afya na hospital, kuhamishia serikali Dodoma hakuna ambaye angesubutu, nakumbuka nilivyokuwa nalala naumwa mbu Kigongo ferry kusubili kivuko sasa anajenga daraja! Huyo anayebeza akimaliza kutukana hadharani arudi nafsini mwake aseme nisamehe Mora wangu mlinde JPM mpe hekima Afya na nguvu za kuipeleka TZ kwenye mafanikio. Kama Mungu amenipangia miaka 100 ya kuishi apunguze 5 aongeze upande wake unapiga kazi si mchezo.Naomba kwa uthubutu huo huo kabla hajamaliza vipindi vyake atutolee ziwani MV Bukoba tuiweke makumbusho, vizazi vya Leo vione moja ya matukio yaliyotikisa Nchi ikazizima kwa vilio mwaka 1996
 
JPM ni Raisi ambaye atakuja kuwekwa kwenye vitabu vya historia


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa kiswahili cha mjini ninaweza kusema nimechizika, kinoma kwa Yale anayoyafanya JPM. Ametafuna mifupa ambayo watangulizi wake hata kujaribu, kwangu Mimi achana na vituo vya Afya na hospital, kuhamishia serikali Dodoma hakuna ambaye angesubutu, nakumbuka nilivyokuwa nalala naumwa mbu Kigongo ferry kusubili kivuko sasa anajenga daraja! Huyo anayebeza akimaliza kutukana hadharani arudi nafsini mwake aseme nisamehe Mora wangu mlinde JPM mpe hekima Afya na nguvu za kuipeleka TZ kwenye mafanikio. Kama Mungu amenipangia miaka 100 ya kuishi apunguze 5 aongeze upande wake unapiga kazi si mchezo.Naomba kwa uthubutu huo huo kabla hajamaliza vipindi vyake atutolee ziwani MV Bukoba tuiweke makumbusho, vizazi vya Leo vione moja ya matukio yaliyotikisa Nchi ikazizima kwa vilio mwaka 1996

Mkuu hizo hospitali na vituo vya afya vyote kwa pamoja havivuki bilioni 300. Leo Mo katangazwa kuwa biashara zake zimeporomoka kwa bilioni 300 na bado anaendelea na biashara. Sasa hiyo miradi ya hospitali inayokufanya uchizike na Magufuli, ungekuwa Mo si ungekufa kwa shock?
 
JPM ni Raisi ambaye atakuja kuwekwa kwenye vitabu vya historia


Sent from my iPhone using JamiiForums

Mkuu hizo sifa ni zile unazolishwa, sasa hivi uchumi uko hoi, na ushahidi ni baishara nyingi kufungwa na kukosekana kwa ajira. Deni la taifa nalo linakuwa kwa kasi ya mwanga.
 
Back
Top Bottom