Hivi we jamaa bado tu hawajakuona manake hujaanza leo kuandika utumbo na kuweka namba yako ya simu!
 
Ndani ya hayo mafanikio, siku ukipata nafasi uje uanike deni la taifa limekuwa kwa kiwango gani ndani ya hiyo miaka minne ya hayo mafanikio.
Una maana jamaa yupo vizuri kwenye matumizi ya mikopo kuliko waliomtangulia?
maana hapo awali tulikuwa tukikopa na hatuoni chochote!
 
Amefanya vitu vya ukweli:- (ujangili umepungua,elimu bure, barabara, umeme, maji, nidhamu, vituo vya afya), Rushwa.

Bado kuna changamoto, TRA; ports, ushuru ni changamoto, kilimo bado sana, mazingira ya uwekezaji bado hayajatulia, there is work to be done, kuyafanyia haya mambo ni kazi yenu (Serikali)

Ajira, elimu kwa vijana kujifunza kujitemea ni muhimu sana, tuangalie tunaweza kuwasaidiaje vijana wetu kupata taaluma, nafasi za kufanya biashara, kujiajiri.

But we are moving foward, despite and inspite of all our problems.
 
Ukisikia unyafuzi wa ubongo ndio huu. Inakuwaje unatamba unaweza miradi mikubwa lakini tishio la ugonjwa hatari wa maisha ya wananchi wako unapiga magoti kuomba msaada?
Ebola ni ugonjwa tishio ambao kwa uhatari wake unaweka kila kitu pembeni una dili nao, lakini kwetu wanunua ndege cash hela $ 9M hatuna hadi tuwapigie magoti mabeberu?
IMG_20190920_051528.jpeg
 
Ndani ya hayo mafanikio, siku ukipata nafasi uje uanike deni la taifa limekuwa kwa kiwango gani ndani ya hiyo miaka minne ya hayo mafanikio.
Hata deni likiendelea kukua sisi tunaona pesa zinapo kwenda (zina kwenda kwenye maendeleo ya taifa-barabara mpaka mlangoni {Yombo}). Siyo tena mifukoni kwa mafisadi. Keep it up Magufuli.
 
Magu kaweza kufanya hayo yote kwa sababu abembelezi mtu yeyote.
Hamwogopi binadamu yeyote.
Anataka majibu yaani jawabu la kazi au mradi hataki story za Karumekenge.
Hafuati mfumo wa urasimu
Kapangua mfumo mzima wa tawala na CCM.
Hakati tamaa,
Mtamsema wee,lakini ndio anaongeza speed.
Hana rafiki wa kudumu,wala hana aibu ya kumfokea Waziri au Kigogo yeyote kwenye umati wa watu.
Ana upenda uraisi hataki aonekane anapwaya kwenye yale anayoyoyahimiza.
Ukiota unamkwamisha,usishangae ,ukajikuta unakimbilia Ikulu kumiomba msamaha tena live kwenye luninga.
 
Ukisikia unyafuzi wa ubongo ndio huu. Inakuwaje unatamba unaweza miradi mikubwa lakini tishio la ugonjwa hatari wa maisha ya wananchi wako unapiga magoti kuomba msaada?
Ebola ni ugonjwa tishio ambao kwa uhatari wake unaweka kila kitu pembeni una dili nao, lakini kwetu wanunua ndege cash hela $ 9M hatuna hadi tuwapigie magoti mabeberu?View attachment 1211817
Hii barua haikuandikwa na serikali! Iangalie vizuri
 
Ukisikia unyafuzi wa ubongo ndio huu. Inakuwaje unatamba unaweza miradi mikubwa lakini tishio la ugonjwa hatari wa maisha ya wananchi wako unapiga magoti kuomba msaada?
Ebola ni ugonjwa tishio ambao kwa uhatari wake unaweka kila kitu pembeni una dili nao, lakini kwetu wanunua ndege cash hela $ 9M hatuna hadi tuwapigie magoti mabeberu?View attachment 1211817

Sasa kama ugonjwa hatari wa Ebola huna hela ya kuucontain, unaandika barua kuomba vijisenti vya dola milioni 9.5 kutoka kwa mabeberu, una haki kweli ya kujitapa kuwa Uko njema hazina?

Hizo hela alizohongahonga wapinzani waunge mkono juhudi angezitumia vizuri hii aibu ya kuomba vijisenti isingekuwepo
 
Una maana jamaa yupo vizuri kwenye matumizi ya mikopo kuliko waliomtangulia?
maana hapo awali tulikuwa tukikopa na hatuoni chochote!

Ni mada pana, yeye amekopa ameingiza pesa kwenye miradi gani, na wenzake waliokopa waliingiza pesa kwenye nini. Pia muda wa kukopa baina ya mmoja na mwingine. Kwa maneno maraisi alichokopa kimefanya nini, na terms za kulipa hiyo mikopo ikoje.
 
Hata deni likiendelea kukua sisi tunaona pesa zinapo kwenda (zina kwenda kwenye maendeleo ya taifa-barabara mpaka mlangoni {Yombo}). Siyo tena mifukoni kwa mafisadi. Keep it up Magufuli.

Uko sahihi sana, tatizo pekee la wananchi wa nchi hii ni barabara pekee yake, ajira kwako sio jambo muhimu?
 
DNdugu zangu hivi nikwanini wanaCCM wengi hawampendi magufuri licha ya wananchi wengi wakawaida kumpenda? Je shida ninini?
 
66 Reactions
Reply
Back
Top Bottom