Hivi ndege imeandikwa hapa Kazi tu,unategemea kwa kutumia slogani ya Ccm kwny mali ya taifa yenye watu wenye vyama tofauti tofauti huo uzalendo/utaifa utatoka wapi?

Kwani mngeiita hata Fahari ya Taifa. ingekuaje?

Mambo mengine mnazingua wenyewe halafu kikinuka mnatafuta mchawi.
 
Umeichukua sehemu ukaikopi hapa alafu umeshindwa kuweka acknowledgment lakini pia paragraph setting imekushinda
 
1568800108088.png

BINADAMU ameumbiwa mitihani mingi, lakini moja kati ya mitihani hiyo ni kupewa uwezo wa kuhisi maumivu na hasira huku akiagizwa na Muumba wake kumsamehe anayemkosea na kumuombea mema adui anayepanga kumdhuru Huenda mtihani huu ndio uliosababisha mpigania uhuru wa India aliyefanikiwa, mmoja kati ya wanafalsafa ambao fikra zao zinaishi ingawa miili yao imelala, Mahatma Gandhi kusema, “watu dhaifu hawawezi kusamehe, kusamehe ni kielelezo cha tabia ya watu imara”.

Lakini falsafa hiyo ya Gandhi itaongezwa nguvu kwa mtu ambaye anasamehe si kwa sababu hana namna ya kumuadhibu aliyemkosea, bali ana mamlaka yote na nguvu za kumuadhibu lakini ameyavumilia maumivu na kumsamehe aliyemuumiza. Hivi karibuni, Rais John Magufuli ameonyesha uimara wa hali ya juu, akiwasamehe watu ambao wameonekana au kusikika hadharani, wakimkashfu au kumtukana. Licha ya kuwa na nguvu kubwa anayopewa na Katiba ya Nchi kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu, amejishusha akawakumbatia waliomtukana na kuwasamehe, ingawa amekiri kweli ‘inauma’.

walitenda kosa hilo. Kumbuka mmoja alikuwa Waziri katika awamu yake na mwingine amewahi kuwa waziri katika serikali zilizopita. Kama hiyo haitoshi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye naye alipokea msamaha wa Rais Magufuli kwa kosa hilo hilo, kumtukana. Alimualika Ikulu, akamsikiliza, akamsamehe hadharani na zaidi akampa ushauri wa namna ya kupiga hatua kwenye maisha yake ya kisiasa.

Akamtia moyo na kumuondoa wasiwasi! Hii ni ishara kuwa Rais Magufuli amefanikiwa kuushinda mtihani ule wa binadamu, ameonyesha uimara na kuishi maandiko ya Mungu anayoyasoma, ingawa anakiri inauma. “Inauma, kusamehe kunaumiza lakini ninasema kwa dhati kabisa kwamba nimemsamehe,” alisema Rais Magufuli alipokuwa akitangaza msamaha wake.

Katika Biblia Takatifu, neno ‘msamaha’ kwa lugha ya Kigiriki limeandikwa zaidi ya mara 146, na kwenye Quran Takatifu msamaha umetajwa zaidi ya mara 100 na rehema takriban mara 200. Hii inaonyesha jinsi ambavyo Mwenyezi Mungu anasisitiza kusameheana. Ni maneno matatu makuu yanaweza kuiokoa dunia nzima, ‘msamaha, upendo na rehema’.

“Unisamehe makosa yangu, kama ninavyowasamehe walionikosea.” Huu ndio mstari wa Biblia Takatifu, unaopatikana kwenye sala maarufu ya ‘Baba Yetu’ aliyoifundisha Yesu Kristo kwa wanafunzi wake, mstari ambao Rais Magufuli alieleza kuwa aliutafakari alipokuwa anausema anaposali na akaamua kuwasamehe Makamba na Ngeleja.

Je, kukasirika ni dhambi? La hasha, kukasirika si dhambi kwani hata Mwenyezi Mungu hukasirika. Watu humuudhi Mungu, na watu huudhi watu, lakini Mungu aliyesema hata kama dhambi zako ni nyekundu kama bendera zitakuwa nyeupe kama theruji atakapokusamehe, anatutaka tuishi hivyo katikati ya maudhi na hasira.

Lakini matunda ya hasira yanaweza kuwa dhambi. Biblia inasema, “kuweni na hasira lakini msitende dhambi, jua silichwe na uchungu wenu bado haujatoka (Waefeso 4:26).” Katika Quran Takatifu pia, inaeleza jinsi ambavyo Mwenyezi Mungu anampenda mtu anayeweza kudhibiti hasira zake na kuwasamehe wenzake (Quran: Surah Al-e-Imran, Ayat 133-134). Ni dhahiri Rais Magufuli alikasirika sana kusikia sauti za walivyokuwa wakimsema kwa lugha za ukakasi, lakini ameamua ‘jua lisichwe akiwa hajatoa uchungu wa maumivu’.

Rais Magufuli ameonyesha hilo, amewasamehe Nape, Makamba na Ngeleja, amesahau na amemuelekeza aliyekuwa amemkosea njia bora zaidi ya kufanikiwa. Ameonyesha kuwa hajabaki na chembe ya kinyongo, tena amemualika Ikulu kwa heshima kama mgeni wake wa heshima na sio mtu anayetaka kumpigia goti. Mwanafalsafa mmoja alisema, “dunia ingekuwa sehemu salama zaidi ya kuishi kama watu wangekuwa wanasameheana.

” Hata hivyo, Nape, Makamba na Ngeleja ambao walikosea wametufundisha somo kubwa la wazi. Kwanza, kukosea tumeumbiwa binadamu. Hata Petro ambaye alipewa hadhi na Yesu kuwa ndiye ‘Jiwe’ ambalo juu yake atajenga kanisa lake, alimkosea Yesu lakini alipojuta na kutubu alisamehewa. Marehemu Bluce Lee, Mfalme wa Karate, aliwahi kusema, “Makosa husamehewa daima, kama mkosaji atakuwa na ujasiri wa kuyakiri.” Makamba, Ngeleja na Nape walikuwa na ujasiri wa kuyakiri makosa yao na kuomba msamaha kwa dhati.

Nape amekuwa funzo zuri, ni kama Mungu amemtumia pia kutukumbusha binadamu sio tu kuomba msamaha, kuitafuta kwa dhati nafasi adhimu ya kuomba msamaha kwa tuliowakosea. “Nape amekuwa akiomba msamaha, akiandika messages (jumbe) hata usiku wa manane, alikuwa anaomba anione… anione. Hata wasaidizi wangu wamekuwa wakiliona hili,” amesema Rais Magufuli. “Amehangaika sana, ameenda hadi kwa Mzee Mangula [Philip Mangula], amefika mpaka kwa Mama Nyerere, amehangaika kweli lakini baadaye… ni katika hiyohiyo kwamba sisi tumeumbwa katika kusamehe.

Na leo umemuona asubuhi amekuja hapa, nikaona siwezi kumzuia kuniona, kikubwa anachozungumza ni ‘naomba Baba unisamehe’,” ameongeza Rais Magufuli. Wengine wasio na busara wameeleza utetezi wa kufunika makosa kuwa eti makosa yale yalifanywa kwenye faragha hivyo aliyeyafichua ndiye mkosaji!! Wanasahau kuwa hata Mungu wetu anajua kuna faragha, na Mungu pia yuko sirini.

Lakini kuwa sirini hakumpi mtu yeyote ruhusa ya kufanya makosa. Kosa ni kosa haijalishi umelifanya kwa mazingira yapi, muhimu ni kukiri, kujuta na kuomba msamaha kama walivyofanya. Kufanya kosa hakukuondolei hadhi yako endapo utakiri, kujuta na kuomba msamaha bali litabaki kuwa fundisho kwa wengine.

Kwa haya yaliyotokea ni dhahiri Rais Magufuli ameyaishi maandiko matakatifu na ameongoza kwa mfano. Tuendelee kumuombea. Tupo wengine huku mtaani, mbavu mbili tu na hata uongozi wa darasa hatujawahi kupata lakini tunavyopania kulipa visasi ni kama tuna mkataba na shetani. Tujifunze kwa rais wetu, vitabu vyote vitakatifu vinaelekeza kusamehe na kuepuka visasi.
 
Hakika hili ndilo swali linalogonga katika vichwa vya baadhi ya watu wakijiuliza namna Rais wa Tanzania Mh.Dr.John Pombe Magufuli alivyoweza kuleta maendeleo makubwa ya maajabu ndani ya kipindi cha miaka minne cha muhula wake wa kwanza.

Hebu fikiria anajenga mradi mkubwa wa kufua umeme wa Nyerere katika Bonde la Mto Rufiji, anajenga reli ya kisasa itakayotumia treni za umeme(Standard Gauge), elimu bure anatoa Bilion 23 kila mwezi kugharamia mpango huo,amenunua ndege kwa pesa taslimu ( cash Money) amejenga vituo vya afya zaidi 300 nchi nzima sambamba na vifaa tiba,hospital mpya za wilaya 67, kwenye miundombinu ya barabara ndio usiseme lami zinatandikwa nchi nzima,miradi ya maji safi na salama ipatayo 1,801ambayo mpaka sasa miradi 500 ipo katika hatua mbalimbali ya utekelezwaji, umeme Vijijini,mwendokasi awamu ya 3 Mbagala,DSM na mengineyo mengi nikisema niyaandike yote hapa sitomaliza.

Sasa hivi hakuna sehemu hata moja Tanzania ambayo Kama ukitembelea lazima ukute shughuli fulani ya maendeleo inaendelea,ama iwe mradi wa maji,umeme,barabara,ujenzi wa zahanati N.K.

Ni miaka minne ya mafanikio makubwa, ni miaka minne ya uthubutu ,utashi ,uzalendo,l na uchapakazi wa hali ya juu wa Rais Magufuli.

Tuendelee kujivunia mafanikio haya Tanzania inayopiga kwa kasi chini ya uongozi imara wa Serikali ya Chama Tawala.

Augustino Chiwinga
0621448591
 
Akifanikiwa pia na Kutuwekea Hadharani walipo akina Ben Saanane, Azory Gwanda na nani alipanga na alihusika Kumpiga Risasi na Kumjeruhi vile Mtanzania Mwenzetu Tundu Lissu bila kusahau zilipo Tsh Trilioni 1.5 nadhani hapo atakuwa amefanikiwa zaidi na tutamuimba na kumsifu kila Uchao na kuona hayo pamoja na hayo yako uliyoyataja hapa juu ndiyo Mafanikio yake makubwa ya Kujivunia.
 
Ndani ya hayo mafanikio, siku ukipata nafasi uje uanike deni la taifa limekuwa kwa kiwango gani ndani ya hiyo miaka minne ya hayo mafanikio.
 
Mwanzo wa story yako ungeanza na hakika swali linagonga katika vichwa vya Baadhi ya watu wajinga ambao hawataki kujiuliza zaidi kama wewe then ............ unaendelea sasa na story yako ya abunuwasi
 
Back
Top Bottom