Waungwana mimi naona Rais John pombe magufuli apite tu uchaguzi ujao hakuna namna na asipopita mi sikubali ntaandama peke yangu Wala sitataka sapoti ya mtu.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Mheshimiwa Rais ameanzisha jitihada kubwa za kulikomboa taifa letu kiuchumi kwani wote tunaona mabadiliko kimaendeleo, tukilinganisha na wakati uliopita. Amekuwa akitumia muda wake mwingi katika harakati za kubuni namna gani atalikomboa taifa letu na wananchi wake kutoka katika lindi la umasikini.

Tumemsikia mara kadhaa akisema kuwa wakati mwingine analazimika kulala chumbani na mafaili ili ayafanyie kazi hata usiku wa manane. Hii yote inaonyesha jinsi gani rais wetu alivyo na uchungu na nchi yetu. Kuna wakati aliwahi kusema kuwa kazi hii ( ya u-rais) ni ngumu sana, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya watu hawakumuelewa na wakatafasiri vibaya (wengine kwa makusudi), wanafikiri mtu akiwa rais, kazi yake ni kutoa amri tu, kumbe sio.

Kuna mambo mengi magumu (complex issues) unatakiwa uzifikirie kwa kina na hatimaye uzipatie suluhisho, hapo ndipo ugumu unapoanzia. Kuna masuala ya afya, maji, miundombinu n.k., yote haya kwa ujumla wake yatazame kitaifa uone changamoto zake; lakini yote haya Mheshimiwa rais ameyatekeleza kwa asilimia kubwa na bado anaendelea kutekeleza mengine.

Ni masikitiko makubwa kuona kuwa pamoja na jitihada hizi za rais wetu mpendwa kulikwamua taifa letu, kuna baadhi ya watu wameanzisha jitihada za kumkwamisha au kumkatisha tamaa ili watimize matamanio yao. Nasema matamanio yao kwa kuwa harakati zao hizo za kumkwamisha rais hazina maslahi kwa taifa, bali ni kwa maslahi yao.

Inasikitisha zaidi tunapoona kuwa watu hao ni watumishi au wamewahi kuwa watumishi katika ngazi mbalimbali. Tulitegemea watu hao wangekuwa mfano bora (role model) wa kuigwa matendo yao na wananchi wa ngazi zote kwa mustakabali wa ustawi wa taifa letu. Badala yake, watu hawa wamegeuka na kuwa kikwazo kwa rais wetu mpendwa.


Mwanaharakati mmoja aliling’amua hili na kutufahamisha wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Baadhi ya watu walimuona ni mzushi, kumbe ni ukweli mtupu na leo hii mambo hayo yamejidhihirisha. Inasikitisha sana.

Lakini wananchi tujiulize swali moja; wakati tunamchagua kiongozi wetu (rais wetu), matamanio yetu yalikuwa ni nini? Wengi watasema tulitaka atuletee maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Tumeona mheshimiwa rais amekuwa na maono makubwa sana juu ya uchumi wa taifa letu.

Leo tunashuhudia shirika la ndege (ambalo kwa kweli lilikuwa limekufa) likifufuliwa kwa kununua ndege nyingi (tena kwa fedha taslimu); Dreamliner, Airbus na bombardier huku ndege zingine tatu (za ukubwa niliotaja) zikiagizwa. Nani angeweza kutekeleza jambo hili?

Tumeshuhudia barabara nyingi zikijengwa na zingine kupanuliwa (kama hii ya Morogoro road, Kimara-Chalinze), angalia barabara za juu (fly overs) kama pale Tazara, Gerezani, hii inayojengwa Ubungo na kule Salender. Hii yote ni kuhakikisha kwamba tatizo la foleni za magari (traffic jam) katika jiji la Dar es Salaam linabakia kuwa historia.

Hata sisi huku mitaani barabara za mitaa ni nzuri; bodaboda, magari madogo na hata makubwa yanapita bila shida yoyote. Juzi nimesafiri kwa dakika 7 umbali ambao hapo awali tulikuwa tunasafiri kwa dakika 30, na hii ni kutokana na barabara kuwa nzuri. Je, haya sio maendeleo?

Usafiri wa majini ni wa uhakika, kuanzia vivuko hadi meli katika bahari na maziwa hapa nchini. Hivi juzi tu Rais alipotoka mapumzikoni Chato alienda Mwanza (akipitia Biharamulo, Katoro, Geita na Sengerema), akiwa huko, pamoja na mambo mengine, alienda kukagua ujenzi wa meli mpya.

Tuliona jinsi alivyosisitiza kukamilika kwa meli hiyo ikiwa ni pamoja na kuziagiza mamlaka zinazohusika kutoa vibali na kusaini nyaraka za kusafirisha malighafi zinazotumika kutengeneza meli zisicheleweshe. Mkandarasi alimuahidi kuwa meli hiyo itakamilika mwezi 3 mwakani. Kumbe tuona rais wetu sio wa kukaa ofisini tu, anakwenda mwenyewe kuangalia utekelezaji. Rais wetu anapiga kazi usipime!

Mheshimiwa rais wetu anatujengea reli ya kisasa (standard gauge), hii ni ya kasi kubwa ili watu (na mizigo) waweze kutekeleza majukumu yao ya kibiashara kwa haraka iwezekanavyo. Badala ya kuchelewa njiani kwa siku mbili au tatu, sasa itakuwa safari ya masaa sita tu (kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza).

Juzi tumeona garimoshi ya ya kutoka Tanga kuelelekea Moshi imefufuliwa baada ya kutotoa huduma kwa muda mrefu. Hii itarahisisha kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Tanga kuelelekea maeneo mengine ya Kaskazini. Na juzi Mheshimiwa rais akiwa njiani kuelekea Rufiji, alitoa maagizo kwa uongozi wa Tazara kuhusu ufanisi wa reli hiyo.

Hii yote ni kwamba Mheshimiwa rais anahakikisha sekta ya usafirishaji inaimarika.Tujiulize, haya sio maendeleo? Hakuna nchi(duniani) iliyoendelea bila kuipa kipaumbele sekta ya usafirishaji kwani ndio kichocheo kikubwa cha uchumi.

Mheshimiwa rais ametujengea vituo vya afya vingi sambamba na ugawaji wa madawa kwenye vituo hivyo. Wananchi angalau sasa hivi tukienda kutibiwa tuna uhakika wa kupata dawa. Hivi juzi tu kimefunguliwa kituo kipya cha afya Kimara na wananchi wanafurahia kupata huduma ya matibabu.

Mheshimiwa rais ameweza kufanikisha mpango wa elimu bure, kutoka elimu ya awali mpaka ya kidato cha nne. Tujiulize, ni nchi ngapi zimeweza kufanikisha hili? Na kwa hili tumeshuhudia watoto wengi wakiandikishwa. Hakuna nchi iliyoendelea bila kuweka kipaumbele kwenye elimu. Mheshimiwa rais aliliona hili na ndio maana akaanzisha mpango huu kabambe wa elimu bure ili watoto wetu wengi wasome bila kujali uwezo wetu kiuchumi sisi wazazi.

Leo tunashuhudia idadi ya watoto wanaoandikishwa ni mara mbili ya ile idadi ya awali. Hii ni kutokana na huu mpango wa elimu ya awali, msingi na sekondari (hadi kidato cha nne) kuwa ya bure inayoendana na upanuzi au ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Wanafunzi wa vyuo vikuu, wengi leo wananufaika na mikopo ya elimu ya juu kutoka bodi ya mikopo, tofauti na hapo awali. Hii ni kutokana na mikakati maalumu ya Mheshimiwa Rais ili kufanikisha wanafunzi wengi wafaidike na mikopo hiyo. Miaka ya nyuma wanafunzi wengi walikuwa hawawezi kusoma vyuo vikuu kutokana na ufinyu wa bajeti iliyokuwa inatolewa kwa bodi ya mikopo.

Hivyo wanafunzi wengi waliokidhi vigegezo hawakuweza kujiunga vyuo vikuu kutokana na ufinyu huo. Leo hii Mheshimiwa Rais ametenga bajeti ya kutosha ili wanafunzi wengi waliodahiliwa vyuo vikuu waweze kusoma elimu ya juu. Tunataka Rais atufanyie nini zaidi ya haya?

Nchi nzima sasa hivi; kila mkoa, wilaya au kata, kuna harakati za kuanzisha viwanda, na hii ni chachu ya maendeleo katika taifa letu. Huu nao ni mpango mkakati wa Rais wetu. Tunashuhudia viwanda vingi vinaanzishwa (hasa kanda ya Mashariki), tutaona baada ya muda mfupi masoko yetu yatatawaliwa na bidhaa zetu za ndani na bidhaa zingine tutauza nje (export). Hizi ni jitihada za Mheshimiwa Rais.

Juzi mkoani Ruvuma (kwa Mheshimiwa Christina Mndeme, Mkuu wa Mkoa), wamefanya kongamano la viwanda na fursa za uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa nje na wa ndani kuwekeza nchini. Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa waziri mkuu, Mheshimiwa Kasimu Majaliwa. Hii itatoa ajira kwa Wanaruvuma na wananchi wengine kwa ujumla.

Mheshimiwa Rais ameweza kuanzishwa kwa mradi wa umeme utokanao na maporomoko ya maji ya mto Rufiji(Stieglers Gorge) ambao uliasisiwa na Mwalimu Nyerere miaka mingi iliyopita. Mradi huo, ambao jana Mheshimiwa Rais aliweka jiwe la msingi, na kuamua kwa kauli moja na wananchi kuwa utapokamilika uitwe jina la muasisi wake (nadhani utaitwa Nyerere Hydroelectric Power), utakuwa chachu kubwa kwa maendeleo kwani viwanda vingi vitatumia nishati hiyo kwani gharama yake ni nafuu sana kulinganisha na nishati itokanayo na vyanzo vingine, kama vile injini za diesel, jua, upepo, jotoardhi, makaa ya mawe, uranium n.k Unafuu huu wa nishati utawezesha hata wananchi wa kawaida kuanzisha viwanda vidigovidogo na hata majumbani kwetu gharama ya nishati itapungua sana.

Bwawa hili sio tu litakuwa chanzo cha umeme, bali pia litatumika kwa shughuli za uvuvi, utunzaji wa mazingira, utalii n.k. Jamani, haya sio maendeleo?

Mheshimiwa Rais amekuwa mzalendo namba moja mwenye uchungu na maliasili za nchi yetu. Tumeshuhudia akizilinda rasilimali zetu kwa nguvu zake zote. Wengi tumeona anavyodhibiti madini, gesi, misitu, mito, hifadhi za wanyama za taifa n.k. Alipokuwa anatoka mapumzikoni hivi karibuni, aliwaambia wananchi wasimwage ovyo kemikali (zebaki) wanazotumia katika uchenjuaji wa madini kwani zina athali kwa uoto wa asili na pia kemikali zikiingia majini na kisha watu kunywa maji hayo, wanaweza kupata saratani.

Aliwashauri pia wapande miti ili kutunza mazingira. Jana tena akiwa anaweka jiwe la msingi, aliwaagiza viongozi wa wizara ya maliasili kuligawa eneo la Selous na kupatikana hifadhi ya taifa itakayoitwa Nyerere National Park. Kuhusu upande wa madini, tumeona mikataba ya madini imepitiwa upya na baadhi ya vipengele vimerekebishwa ili wawekezaji wasijinufaishe peke yao, bali pawe na faida pande zote mbili (win win situation) ili mwisho wa siku hawa wawekezaji watakapomaliza madini na kuondoka zao wasituachie mashimo tu bila faida yoyote.

Mheshimiwa Rais kaanzisha masoko ya madini nchi nzima ili sasa madini tunayochimba yauzwe ndani ya nchi na faida yake (mzunguko wa fadha) itumike hapahapa nchini. Hii pia itasaidia kutunza takwimu za mauzo (sales data) kwa ajili ya marejeo ya aina yoyote ile hapo baadaye.

Jitihada za Rais katika kudhibiti madini zimedhihirika tena pale dhahabu kilo 35 na shilingi milioni 500 zilipokamatwa uwanja wa ndege wa huko Kenya. Hizi ni jtihada za Mheshimiwa Rais, na tayari fedha hizo pamoja na zile zitakazopatikana baada ya dhahabu iliyokamatwa kuuzwa, amezielekeza katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Fuga (railway station) mpaka Nyerere Hydroelectric Power Station.

Mheshimiwa Rais, wananchi wanatambua jitihada zako katika suala zima la kuwaletea maendeleo. Hata hawa wanaokupinga sio kwamba hawatambui, ila wanafanya hivyo kwa maslahi (interest) yao. Na pengine nia yao ni kukupa hofu au kukukatisha tamaa. Lakini Rais wetu, kwa bahati nzuri, wewe moja ya taaluma zako ni ualimu, kwa hivyo una saikolojia ya hali ya juu na ndio maana hubabaiki kwa kuwa unajua maana ya kila wafanyalo.

Rais wetu mpendwa piga kazi, wananchi tupo pamoja na wewe. Sisi wananchi ndio tuliokuchaguwa wewe uwe kiongozi wetu na kwa hivyo una kibali mbele ya Mwenyezi Mungu, kwani sisi tuliokuchaguwa ni wa Mwenyezi Mungu.

Musa aliwaongoza wana wa Israel kutoka utumwani Misri kwenda nchi ya ahadi, Mheshimiwa Rais, utuongoze Watanzania katika zama hizi tunapongia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda. Tunazidi kukuombea kwa Mwenyezi Mungu.

HAPA KAZI TU.
 
Tusipende kuishi kwa ushabiki kwan maendeleo upimwa kwa namna mtu anavyo ishi na sio namna serikali inavyo ona

Oja yako namba moja ina mashiko ila sio elimu bora n elimu ilimrad watoto waende shule

2-ukiwa wasema kitu sema kwa fact 1.5T zipo wap police walio kamatwa na kuachiwa kuhusu dhahabu ule sio ofisad?

3-mauaji ya kibiti ujawai sikia na kuhusu watu kutekwa na kusemekana wanajiteka ni sahihi unabid utambue wewe mwenyewe ulivyo apo n rasili mali unabd kuwaza iliwa kwako je itakuaje?

5- ningependa kutambua umesha fanya safari kwa kutumia izo ndege kwa mara ngap? Ndege inafanya kazi n moja tu ndio iyo itoke dar ipite KIA iende entebe irud chukua watu kia irud dar na hapo watu walikata tiket ya mchana wanakuja chukuliwa saa mbili usiku na sio mara moja n mara kibao wengne ilisha tugarmu mpaka kukata tiket zingne zaid ya mara tatu,ndege mnasafiri watu kum apo unazani faida ipo wap?

6- sawah uchumi wa maneno ila sio uchumi wenye pumzi tunao uona kila siku dollar inapanda yuan inapanda leo ihii tuan ipo 347 kutoka 330 enzi ya mzee wetu kikwete uchumi umepanda kwenye midomo ya vibaraka au kwenye nn?

8-ameweka jiwe la msingi na sio kujenga hamna mradi mkubwa ata mmoja unaoweza kamilika ndan ya muda mchache iyo treni ataendesha kwa kitu gan umeme wetu binafsi majumban unakatika iyo tren itaendeshwa kwa kitu gan? Tusipende kushadadia ila tuwaze kwa mapana sana

9- mapato ya kuumiza watu n sawa na watu awawez kutumia ela kama mwanzo sababu wanajua kuzipata n shida ila ukiangalia watu wake wote wakarbu wanavyo zitumia hapo bado ufisad upo

10 ni plan ila bado aijatekelezwa na kuwa na plan n jambo jema utekelezaji je?

11 nimekuja tambua kuwa ujawai zunguka na kuona unacho kisema izo sio flyover ila ni kama madaraja tu ya kawaida sana zunguka nchi za wenzetu utaona maana ya flyover na sio ivyo vidaraja vya juu

12- madawa ya kulevya yako pale pale semawanafanya watu wa juu sio kila mtu anafanya saiv

13- aina ukwel wowote dawah hospital azipo juzi tu hapo tuna ambiwa tukanunue madumu ya drip nje hosp yameisha ndio kaborasha nn embu tuanze ulimbuken

14 hapa ni uongo mfano mzur n uhuru wa kujieleza n nan anaeweza mkosoa adharan akabaki salama au ulivyokuwa wa andika ihii point ukuwaza

15 mshikamano gan wakat wawekezaj kila leo wanaondoka kila leo kuja jipya kuhusu nchi yetu na mataifa mengne kama ndege tu kuanza safari ya south na kutoshusha watu hapo uhusiano gan mzuri upo labda wa East African ndio useme ivyo ila sio mataifa mengne

Kwenye umeme kukatika umetukosea sana ndugu! Umeme kukatika kumepungua kwa 98% siku hizi ukiulizwa umeme ulikatika lini unaweza ushindwe kukumbuka. Mimi pamoja na kuwa nipo kariakoo iliyodorora lakini bado nakubali kuwa Rais Magufuli ni Rais sahihi sana kwa Taifa letu ila namwombea asikatishwe tamaa na hizi lawama , hasa kwenye Madini asilegee hata kidogo , endelea kuwabana Barick na makampuni mengine hadi kielweke , angalau madini yaweze kuchangia pato la Taifa.
 
Uwanja wa ndege upanuzi umeanza siku nyingi ni ufunguzi tu, fly over zimejengwa wakati wa Kikwete ni umaliziaji na pesa za world bank, daraja la salenda linajengwa kwa msaada wa korea walisema haya kuanzia wakati wa kikwete. Ndege ndiye kanunua yeye barabara ya Dar Moro ilianza zamani lakini wamesimamisha. Treni ilianza zamani wakaiharakisha lakini mradi ulikiwepo. Mradi wa umeme umeanza lakini ndiyo umeanza tu...... naona mna kuza mambo kuliko yalivyo hiyo miradi haijakamilika na mingi sio yake. Shule bure ndiyo mradi wake pekee na mabweni yaani raisi kujenga mabweni yawe agenda wakati wenzake waligenga chuo cha Dodoma kizima na plan zote wanafunzi 40,000 wenzake waliweka pipeline ya gas,
Mkuu are you serious ???
Hauko serious kabbisa.
Vipi kuhusu Ubungo interchange??
Ile fly over ya mfugale ni awamu ya tano.
Mradi wa daraja la kigamboni na muhimbili cardiac institute ndio awamu ya kikwete.
 
Mkuu are you serious ???
Hauko serious kabbisa.
Vipi kuhusu Ubungo interchange??
Ile fly over ya mfugale ni awamu ya tano.
Mradi wa daraja la kigamboni na muhimbili cardiac institute ndio awamu ya kikwete.

Watanzania wengi hasa wadogo ni mbumbumbu daraja la salenda linajenga kwa msaada wa south Korea, fly over zote ni pesa ya bank kuu ya dunia na walianza toka zamani ukiona daraja leo planning imeanza zaidi ya miaka 5. Airport imejengwa kwa miaka mingi tu😂 lakini ndiyo inaisha. Hata treni plan haikuanza leo na plan ilikuwepo mpaka ya kujenga treni upande wa mtwara na lindi. Hebu tuletee budget ya serikali utuambie hizo fly over wamelipa lini😂 pumba tu
 
Mkuu are you serious ???
Hauko serious kabbisa.
Vipi kuhusu Ubungo interchange??
Ile fly over ya mfugale ni awamu ya tano.
Mradi wa daraja la kigamboni na muhimbili cardiac institute ndio awamu ya kikwete.

Fanyeni shughuli vijana badala ya kushinda mitandaoni tu wakati hamna kitu mifukoni nchi ni maendeleo ya vijana msisubiri serikali pekee na ushabiki kwenye kila kitu kidogo kinachojegwa ni mambo ya kawaida
 
Fanyeni shughuli vijana badala ya kushinda mitandaoni tu wakati hamna kitu mifukoni nchi ni maendeleo ya vijana msisubiri serikali pekee na ushabiki kwenye kila kitu kidogo kinachojegwa ni mambo ya kawaida
Waambie wasio nazo.
Maana mm nina maendeleo ya baba na mama wameniandalia.
Bado yangu nayaongezea.
Kwahiyo usione twashinda net ukadhan hoe hae.
Huwez kumkuta msomali Tz anakufa na njaa.
 
Ukitaka kujua nchi imetulia kwa sasa baada ya rais Magufuli kuingia madarakani 2015, tofauti na kikundi cha watu wachache ambao mirija yao imezibwa ,wakitumia kichaka cha kujiteka na kiupakazia serikali.
Hata hivyo drama hii imeshindwa ku-hit kama kigenge hiki kilivyotarajia.

Yafuatayo ni matukio sugu hayapo kwa sasa na ni kiashiria tosha kwamba nchi inaendeshwa kwa ustadi na umakini

1-Hakuna migomo ya wafanyakazi na maandamano ya mara kwa mara ,wafanyakazi wako bize kutoa huduma kwa jamii

2-Hakuna migomo na maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu mara kwa mara kama ilivyokua awali.mikopo inatoka kwa wakati na hakuna upendeleo

3-vurugu za maandamano na uporaji wa vyama vya upinzani ulioshamiri kila uchao ,yamekoma

4-ujambazi rate inmeshuka sana

5-utapeli na udhulumati wa wazi rate imeshuka .

Mengine ongeza na wewe

Hakuna kweli hata moja, wewe ni moja ya wale waongeao bila kushirikisha bongo
 
Habari wanabodi,

Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wote wanabodi.

Ni kwamba kumekuwa na tuhuma nyingi sana za ajabu na kijinga ambazo hazina hata miguu ya kusimamia kwamba Mr. President ameshindwa kuiongoza nchi na kusababisha mpasuko katika chama cha CCM.

Hakika uamini usiamini hizo tuhuma zimekuwa zikitolewa na wanachama ambao ni wapigaji ambao ile mizizi yao ya upigaji imekatwakatwa na kutupwa baharini. Hivyo basi, kwa sababu ya kuzibwa ile mianya ambayo waliitumia kuwaibia wananchi wake leo hii wameamua kuja na tuhuma ambazo hazina mashikohata kidoo ili waonekane wao ni bora sana kuliko Mr. President.

Mr. President ukimuondoa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere hakuna Rais mwingine aliyeweza kutokea mwenye uwezo mkubwa na akili kubwa kama wewe. Mbali na uwezo wako mkubwa, wewe ni Rais mbunifu sana tumeshuhudia ubunifu wa hapa na pale mfano ni pale ambapo ulipoanzisha akaunti ya pamoja y kukusanya mapato ya taifa. Huu ubunifu umeweza kuzuia upigaji wa fedha za umma kwa asilimia 85/%.

Kadhalika, Mr. President, wewe ni mfano mkubwa wa kuigwa ulipoanzisha mapambano dhidi ya wahujumu uchumi wala rushwa kitu ambacho hakuna Rais yoyote aliwahi kufanya hiki kitu bali kuna ambao walibariki hayo mambo kama yalivyotajwa hapo juu.

Pia, tumeshuhudia miradi mikubwa sana kujengwa katika taifa letu kwa muda mchache sana tena kwa fedha za watanzania ambazo zinatokana ukusanyaji wa kodi. kiukweli hili jambo linathibitisha uwezo wako mkubwa katika utawala. Tangu nchi hii ipate uhuru hapjawahi kutokea miradi mikubwa ya namna hii.

Aidha, kwa muda mchache uliweza kununua ndege kitu ambacho pia kimesababisha uonekane shujaa katika taifa na kimataifa kwa ujumla.

Mr. President umeweza kuondoa akili mgando kwa baadhi ya watanzania kwamba Maisha mazuri ni lazima upate ajira. Umeweza kuwaonesha kwamba Maisha siyo kuajiriwa serikalini tu bali hata kujiajiri ni jambo la msingi sana.Hii ni jambo la kishujaa sana kwani leo hii vijana wako wanapambana sana na kufanya kazi kwa bidi ili waweze kujiajiri wenyewe. Indeed, unastahili pongezi sana.

Mr.president huwa unaenda mbali sana kwa kuwaadhibu viongozi wazembe na wasiojitambua na ambao wanashindwa kwendana na falsa yako ya Hapa kazi. kwa hili hakuna pingamizi kwani watanzania tumeshuhudia ukiwaadhibu hao viongozi kwa sababu ya uzembe wao na kukosa uzalendo kwa taifa. Mr. President hongera sana kwa kunapenda sana viongozi wanaojibika wenye kujituma na wabunifu.

Mr. President unastahili pongezi kwa kuhakikisha watoto wa watanzania wanapata elimu bure.Ingawa kuna changamoto yingi sana katika hili jambo, umejitahidi sana kwa hili na hizi changamoto zitaisha tu kwani hakuna changamoto ambayo inaweza kuwa ya milele bali changamoto hutokea tu kwa kipindi kifupi. Pia kumbuka hakuna jambo lisilokuwa na changamoto.

Mr. President ninakuomba ukiwa kama baba wa cha cha CCM hakikisha wanachama wenye nia mbaya na chama chako na kwa taifa kwa ujumla. Wanachama wako wengi wao walizoea vya kunyongwa leo hii wanapata shida sana kula vilivyochinjwa. Walipenda sana mtelezo bila kufanya kazi. Leo hii wanataka kutuaminisha kwaamba wao ni wasafi kuliko wewe. Kitu ambacho ni uongo mtupu.

Tumekuwa tukiwashuhudia wakifanya madudu mengi sana na kupelekea wananchi wao kuteseka, watu ambao walikosa huruma na uzalendo kwa wananchi na kwa Taifa leo hii wanataka kutuaminisha kuwa wao ni wasafi. Usafi huo wameutoa wapi? wanachuki binafsi
dhidi ya utendaji kazi wako uliojaa weledi na ubunifu mkubwa sana. Walishindwa nini tangu zamani kuwa wazalendo ila wanataka kutuaminishia leo hii kuwa wanapenda nchi hii?

Mr. President, wewe nimti wa matunda, kumbuka ule usemi kwamba mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe. Huwezi kuona mti ambao hauna matunda ukirushiwa mawe hata siku moja. Mbali na hili, chuki zao binafsi na lawama zao ambazo hazina miguu wala kichwa usikubali vikuyumbishe.

NB. Kila mtu ana mapangufu yake ingawa mazuri aliyoyafanya Mr. President yanafunika/yamefunika mapungufu yake yote katika utendaji kazi wake.

Mr. president hii ni Summary ya mambo makubwa uliyofanya kwa taifa letu.

1. Kujenga miradi mikubwa mfano Stigler's Gorge project, Ujenzi wa barabara ya Agakhan to Masaki, Flyover, Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni.

2. Kuanzisha mahakama maalum za kushughulikia ufisadi na kuwafunga wahujumu uchumi.

3. Kuanzisha akaunti ya taifa ya pamoja kwa ajili yakutunza mapato.

4. Elimu bure kwa Watanzania.

5. Kuhimiza suala la uzalendo nchini.

6. Ununuzi wa Ndege.

7. Kuondoa safari za nje ya nchi ili kupunguza matumizi mabaya ya kodi za wananchi.

8. Ujenzi mkubwa wa uwanja wa ndege.

9. Serikali kuhamia mkoani Dodoma.

10. Dhana ya kujiamini na kuthamini vya kwetu na siyo vya wazungu.

11. Kuhamasisha watanzania kufanya kazi na waache maisha ya uvivu, uzembe na kupenda mtelezo(Falsafa ya hapa kazi tu)

Karibuni Tumpongeze Mr. President kwa mapinduzi na mafanikio makubwa nchini. Ingawa kuna watu wenye chuki zao binafsi watapinga hili suala kwa hoja nyepesi na ambazo hazina kichwa wala miguu.

Utapata tabu sana kung’arisha kisicho ng’ara. Sisi wananchi tunataka kuona uchumi ukikua na mchikamano wa nchi, hizi ngonjera/poroje zote hazina mana kama nchi hali ni tete hivi.
 
Mimi Ngajapo kwa akili niliyopewa na mwenyezi mungu na kuongeza kidogo elimu ya dunia (digrii) niliyonayo na akili niliyopata kutokana na mwenendo wa kimaisha. ni vigumu na haitawezekana kuniaminisha kwamba eti viongozi wa CCM waliopita wana ubora au unafuu katika uongozi kuliko Magufuli???? never ever!!!!

Hao viongozi waliopita mnaowasifia eti walikuwa bora kuliko Magufuli labda walikuwa wajomba zenu au mlikuwa mna maslahi nao lkn mimi nakataa hamtaniaminisha hata siku moja ili niwakubalie hoja zenu. Na sitaki niandike mengi lakini kila mmoja anajua udhaifu wao katika kusimamia rasilimali za taifa.
-Hao kila siku walikuwa wanafikiria kugawana rasilimali za nchi
-Nchi ilibaki ukiwa kama vile haina viongozi wa kitaifa.
-Muelekeo wa maisha ulikuwa mbovu, tulikuwa hatujui hatma ya maisha tunakolelekea.
-Viongozi wakati wote ni kufanya sherehe huku umaskini ukitamalaki kwa watanzania ukijaribu kupaza sauti unambiwa una wivu.
-Mjinga ndio anayemuongoza msomi, mfano bunge lijalo kama sio magufuli tungejikuta tunaongozwa na standard seven na wasanii ambao hata kutunga sera za nchi hawewezi zaidi ya porojo na vichekesho bungeni.

mambo ni mengi yalikuwa hovyo mno....acha tu magufuli abadilishe ili tuende sawa.

Jiwe unayemsema ndiye chanzo cha matatizo makuu nchini
 
Waambie wasio nazo.
Maana mm nina maendeleo ya baba na mama wameniandalia.
Bado yangu nayaongezea.
Kwahiyo usione twashinda net ukadhan hoe hae.
Huwez kumkuta msomali Tz anakufa na njaa.

Tumia muda kujifunza maana madogo wa siku hizi mnaingia kwenye mijadala na kutoa pumba tu
 
10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...
Muanzisha uzi, kwa kuwa huu uzi umefika page zaidi ya 1,2000, ili anayeufungua leo aweze kupata kuyajua makubwa aliyoyafanya Rais Magufuli ungeyachukua kuyaweka kwenye updates za post yako ya kwanza.
 
Naipenda sana nchi yangu, kwani ni nchi inayoongozwa kwa utawala bora.


Nchi yangu sasa tuna ndege za kutosha.

Barabara za juu na chini ambazo zinaendelea kujengwa.

Reli ya umeme ambayo pia inaendelea kujengwa.

Viwanda vingi vimejengwa na vingine vinaendelea kujengwa.

Wasomi wameongezeka na wengi wameajiriwa.


Nitakipenda zaidi Chama changu

Kwani kimefanya mambo mengi mno.
 
Umesahau majeruhi wa ajali ya tanker iliyotokea morogoro wanalamba laki ,tano cash..😛😜😜
 
Back
Top Bottom