Jpm kiboko sana huyu jamaa watu kimya
Lazima watu wawe kimya hasa baada ya waziriu wake kutamka hadharani kwamba Azory Gwanda amekufa (soma: ameuawa)! Watu lazima wawe kimya kwa sababu wanaogopa kuuawa kama alivyouawa Azory Gwanda! Watu lazima wawe kimya kwa sababu wanaogopa kumiminiwa mvua ya risasi kama alivyomiminiwa Tundu Lissu! Lazima watu wawe kimya kwa sababu wanaogopa kupotezwa kama alivyopotezwa Ben Saanane! Watu lazima wawe kimya kwa sababu wanaogopa kutekwa na kuachiwa baada ya kutoa pesa mingi kama ilivyokuwa kwa Mo Dewji!

In short, lazima watu wawe kimya kwa sababu wanajua the devil family is running the country! The devil family that loves blood over water!
 
10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...

Uwanja wa ndege upanuzi umeanza siku nyingi ni ufunguzi tu, fly over zimejengwa wakati wa Kikwete ni umaliziaji na pesa za world bank, daraja la salenda linajengwa kwa msaada wa korea walisema haya kuanzia wakati wa kikwete. Ndege ndiye kanunua yeye barabara ya Dar Moro ilianza zamani lakini wamesimamisha. Treni ilianza zamani wakaiharakisha lakini mradi ulikiwepo. Mradi wa umeme umeanza lakini ndiyo umeanza tu...... naona mna kuza mambo kuliko yalivyo hiyo miradi haijakamilika na mingi sio yake. Shule bure ndiyo mradi wake pekee na mabweni 😂 yaani raisi kujenga mabweni yawe agenda wakati wenzake waligenga chuo cha Dodoma kizima na plan zote wanafunzi 40,000 wenzake waliweka pipeline ya gas, 😂
 
He's already mess it up and screws our economy...KAZI ipi tena apige...akae pembeni Kesha feli completed
Man our treasurery is full of cash come sun come rain, the money you used to swindle is no more, all swindlers have same talk because they have nothing to swindle before being swindled.
 
Habari wanabodi,

Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wote wanabodi.

Ni kwamba kumekuwa na tuhuma nyingi sana za ajabu na kijinga ambazo hazina hata miguu ya kusimamia kwamba Mr. President ameshindwa kuiongoza nchi na kusababisha mpasuko katika chama cha CCM.

Hakika uamini usiamini hizo tuhuma zimekuwa zikitolewa na wanachama ambao ni wapigaji ambao ile mizizi yao ya upigaji imekatwakatwa na kutupwa baharini. Hivyo basi, kwa sababu ya kuzibwa ile mianya ambayo waliitumia kuwaibia wananchi wake leo hii wameamua kuja na tuhuma ambazo hazina mashikohata kidoo ili waonekane wao ni bora sana kuliko Mr. President.

Mr. President ukimuondoa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere hakuna Rais mwingine aliyeweza kutokea mwenye uwezo mkubwa na akili kubwa kama wewe. Mbali na uwezo wako mkubwa, wewe ni Rais mbunifu sana tumeshuhudia ubunifu wa hapa na pale mfano ni pale ambapo ulipoanzisha akaunti ya pamoja y kukusanya mapato ya taifa. Huu ubunifu umeweza kuzuia upigaji wa fedha za umma kwa asilimia 85/%.

Kadhalika, Mr. President, wewe ni mfano mkubwa wa kuigwa ulipoanzisha mapambano dhidi ya wahujumu uchumi wala rushwa kitu ambacho hakuna Rais yoyote aliwahi kufanya hiki kitu bali kuna ambao walibariki hayo mambo kama yalivyotajwa hapo juu.

Pia, tumeshuhudia miradi mikubwa sana kujengwa katika taifa letu kwa muda mchache sana tena kwa fedha za watanzania ambazo zinatokana ukusanyaji wa kodi. kiukweli hili jambo linathibitisha uwezo wako mkubwa katika utawala. Tangu nchi hii ipate uhuru hapjawahi kutokea miradi mikubwa ya namna hii.

Aidha, kwa muda mchache uliweza kununua ndege kitu ambacho pia kimesababisha uonekane shujaa katika taifa na kimataifa kwa ujumla.

Mr. President umeweza kuondoa akili mgando kwa baadhi ya watanzania kwamba Maisha mazuri ni lazima upate ajira. Umeweza kuwaonesha kwamba Maisha siyo kuajiriwa serikalini tu bali hata kujiajiri ni jambo la msingi sana.Hii ni jambo la kishujaa sana kwani leo hii vijana wako wanapambana sana na kufanya kazi kwa bidi ili waweze kujiajiri wenyewe. Indeed, unastahili pongezi sana.

Mr.president huwa unaenda mbali sana kwa kuwaadhibu viongozi wazembe na wasiojitambua na ambao wanashindwa kwendana na falsa yako ya Hapa kazi. kwa hili hakuna pingamizi kwani watanzania tumeshuhudia ukiwaadhibu hao viongozi kwa sababu ya uzembe wao na kukosa uzalendo kwa taifa. Mr. President hongera sana kwa kunapenda sana viongozi wanaojibika wenye kujituma na wabunifu.

Mr. President unastahili pongezi kwa kuhakikisha watoto wa watanzania wanapata elimu bure.Ingawa kuna changamoto yingi sana katika hili jambo, umejitahidi sana kwa hili na hizi changamoto zitaisha tu kwani hakuna changamoto ambayo inaweza kuwa ya milele bali changamoto hutokea tu kwa kipindi kifupi. Pia kumbuka hakuna jambo lisilokuwa na changamoto.

Mr. President ninakuomba ukiwa kama baba wa cha cha CCM hakikisha wanachama wenye nia mbaya na chama chako na kwa taifa kwa ujumla. Wanachama wako wengi wao walizoea vya kunyongwa leo hii wanapata shida sana kula vilivyochinjwa. Walipenda sana mtelezo bila kufanya kazi. Leo hii wanataka kutuaminisha kwaamba wao ni wasafi kuliko wewe. Kitu ambacho ni uongo mtupu.

Tumekuwa tukiwashuhudia wakifanya madudu mengi sana na kupelekea wananchi wao kuteseka, watu ambao walikosa huruma na uzalendo kwa wananchi na kwa Taifa leo hii wanataka kutuaminisha kuwa wao ni wasafi. Usafi huo wameutoa wapi? wanachuki binafsi
dhidi ya utendaji kazi wako uliojaa weledi na ubunifu mkubwa sana. Walishindwa nini tangu zamani kuwa wazalendo ila wanataka kutuaminishia leo hii kuwa wanapenda nchi hii?

Mr. President, wewe nimti wa matunda, kumbuka ule usemi kwamba mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe. Huwezi kuona mti ambao hauna matunda ukirushiwa mawe hata siku moja. Mbali na hili, chuki zao binafsi na lawama zao ambazo hazina miguu wala kichwa usikubali vikuyumbishe.

NB. Kila mtu ana mapangufu yake ingawa mazuri aliyoyafanya Mr. President yanafunika/yamefunika mapungufu yake yote katika utendaji kazi wake.

Mr. president hii ni Summary ya mambo makubwa uliyofanya kwa taifa letu.

1. Kujenga miradi mikubwa mfano Stigler's Gorge project, Ujenzi wa barabara ya Agakhan to Masaki, Flyover, Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni.

2. Kuanzisha mahakama maalum za kushughulikia ufisadi na kuwafunga wahujumu uchumi.

3. Kuanzisha akaunti ya taifa ya pamoja kwa ajili yakutunza mapato.

4. Elimu bure kwa Watanzania.

5. Kuhimiza suala la uzalendo nchini.

6. Ununuzi wa Ndege.

7. Kuondoa safari za nje ya nchi ili kupunguza matumizi mabaya ya kodi za wananchi.

8. Ujenzi mkubwa wa uwanja wa ndege.

9. Serikali kuhamia mkoani Dodoma.

10. Dhana ya kujiamini na kuthamini vya kwetu na siyo vya wazungu.

11. Kuhamasisha watanzania kufanya kazi na waache maisha ya uvivu, uzembe na kupenda mtelezo(Falsafa ya hapa kazi tu)

Karibuni Tumpongeze Mr. President kwa mapinduzi na mafanikio makubwa nchini. Ingawa kuna watu wenye chuki zao binafsi watapinga hili suala kwa hoja nyepesi na ambazo hazina kichwa wala miguu.
 
Subiri watu na matumbo yao yenye harufu za kifisafi waje hapa. Siku hizi wamesi sana kwenda ikulu kutafuta madili.
 
Ninachokiona wakati huu ni kwamba kila mtu anapambana kujiondoa kwenye mikono ya sheria na wanaamua kutumia wananchi Kama ngao kwa sababu wanajua udhaifu wa watanzania katika kuchanganua mambo.kuna watu walijimilikisha nchi hii na wakaamini kwamba ni wao tu na vizazi vyao wanastahili neema zote za nchi hii,so anapojotokeza mtu tena ambae wanaamini walimuweka wao na hivyo ataenenda kwa maelekezo yao wanapoona anawageuka na kusimama katika misimamo tofauti na wao.....ndio hivyo yanatokea yanayotokea.kwa wakati huu,hakuna anayejua yanayofanyika sirini kama jpm na sababu kwa wenye akili inajulikana!!!so it's better mkakubaliana na ukweli kuliko kupingana naye,at least kwa kipindi ambacho yupo madarakani kwa sababu Kama pande zote zikitoka hadharani kutafuta simpathy ya wananchi trust me guys upande wenu ndio utapoteza zaidi na msishangae mawe haya anayorushiwa jpm yakaelekezwa kwenu tena kea speed ya hatari!!!
 
Sawa mkuu.
 
ASIPONGEZWE KWA SABABU ZIFUATAZO

1. Kujenga miradi mikubwa mfano Stigler's Gorge project, Ujenzi wa barabara ya Agakhan to Masaki, Flyover, Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni.
MAJIBU:Stigler's gorge ni mradi utakaoleta hasara kubwa sana kwa kuzazi chetu na kinachokuja. Huu mradi siyo mara ya kwanza unaendeshwa. Wazungu walishaanza kupeleka mpaka vifaa kabisa miaka ya 80 kwenda 90. Ila walipoofanya study ya madhara ya kimazingira na na uchambuzi wa hasara na faida (cost/benefit) wakaona ni ujinga kuendelea na huo upuuzi, wakajitoa wakakimbia. Mpaka sasa wao wanaona ni ujinga kwa nchi kutumbukiza matrilioni ya pesa kwenye hilo limradi ambali halitaweza kuzalisha hizo megawati wanazotudanganya watazalisha. HAPA NAKUPA POLE WEWE UNAYESHABIKIA MRADI HUU.

2. Kuanzisha mahakama maalum za kushughulikia ufisadi na kuwafunga wahujumu uchumi.
MAJIBU: Tangu tuanzishiwe hii mahakama, hakuna kesi ya maana ya ufisadi iliyorindima na kufikiwa kwa hukumu. Ni afadhali pale Kisutu walipopelekwa akina Yona na Mramba na wakapata hukumu yao. Hii mahakama imeendelea kuwa mahakama kivuli, huku tukisikia drama za kesi za kuhujumu uchumi na kufutiana mashtaka bila kueleweshwa ni nini kipo nyuma ya haya mambo mapya ya kufutiana mashtaka bila kuelewa kama wananchi ni kwanini na ni nini faida au hasara kwa nchi za kuwafutia mashtaka. HAPA NIKUPE POLE WEWE MWANANCHI AMBAYE KODI YAKO IMEPOTEA BURE.

3. Kuanzisha akaunti ya taifa ya pamoja kwa ajili yakutunza mapato.

MAJIBU: Uanzishwaji wa akaunti ya pamoja ni jambo jema ambalo lilipaswa kupongezwa. Tatizo la uanzishaji wa hii account ni kuwa imekuwa kama personalized issue. Rais anajitwalia mamlaka ghafla na kuagiza anayotaka huku akiwafaanya watekelezaji wa sera walio chini kama makondoo yasiyopaswa kutumia mamlaka yaliyokasimishwa kwao kama taasisi. Tumeshuhudia rais akiagiza mambo yanayopingana na sera zake mwenyewe. Mara anasema hili, mara kesho anawageuka watekelezaji wa sera na kuwalaumu kwa kutotumia akili. Hapa ningempongeza kama kungekuwa na sera nzuri zilizo rafiki kwa ufufuaji wa bishara. Mawaziri wahusika angewapima pia kwa uwingi na aina za biashara mpya zilizoanzishwa na impact ya hizo biashara kwa maisha yetu sisi raia. POLE SANA.

4. Elimu bure kwa Watanzania. : KAJITAHIDI KIDOGO

5. Kuhimiza suala la uzalendo nchini.: HAKUNA PONGEZI

MAJIBU: Uzalendo anaohimiza ni wa kujiunga na CCM hata kwa gharama ya ufujaji na utapanyaji wa kodi za wananchi ambazo alipaswa kuzilinda kwa weledi mkubwa sana. Yeye anahimiza uzalendo wa kijinga kabisa. Akikaa huko ikulu anajiona kama Mungu. Anafikiri uzalendo ni watu kumsujudia na kumlamba viatu. HAPA POLE SANA.

6. Ununuzi wa Ndege.: HAKUNA PONGEZI
MAJIBU:
Kati ya mambo aliyofanya na yameshaligharimu taifa kifedha na yatakyoendelea kuligharimu taifa ni haya maamuzi ya kununua midege bila mpango wa biashara. Hasara zinazopatikana ni moja tu ya gharama ambazo zitaendelea kututesa sisi wananchi kwa kushindwa kupata mlo, kushindwa kujitibu, kushindwa kusomesha watoto wetu elimu bora nk.
Pamoja na ushauri mzuri sana aliokuwa anaupata kutoka kwa wazoefu, yeye alijivika roho ya kibri na kukimbilia kununua ndege kwa cash kinyume na biashara yoyote inayoendeshwa hapa duniani. Watu wanakufa njaa wewe unakimbilia kuchota pesa ukanunue ndege kwa cash. HAPA NAPO HAKUNA PONGEZI.

7. Kuondoa safari za nje ya nchi ili kupunguza matumizi mabaya ya kodi za wananchi. KAJITAHIDI KIDOGO

8. Ujenzi mkubwa wa uwanja wa ndege. : UWANJA WA DAR NI JK, CHATO NI UPUUZI MTUPU
MAJIBU: Kama unamaanisha Chato - nakupa pole. Chato hakutakuwa na hizo biashara za watalii anazofikiri zitafanyika. Hapo analazimisha tu, ila hayo mambo ya kuhamisha mpaka wanyama yatamgeukia usoni na itakula kwake mara mia. Kwetu wananchi imeshakula kwetu kuanzia tumchague mwaka 2015, na itaendelea kula kwetu mpaka atakapoondoka madarakani. HAPA NAITA MAAMUZI MABOVU KABISA NA UPUUZI KUWEKA INT. AIRPORT CHATO.

9. Serikali kuhamia mkoani Dodoma. :HAKUKUWA NA SABABU, KULITAKIWA UTAFITI WA RE-STRUCTURING GOVERMENT ORGANIZATION AND STRATEGIC RE-LOCATION
MAJIBU: Strategic relocation ingewezesha kuwa na realistic positioning ya wizara na taasisi mbalimbali za serikali. Mfano, mataasisi ya fedha yangebakia Dar kama financial hub ya nchi. Makampuni makubwa ya Serikali yangewekeza kuwa na headquaters Dar. Hata Rais angeweza kubakia Dar, huku Waziri Mkuu akihamia Dodoma na zile wizara zinazoshughulika na mambo ya kiujumla ya Tanganyika. Uhamaji huu pia ulitakiwa uakisi mfumo mpya wa kikatiba ambao tunataka kuwa nao kama nchi. Rais alikurupuka sana kukimbilia kuhama bila kuangalia mifumo mipya ambayo tutakuwa nayo siku za usoni. HAPA NAMPA ZERO KWA KUKURUPUKA.

10. Dhana ya kujiamini na kuthamini vya kwetu na siyo vya wazungu. : HAMNA KITU. HUU NI UONGO. BADO TUNAABUDU WAZUNGU. ANGALIA KAZI KUBWA KUBWA NA ZA KATI WANAPEWA AKINA NANI KAMA SIYO WACHINA NA WAZUNGU. ZAIDI AMEANGAMIZA HAWA WALE WAZAWA WALIOKUWA WANAJITAHIDI.

11. Kuhamasisha watanzania kufanya kazi na waache maisha ya uvivu, uzembe na kupenda mtelezo: KAZI HAZIHAMASISHWI. AJIRA SIYO KUHAMASISHA. NI KUWEKA MIPANGO NA MIKAKATI INAYOTEKELEZEKA YA PRIVATE SECTOR KUAJIRI WANAOSOMA. MFANO SIKU HIZI NAFASI MOJA YA AJIRA WANAPELEKWA WATU ZAIDI YA 500 UWANJA WA TAIFA KUFANYA USAILI. NI AIBU KWA RAIS WA NAMNA HII.

HITIMISHO:
Tuachane na propaganda za kujifanya tunampongeza rais huku tukiwa nje huko tunajadiliana jinsi anavyoharibu uchumi na maisha ya watu. Tumshauri kwa uwazi na ukweli. Watu na vyombo vya habari viwe huru kujadili kwa uwazi hali yetu na mafanikio yetu, bila kusahau kusema wazi pale tunapokwama. Siyo dhambi watu kuja na mawazo mbdala.
 
Back
Top Bottom