10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...
Shida ya one-man show. Yaani yeye anahusika na barabara za huko ndani ndani kwa Mkoyoyo, mpaka kwenye koro-show na mbaazi za mashangazi wa Majaliwa na Nape. Ndiyo maana huwa anajifananisha na malaika. Pombe's failure was inevitable, the wise saw it coming. Sasa sijui waimba ngonjera wake bado mna pumzi?
 
Umeandika vema. Mara nyingi kwa ushauri tuu, ukiandika makala hizi; ipanue zaidi kwa kudokeza machache ambayo unadhani pengine yanahitaji improvement katika utekelezwaji. Makala itanoga zaidi. Otherwise shukrani sana.
 
Ndio maana Rais anaongea hamtaki kuelewa anacho fanya,,bora aendelee kuwatoa wanao sumbua maana wa bongo tuna akili za mbuzi.Jpm pga kaz sis tunaona tz watu wa lawama
 
Maendeleo hayana vyama tujikite kujenga nchi lkn katiba ifuatwe
Ndio maana Rais anaongea hamtaki kuelewa anacho fanya,,bora aendelee kuwatoa wanao sumbua maana wa bongo tuna akili za mbuzi.Jpm pga kaz sis tunaona tz watu wa lawama
 
Ndio maana Rais anaongea hamtaki kuelewa anacho fanya,,bora aendelee kuwatoa wanao sumbua maana wa bongo tuna akili za mbuzi.Jpm pga kaz sis tunaona tz watu wa lawama
He's already mess it up and screws our economy...KAZI ipi tena apige...akae pembeni Kesha feli completed
 
Hakuna mafanikio makubwa Kama pyschological promo. Amani moyoni ni mafanikio ukiwa unamuamini kiongozi na anakuhakikishia hayo ni mafanikio.
Mh Magu .ajue huko alipo kwamba uaminifu wake ni silaha na amani moyoni mwetu

Na hakuna kitu mbaya Kama psychological trauma
 
Ukitaka kujua nchi imetulia kwa sasa baada ya rais Magufuli kuingia madarakani 2015, tofauti na kikundi cha watu wachache ambao mirija yao imezibwa ,wakitumia kichaka cha kujiteka na kiupakazia serikali.
Hata hivyo drama hii imeshindwa ku-hit kama kigenge hiki kilivyotarajia.

Yafuatayo ni matukio sugu hayapo kwa sasa na ni kiashiria tosha kwamba nchi inaendeshwa kwa ustadi na umakini

1-Hakuna migomo ya wafanyakazi na maandamano ya mara kwa mara ,wafanyakazi wako bize kutoa huduma kwa jamii

2-Hakuna migomo na maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu mara kwa mara kama ilivyokua awali.mikopo inatoka kwa wakati na hakuna upendeleo

3-vurugu za maandamano na uporaji wa vyama vya upinzani ulioshamiri kila uchao ,yamekoma

4-ujambazi rate inmeshuka sana

5-utapeli na udhulumati wa wazi rate imeshuka .

Mengine ongeza na wewe
 
Back
Top Bottom