mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Kwamba yeye hajui mifumo na mifumo haipo! Ukweli ni kwamba mifumo ipo, sheria zipo, nk.Rais anapaswa kuweka misingi au mifumo na siyo kuongoza nchi kwa matamko ya barabarani. Akiondoka madarakani hakika hataacha kitu cha kudumu kwa anaongoza kwa matamko tu. Tunahitaji mifumo ambayo hata aje rais wa namna gani mifumo itamwongoza mfano ni mataifa yaliyoendelea kama USA. Trump hawezi kuiangusha Marekani na ukichaa wake kwani maamuzi ya msingi yanafanywa na wengi na yalishapitishwa na mifumo iliyopo.
Kwa mfano kuna viongozi wa Serikali za Kijiji, Serikali za Mitaa, Madiwani, Wabunge na hatimaye Mawaziri. Na kila kiongozi ana majukumu, madaraka na mamlaka yake.
Kilicho wazi ni viongozi "kula bata" na kulewa madaraka.