akirudi mpe na shule nyingine ataelewa tuNchi nyingi ziliendelea haraka baada ya kupambania mambo makubwa hasa kumi hapa jipime uwezo wako kutizama mambo bila ushabiki mandaz;
1. Nishati kiujumla yaani umeme,mafuta,gesi,makaa ya mawe nk.
*Katika hili anajaribu kwenye 'iyo steglers' tuu na hatujajua itafanikiwa kwa kiasi gani lakini gas haieleweki,mafuta hatuna uhakika,makaa ya mawe hali ni dhaifu. Hakuna jambo la 'miaka kumi hapi'
2. Elimu kiujumla yaani tafiti,ufundi technolojia,walimu bora nk.
*Katika hili amejaribu tuu kuondoa ada lakini wanafunzi bado wanalipia vitu kadhaa,hakuna tafiti zamaana,hakuna Elimu kabambe ya ufundi,walimu ni masikini na wamejawa msongo wa mawazo kwakuwa hawajaliwi. Hayo ya miaka kumi ni yepi?
3. Kilimo kiujumla yaani umwagiliaji,mifugo yakisasa,uvuvi na kilimo biashara.
* Kwahili hakuna cha kumsifu,amezorotesha mazao ya biashara,maafisa kilimo wlhawaeleweki wanafanya mini,umwagiliaji mdogo uliopo upon mashakani na watu wengi wamekata tamaa na kilimo. Nionavyo hajafanya hata ya mwaka mmoja.
4. Uchukuzi na makaazi kiujumla yaani usafiri wa treni,anga,barabara,nyumba za kisasa nk.
*hapa amejaribu barabara japo zinaharibika hovyo,reli na ndege anavivamia bila tafiti za kutosha. Tunaweza tusipate faida kwenye ndege mpaka zitapokufa zote na treni lazima I we kimkakati kama wenzetu Kenya,Ethiopia,Angola nk.
Makaazi ni eneo ambalo bado tumerudi nyuma national housing haieleweki tena wakati eneo hili limefaidisha serikali nyingi kimapato,kupunguza maradhi,kupangilia makazi na kupendezesha miji.
5. Utalii/madini kiujumla.
* tumejaaliwa madini tele na maeneo bora ya utalii hapa hajafanya chochote cha miaka kumi zaidi ya kuzuia wizi kwa kiwango flani tuu kwenye madini. Utalii hatujitangazi hatujulikani duniani na sekta hii haijafanikiwa hata kama enzi ya kikwete.
6. Uwekezaji/viwanda na biashara kiujumla
*Sioni hicho cha miaka kumi hapa biashara zinafungwa,wafanyabiashara wanakimbilia nje yeye mwenyewe amekiri kuyaona mipakani. Viwanda zilikuwa mbwembwe za yule waziri maneno mingi mwenye kiki kama msanii ukweli hatuna mazingira mazuri ya viwanda maana hata nguvu ya kununua watu hawana
Uwekezaji hasa toka nje umepotea,hakuna wanaotamani kuja kuwekeza sehemu watu matajiri wanaburuzwa na kutabiriwa kuishi kama mashetani...
Niendelee nisiendelee...?? Sema suu!!