babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,985
2,000

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...

Pia soma;

https://www.jamiiforums.com/threads...fuli-viva-rais-magufuli-viva-tanzania.970067/
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
14,106
2,000
Wapi tija? Mbona maisha ni magumu?,ajira Hakuna, mmeshindwa ongeza hata mishahara,kulipa wastaafu mafao,acheni propaganda za kuwadanganya futureless people wanyonge maadamu tu mnashiba
Labda kazi ya kuleta umasikini nchini.
Uchumi unavyopanda maisha lazima yawe magumu. Maisha hayawezi kuwa raisi hata siku moja, unaweza kunitajia ni nchi gani ambayo imeendelea na maisha ya raia wake ni rahisi? Nafahamu huwezi kujibu hilo bali utakaa na kulialia tu na kuwewesekaweweseka. Chapa kazi mkuu malipo ni hapa hapa duniani.
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
14,106
2,000
Kama si propaganda Why anawaogopa wapinzani mikutano tu ya ndani ya wanawake anapata homa,why aprint fomu moja tu ya kugombea?
Mkutano upi wa ndani? weka ushahidi? JPM amuogope nani wakati yeye ndiye amiri Jeshi mkuu? Hizo ni ndoto tu, endelea kuota ukiamka utakuta Tanzania iliyopiga maendeleo.
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,382

Achaa mahaba labda we ni kipofu.
Kosa la Zito na Bwege ni lipi?
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,382
2,000
Uchumi unavyopanda maisha lazima yawe magumu. Maisha hayawezi kuwa raisi hata siku moja, unaweza kunitajia ni nchi gani ambayo imeendelea na maisha ya raia wake ni rahisi? Nafahamu huwezi kujibu hilo bali utakaa na kulialia tu na kuwewesekaweweseka. Chapa kazi mkuu malipo ni hapa hapa duniani.
Wenzetu wamewekewa mifumo ya kufanya kazi,ukilima kazi yako sio kutafuta soko Bali soko ndo linakutafuta,mikopo rahisi na wezeshi,Kodi rafiki.Hapa tu Kodi ya kuingiza gari ili uzalishe ni kubwa kuliko hata gharama za kuzalisha gari Hilo kiwandani, mtawala anajisifia kuwasomesha namba watu ili wawe masikini ili aweze kuwatawala then anasema makusanyo yameongezeka.Vikwazo vya kufanikiwa kwa jumla ni vingi.Kama wakoloni wao waliweza boresha maisha ya watu sababu waliotengeneza mifumo mizuri ya kuwafanya watu wafanye kazi.Sera mbovu uzalisha tatizo la ajira ajira.
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,382
2,000
Ambaye amekosa ajira ni wewe peke yako kisa kukesha JF. Ardhi yote tuliyonayo bado unalalamika? Chukua jembe kalime hakuna atakayekusidia kama wewe mwenyewe umeshindwa kujisaidia.
Unadhani kulima ni rahisi Kama kufanya mapenzi.Hilo kundi la machinga na bodaboda sababu ya sera mbovu za ujima lililojaa mjini means hio ardhi hawaioni?
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,382
2,000
Ambaye amekosa ajira ni wewe peke yako kisa kukesha JF. Ardhi yote tuliyonayo bado unalalamika? Chukua jembe kalime hakuna atakayekusidia kama wewe mwenyewe umeshindwa kujisaidia.
Mifumo mibovu ya kuwafanya watu wawe masikini ili uwatawale ili wakuabudu,kwa kuuwa private sector kimakusudi eti ni wapiga dili Sasa sijui wakulima waliozulumiwa hizo dili sijui walizipigia wapi.
Badala ya kuleta maendeleo ya watu Bali vitu ili ukumbukwe kupitia vitu usipokuwepo,inachochea umasikini na ongezeko la machinga na bodaboda ambao si wazalishaji wa kukuza uchumi Bali ni madalali wa viwanda vya china.
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
14,106
2,000
Je imeleta tija kwa wanyonge ( future less people)
Kipofu haambiwi tazama.

Wenzetu wamewekewa mifumo ya kufanya kazi,ukilima kazi yako sio kutafuta soko Bali soko ndo linakutafuta,mikopo rahisi na wezeshi,Kodi rafiki.Hapa tu Kodi ya kuingiza gari ili uzalishe ni kubwa kuliko hata gharama za kuzalisha gari Hilo kiwandani, mtawala anajisifia kuwasomesha namba watu ili wawe masikini ili aweze kuwatawala then anasema makusanyo yameongezeka.Vikwazo vya kufanikiwa kwa jumla ni vingi.Kama wakoloni wao waliweza boresha maisha ya watu sababu waliotengeneza mifumo mizuri ya kuwafanya watu wafanye kazi.Sera mbovu uzalisha tatizo la ajira ajira.
Wamewekewa na nani? Jiulize? Unatakiwa wewe mwenyewe uweke mazingara yatakayokusaidia hapo baadaye kujiwezesha, hatuwezi kuendelea kuwa watumwa wa mtu mweupe. Kama unafikiri kuwasomesha watu sio kuwakomboa kiuchumi kalaga baho!

Mifumo mibovu ya kuwafanya watu wawe masikini ili uwatawale ili wakuabudu,kwa kuuwa private sector kimakusudi eti ni wapiga dili Sasa sijui wakulima waliozulumiwa hizo dili sijui walizipigia wapi.
Badala ya kuleta maendeleo ya watu Bali vitu ili ukumbukwe kupitia vitu usipokuwepo,inachochea umasikini na ongezeko la machinga na bodaboda ambao si wazalishaji wa kukuza uchumi Bali ni madalali wa viwanda vya china.
Kwa hiyo JPM ndio amekufanya wewe uwe masikini? Je, unasemaje kwa wale ambao wamekuwa matajiri katika kipindi hiki cha utawala wake? Matatizo yako binafsi ya kushindwa kwako binafsi sio swala la kitaifa. Umasikini wako na ulofa isiwe nongwa ya kutuchelewesha kwenda kwenye uwezeshaji uliotukuka kwa kila Mtanzania anayejitambua na wajibu wake kwa Taifa.
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,382
2,000
Kipofu haambiwi tazama.Wamewekewa na nani? Jiulize? Unatakiwa wewe mwenyewe uweke mazingara yatakayokusaidia hapo baadaye kujiwezesha, hatuwezi kuendelea kuwa watumwa wa mtu mweupe. Kama unafikiri kuwasomesha watu sio kuwakomboa kiuchumi kalaga baho!Kwa hiyo JPM ndio amekufanya wewe uwe masikini? Je, unasemaje kwa wale ambao wamekuwa matajiri katika kipindi hiki cha utawala wake? Matatizo yako binafsi ya kushindwa kwako binafsi sio swala la kitaifa. Umasikini wako na ulofa isiwe nongwa ya kutuchelewesha kwenda kwenye uwezeshaji uliotukuka kwa kila Mtanzania anayejitambua na wajibu wake kwa Taifa.
Nazungumzia uchumi wa jumla sio wa wapiga dili wa awamu hii.Ungekuwa unajitegemea ungejuwa Hali halisi lkn kwa sababu unaishi kwa shemeji mnufaika na we ni kula kulala ni lzm uwe ni kipofu mnufaika,lakini majority wapo hoi.
Kama unaweka mifumo ya kuwabana watu mfano Kodi komozi,kuuwa sekta binafsi,kupora biashara za watu, Kuzulumu wakulima, Kuzulumu watumishi haki zao, kuwashughulikia matajiri sababu ya chuki,kuuwa diplomasia,nk Hawa majority watakuwa vipi na nafuu ya maisha.Mimi hata sukari iuzwe elf 10 kilo namudu,nauli iwe elf 5 namudu vipi majority?.Si mbinafsi sababu nashiba nisiumie kuona wengi wakifanywa masikini kimakusudi.Ungekuwa umesoma na kuujua uchumi ungeelewa.
Maendeleo sio kondomu Hadi uzame mfukoni,je maendeleo ya vitu yanareflect kubadili maisha ya watu?
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,382
2,000
Kipofu haambiwi tazama.Wamewekewa na nani? Jiulize? Unatakiwa wewe mwenyewe uweke mazingara yatakayokusaidia hapo baadaye kujiwezesha, hatuwezi kuendelea kuwa watumwa wa mtu mweupe. Kama unafikiri kuwasomesha watu sio kuwakomboa kiuchumi kalaga baho!Kwa hiyo JPM ndio amekufanya wewe uwe masikini? Je, unasemaje kwa wale ambao wamekuwa matajiri katika kipindi hiki cha utawala wake? Matatizo yako binafsi ya kushindwa kwako binafsi sio swala la kitaifa. Umasikini wako na ulofa isiwe nongwa ya kutuchelewesha kwenda kwenye uwezeshaji uliotukuka kwa kila Mtanzania anayejitambua na wajibu wake kwa Taifa.
Click to expand...
100% sera mbovu za awamu hii,kutwa kucha kupambana na upinzani badala ya kupambana na umasikini wetu ndio zimeleta umasikini nchini.
Unajua tafsiri au Nia ya kusomesha watu namba, kulimia meno, vyuma kukaza, ungekuwa unajitegemea ungelewa lengo lake ni nn.Nikusaidie ni kitendo cha kufanya watu wawe masikini ili uwatawale.Kumbuka makomunist yote hayana uwezo wa kuongoza intelligent people na watu waliofanikiwa,ili waweze kutawala ni lzm wawashushe watu wawe masikini na kutengeneza hofu na uoga kwa kutumia nguvu na si hoja ya ushawishi kwa sababu hawana brain hio.Thus wenzetu sio kila takataka upewa leseni ya udereva ili usijeangusha gari only bright one na wasio na itikadi za kijamaa na kikomunisti ndani mwao ili wasiletee watu umasikini.
Tangu awamu ya kusomesha watu namba iingie jumla ya watu milioni 4 wamepoteza ajira zao rasmi.Achilia propaganda za ajira milioni 6 labda za machinga na bodaboda ambazo hazichochei ukuaji wa uchumi.
Hakuna makomunist yeyeto yanayoshughulika na maendeleo ya watu Bali vitu lengo ni kutafuta sifa na kuja kukumbukwa.
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,382
2,000

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...

Pia soma;

https://www.jamiiforums.com/threads...fuli-viva-rais-magufuli-viva-tanzania.970067/
Maendeleo ya vitu sio maendeleo ya watu Kama hayareflect tija maendeleo ya watu ni bure.
 
Drat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
528
1,000
Maendeleo ya vitu hata jakaya ameyafanya Magufuli cha maana alichofanya ni kukomesha Rushwa na kuleta nidhamu
Kipindi cha kikwete ulikuwa unajua habari za rushwa kubwa kwa sababu aliruhusu Transparency.
Ni watu ambao mnaendeshwa na mapenzi ya vyama hamtaki kufumbua macho, sisemi kama hajakomesha, lakini ni vyema angeruhusu masuala kama ya ununuzi wa ndege,ripoti ya former CAG kujadiliwa, suala kama la Kangi kujadiliwa ili lijulikane kiundani,kivuko alichokikabidhi jeshi kijadiliwe manunuzi yake(sababu ilitia shaka).
Kwa watu wa chini mtu anaesema siku hizi hakuna rushwa sababu hajasikia Dowans n.k muulize kama ana gari Traffic wanafanyaje?Kama ni malaya muulize zile bar wanakojiuza mwenye bar anatumia ujanja gani, kama ni dereva wa basi muulize katika mizani siku hizi vipi?
Hint, siku hizi watu wanachukua cash tena kwa dollar sometimes wanakaa nazo home ili wasiwe traced kirahisi
 
Sasa transparency ya JMK aliwezesha miradi ipi ambayo leo hii tungekuwa tunamsifia? Kwa haraka tu nakumbuka vigenerator kila kona ya maduka Dar Es Salaam vile vile haikuwa rahisi kupanda ndege za kwetu wenyewe Watanzania. Barabara mbovu pamoja na mwelekeo wa watoto wa JMK nao kuwa marais huko mitaani. Rushwa ilitamalaki madini waliokuwa wanafaidi ni makampuni kutoka nje nk. Husda ni kitu kibaya kwa afya yako.
 
😃😃😃 Husda inatoka wapi?Au uko "programmed" kutaja maneno kama hayo mtu wa "pwani"?
Ili upimwe katika issues kama hizo lazima tu observe good governance ambayo hiyo Transparency iko ndani yake...
Halafu kuhusu miradi hata JK wenu,nasisitiza wenu "kijani" nae ana miradi yake aliyomalizia na kuanzisha; mwendokasi, udom,kilometa kibao kadhaa za lami JPM akiwa Waziri,kutanua wigo wa udahili elimu ya juu n.k.,kuleta Foreign Direct Investment kubwa "Dangote"...ambayo ni ya thamani ya almost 1.38 T kwa rate ya 2300/-.....
Kwa hiyo wewe kama mwana CCM haustahili kuniambia nchi ilikuwa inaliwa huyu sasa anatukomboa,wakati ni "ile ile" ila kwa sasa watu na bunge limevaa barakoa...
Tungeshakuwa mbali sana, lakini hatujafika, and we are not ready to take another risk ati akae mpaka achoke, nchi sio ya kifalme hii tufuate katiba na taratibu za sheria.
"Umaamuma ni hatari kwa uhai wako"
 
1593451051569.png

Wapi nimesema asifuate katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Wacha kukariri twende na facts sio mihemuko ya kukariri. Come on with those facts then we can discuss.
 
Drat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
528
1,000
Sasa transparency ya JMK aliwezesha miradi ipi ambayo leo hii tungekuwa tunamsifia? Kwa haraka tu nakumbuka vigenerator kila kona ya maduka Dar Es Salaam vile vile haikuwa rahisi kupanda ndege za kwetu wenyewe Watanzania. Barabara mbovu pamoja na mwelekeo wa watoto wa JMK nao kuwa marais huko mitaani. Rushwa ilitamalaki madini waliokuwa wanafaidi ni makampuni kutoka nje nk. Husda ni kitu kibaya kwa afya yako.
We jamaa ni "kajinga"😃 una akili za kibaamedi, niamini. Nilikuwa najibu kuhusu "kukomesha rushwa" ukaja kuhusu miradi, nikakuonyesha hata yule wenu mwingine kuna miradi alifanya, umehamia katika suala jingine.
"We baamedi,tunaongelea pombe kali, wewe unaleta beer"😃.Pleaase pleaase abide by your id "wacha moja".
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom