babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,964
2,000

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...

Pia soma;

https://www.jamiiforums.com/threads...fuli-viva-rais-magufuli-viva-tanzania.970067/
 
chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,332
2,000
Hakuna hata mmoja ambae alipewa hongo. Wamekiri kuwa JPM anafanya kazi.Miradi mikubwa ndani ya miaka minne, Sgr, JNHHP daraja la wami,busisi n.k
Huko wanako toka pamejaa utapeli na umimi na si wapinzani bali ni wapingaji. Kisingizio cha uongo ni kununuliwa.
Wananchi wameshachoka utapeli na wanaona kwa macho nini JPM anafanya..
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
71,760

Ulimola ? habari za Geita mkuu
 
MAPITO Mwanza

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
1,280
2,000
Hakuna hata mmoja ambae alipewa hongo. Wamekiri kuwa JPM anafanya kazi.Miradi mikubwa ndani ya miaka minne, Sgr, JNHHP daraja la wami,busisi n.k
Huko wanako toka pamejaa utapeli na umimi na si wapinzani bali ni wapingaji. Kisingizio cha uongo ni kununuliwa.
Wananchi wameshachoka utapeli na wanaona kwa macho nini JPM anafanya..
chizi karogwa tena
 
Deghe Mangae

Member
Mar 3, 2020
39
95
Kila Chenye mwanzo kamwe hakikosi mwisho wacha tuumie kwanza time will tell, yuko wapi Mabutu seseseko kuku wazabanga alifanya vitu vya ajabu sana
Pamoja na kuboresha mazingira ya kijijini kwao, Relax Negativity and positivity kwetu ni FULSA Lazima tucheze nazo
Msaliti wa nchi lazima auawe. There is no excuse! Na atakuwa kweli sio masihara.

Kama wasipo uawa wao ina maana sisi ndiyo tufe kwa ajili ya tamaa zao za madaraka?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
429
500
1584084036141.png
1584084079036.png

MAFANIKIO ya kishindo, kujivunia na ya kihistoria yanayojumuisha maeneo 23 yamepatikana katika Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi kifupi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango (pichani) alielezea mafanikio hayo juzi wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21. “Mafanikio haya makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuanzia mwaka 2016/17 hadi Januari 2020 chini ya utawala wa Rais Magufuli na Serikali yake ya CCM,” alisema Dk Mpango.

Dk Mpango alisema katika bajeti ya mwaka 2019/20, Sh trilioni 12.25 zilitengwa kugharamia miradi ya maendeleo, ambapo kati ya hizo Sh trilioni 9.74 zilikuwa fedha za ndani na Sh trilioni 2.51 fedha za nje.

Miongoni mwa mafanikio makubwa ni Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Standard Gauge (SGR) ambao kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (kilometa 300) umefikia asilimia 75 na Morogoro – Makutupora (kilometa 422) asilimia 25.

Hadi Septemba 2019 mradi huu umezalisha ajira 13,117. Aidha, zabuni zenye thamani ya Sh bilioni 664.7 zimetolewa kwa wazabuni na makandarasi wa ndani 640. Sh trilioni 2.96 zimetumika kugharamia mradi huu, zikijumuisha Sh bilioni 237.5 zilizotolewa katika kipindi cha Julai 2019 hadi Januari 2020.

Pia ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere wa megawati 2,115, ambao kazi zilizokamilika ni ujenzi wa miundombinu wezeshi ya mradi kama njia ya kusafirisha umeme, barabara kwa kiwango cha changarawe, mfumo wa maji, mawasiliano ya simu na nyumba za makandarasi na ujenzi wa daraja la muda namba 2.

Pia utafiti wa miamba na udongo na uchimbaji wa mtaro wa chini kwa chini wenye urefu wa mita 147.6, kuelekea kwenye mtaro wa chini kwa chini wa kuchepua maji na mtambo wa kuchakata kokoto namba moja, ambapo utekelezaji wa mradi wote umefikia asilimia 10.74.

Dk Mpango alisema Sh trilioni 1.28 zimetumika kugharamia mradi huu, ikijumuisha Sh bilioni 200.7 ambazo zimetolewa katika kipindi cha Julai 2019 hadi Januari 2020. Mradi huu umezalisha ajira zipatazo 3,074 na makandarasi wa kampuni 10 za Tanzania wamepata fursa.

“Serikali imeendelea kuboresha Shirika la Ndege Tanzania kwa kununua ndege mpya 11, kati yake ndege nane (8) mpya zenye thamani ya shilingi trilioni 1.27 zimepokelewa na malipo ya awali ya shilingi bilioni 85.7 kwa ajili ya ununuzi wa ndege nyingine mpya tatu (3) yamefanyika ambapo ndege mbili (2) ni aina ya Airbus A220-300 na moja (1) ni aina ya De Havilland Dash 8-400,” alisema Dk Mpango.

Miradi kadhaa ya umeme imekamilika, ukiwemo wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Makambako – Songea ambao Sh bilioni 160.1 zimetumika. Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400 kutoka Singida – Arusha – Namanga unaendelea, ambapo utekelezaji umefikia asilimia 63 na Sh bilioni 219.4 zimetumika katika kipindi cha Julai 2016 hadi Januari 2020.

Pia inaendelea na utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini kupitia REA, ambapo vijiji 8,641 kati ya vijiji 12,268 vya Tanzania Bara vimeunganishwa umeme sawa na asilimia 70.4.

Alisema katika kipindi cha Julai 2015 hadi Januari 2020, Sh trilioni 1.53 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huu, ikijumuisha Sh bilioni 207.2 zilizotolewa katika kipindi cha Julai 2019 hadi Januari 2020.

Alisema serikali inaendelea kuboresha huduma ya majisafi na salama vijijini na mijini, ambayo utekelezaji wa miradi 875 unaendelea ikijumuisha miradi 802 ya maji vijijini na miradi 73 ya maji mijini na 75 ya maji vijijini imekamilika.

Serikali imeendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kugharamia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya vituo 540 vya kutolea huduma za afya, ikijumuisha vituo vya afya 361, hospitali za halmashauri za wilaya 71, hospitali za zamani tisa na zahanati 99. Watumishi 477 wameajiriwa na kupangiwa vituo.

Aibainisha kuwa serikali inaendelea na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III), ambao kaya 1,067,041 zenye wanakaya 5,130,001 zimetambuliwa na kuandikishwa katika vijiji na mitaa 9,627 kwenye halmashauri 159 Tanzania Bara na kaya 32,248 zenye wanakaya 169,999 katika Shehia 204 za Zanzibar na ruzuku ya fedha Sh bilioni 968.73 imehawilishwa katika kaya hizo. Kati ya hizo, Sh bilioni 935.94 ni kwa Tanzania Bara na Sh bilioni 32.79 ni kwa Zanzibar.

Katika sekta ya madini, serikali imepitia na kurekebisha sera, sheria na mikataba ya uwekezaji katika sekta ya madini, ambapo marekebisho hayo yamewezesha kuanzishwa kwa Kampuni mpya ya Twiga Minerals Corporation inayomilikiwa kwa ubia kati ya serikali (hisa asilimia 16) na Kampuni ya Barrick (hisa asilimia 84), kuanzishwa kwa masoko 28 na vituo 25 vya ununuzi wa madini, na kukamilika kwa ujenzi wa vituo vinne vya umahiri katika maeneo ya Bariadi, Musoma, Bukoba na Handeni na kuendelea na ujenzi wa vituo vya Songea, Mpanda na Chunya. Serikali imepata mafanikio mengi katika maeneo mengine yakiwemo ya viwanda, kilimo, uvuvi, ufugaji, ujenzi wa barabara na madaraja na usajili wa wajasiriamali na utoaji haki mahakamani.
 
The coolest jw

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
502
1,000
Alichoongeza ni kuwanyima wafanyakazi annual increment na kupandisha madaraja kwa wakati na pia kuwauwa wapinzani wake kwa kuwatuma watu wasiojulikana na kumshambuli kama TL
 
KIBESENI

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
328
500
Huwa siamini tuhuma nyingine juu ya huyu rais kipenzi chao waliomchagua. Imekuwa kawaida sana siku hizi watu wengi hapa tz yetu kudai magu kaleta hali ngumu kimaisha. Siku hizi, mimi nashindwa kuelewa kabisa, hii hali kuwa ngumu magu kaletaje.

Maana lidhiki ya mtu unayo wewe mwwnyewe. Kwa kufanya kazo kwa bidii. Yako mengi na mimi yanayonifanya nisimuunge mkono sana. Lakini mengine Watanzania mnamsingizia raisi wenu, hajasababisha wala kufanya hari ya maisha kuw ngumu, FANYA KAZI BILA KUCHAGUA UONE KAMA HALI ITAKUWA NGUMU.

Voice from village, samahani mwandiko lakini.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
3,318
2,000

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...

Pia soma;

https://www.jamiiforums.com/threads...fuli-viva-rais-magufuli-viva-tanzania.970067/
Hata nchi ikikaimiwa na makamu wa rais hayo yote yangetokea na zaidi.
 
Top Bottom