Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2020

babalao 2

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
4,754
Points
2,000
babalao 2

babalao 2

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
4,754 2,000

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...
 
omtiti

omtiti

Senior Member
Joined
Jun 19, 2019
Messages
153
Points
250
omtiti

omtiti

Senior Member
Joined Jun 19, 2019
153 250
Ukitaka kujua nchi imetulia kwa sasa baada ya rais Magufuli kuingia madarakani 2015, tofauti na kikundi cha watu wachache ambao mirija yao imezibwa ,wakitumia kichaka cha kujiteka na kiupakazia serikali.
Hata hivyo drama hii imeshindwa ku-hit kama kigenge hiki kilivyotarajia.

Yafuatayo ni matukio sugu hayapo kwa sasa na ni kiashiria tosha kwamba nchi inaendeshwa kwa ustadi na umakini

1-Hakuna migomo ya wafanyakazi na maandamano ya mara kwa mara ,wafanyakazi wako bize kutoa huduma kwa jamii

2-Hakuna migomo na maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu mara kwa mara kama ilivyokua awali.mikopo inatoka kwa wakati na hakuna upendeleo

3-vurugu za maandamano na uporaji wa vyama vya upinzani ulioshamiri kila uchao ,yamekoma

4-ujambazi rate inmeshuka sana

5-utapeli na udhulumati wa wazi rate imeshuka .

Mengine ongeza na wewe
 
Perfectz

Perfectz

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2017
Messages
5,439
Points
2,000
Perfectz

Perfectz

JF-Expert Member
Joined May 17, 2017
5,439 2,000
SASA HIVI KILA MTU ANA ANGALIA MAISHA YAKE MKATE TU WA SIKU SHIDA.
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
26,315
Points
2,000
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
26,315 2,000
Tumeruhusiwa kufyatua watoto wengi ili tukuze uchumi wa nchi yetu
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
2,664
Points
2,000
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
2,664 2,000
Haya usha-post, mrudishie shemeji yako smartphone yake manake watu aina yako hamkawagi kuanza kusoma na messages zake za whatsapp.
 
BOB OS

BOB OS

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Messages
2,432
Points
2,000
BOB OS

BOB OS

JF-Expert Member
Joined Dec 11, 2011
2,432 2,000
dah hawa ndio uvccm,,,,,
kama nchi kuna shida mahali,,haya kachukue buku7 yako fasta
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
2,664
Points
2,000
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
2,664 2,000
Jpm kiboko sana huyu jamaa watu kimya
Lazima watu wawe kimya hasa baada ya waziriu wake kutamka hadharani kwamba Azory Gwanda amekufa (soma: ameuawa)! Watu lazima wawe kimya kwa sababu wanaogopa kuuawa kama alivyouawa Azory Gwanda! Watu lazima wawe kimya kwa sababu wanaogopa kumiminiwa mvua ya risasi kama alivyomiminiwa Tundu Lissu! Lazima watu wawe kimya kwa sababu wanaogopa kupotezwa kama alivyopotezwa Ben Saanane! Watu lazima wawe kimya kwa sababu wanaogopa kutekwa na kuachiwa baada ya kutoa pesa mingi kama ilivyokuwa kwa Mo Dewji!

In short, lazima watu wawe kimya kwa sababu wanajua the devil family is running the country! The devil family that loves blood over water!
 
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,621
Points
2,000
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,621 2,000

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...

Uwanja wa ndege upanuzi umeanza siku nyingi ni ufunguzi tu, fly over zimejengwa wakati wa Kikwete ni umaliziaji na pesa za world bank, daraja la salenda linajengwa kwa msaada wa korea walisema haya kuanzia wakati wa kikwete. Ndege ndiye kanunua yeye barabara ya Dar Moro ilianza zamani lakini wamesimamisha. Treni ilianza zamani wakaiharakisha lakini mradi ulikiwepo. Mradi wa umeme umeanza lakini ndiyo umeanza tu...... naona mna kuza mambo kuliko yalivyo hiyo miradi haijakamilika na mingi sio yake. Shule bure ndiyo mradi wake pekee na mabweni 😂 yaani raisi kujenga mabweni yawe agenda wakati wenzake waligenga chuo cha Dodoma kizima na plan zote wanafunzi 40,000 wenzake waliweka pipeline ya gas, 😂
 
G

gunga yenna

Member
Joined
Apr 11, 2019
Messages
89
Points
95
G

gunga yenna

Member
Joined Apr 11, 2019
89 95
He's already mess it up and screws our economy...KAZI ipi tena apige...akae pembeni Kesha feli completed
Man our treasurery is full of cash come sun come rain, the money you used to swindle is no more, all swindlers have same talk because they have nothing to swindle before being swindled.
 
joshydama

joshydama

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Messages
3,360
Points
2,000
joshydama

joshydama

JF-Expert Member
Joined May 10, 2016
3,360 2,000
Habari wanabodi,

Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wote wanabodi.

Ni kwamba kumekuwa na tuhuma nyingi sana za ajabu na kijinga ambazo hazina hata miguu ya kusimamia kwamba Mr. President ameshindwa kuiongoza nchi na kusababisha mpasuko katika chama cha CCM.

Hakika uamini usiamini hizo tuhuma zimekuwa zikitolewa na wanachama ambao ni wapigaji ambao ile mizizi yao ya upigaji imekatwakatwa na kutupwa baharini. Hivyo basi, kwa sababu ya kuzibwa ile mianya ambayo waliitumia kuwaibia wananchi wake leo hii wameamua kuja na tuhuma ambazo hazina mashikohata kidoo ili waonekane wao ni bora sana kuliko Mr. President.

Mr. President ukimuondoa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere hakuna Rais mwingine aliyeweza kutokea mwenye uwezo mkubwa na akili kubwa kama wewe. Mbali na uwezo wako mkubwa, wewe ni Rais mbunifu sana tumeshuhudia ubunifu wa hapa na pale mfano ni pale ambapo ulipoanzisha akaunti ya pamoja y kukusanya mapato ya taifa. Huu ubunifu umeweza kuzuia upigaji wa fedha za umma kwa asilimia 85/%.

Kadhalika, Mr. President, wewe ni mfano mkubwa wa kuigwa ulipoanzisha mapambano dhidi ya wahujumu uchumi wala rushwa kitu ambacho hakuna Rais yoyote aliwahi kufanya hiki kitu bali kuna ambao walibariki hayo mambo kama yalivyotajwa hapo juu.

Pia, tumeshuhudia miradi mikubwa sana kujengwa katika taifa letu kwa muda mchache sana tena kwa fedha za watanzania ambazo zinatokana ukusanyaji wa kodi. kiukweli hili jambo linathibitisha uwezo wako mkubwa katika utawala. Tangu nchi hii ipate uhuru hapjawahi kutokea miradi mikubwa ya namna hii.

Aidha, kwa muda mchache uliweza kununua ndege kitu ambacho pia kimesababisha uonekane shujaa katika taifa na kimataifa kwa ujumla.

Mr. President umeweza kuondoa akili mgando kwa baadhi ya watanzania kwamba Maisha mazuri ni lazima upate ajira. Umeweza kuwaonesha kwamba Maisha siyo kuajiriwa serikalini tu bali hata kujiajiri ni jambo la msingi sana.Hii ni jambo la kishujaa sana kwani leo hii vijana wako wanapambana sana na kufanya kazi kwa bidi ili waweze kujiajiri wenyewe. Indeed, unastahili pongezi sana.

Mr.president huwa unaenda mbali sana kwa kuwaadhibu viongozi wazembe na wasiojitambua na ambao wanashindwa kwendana na falsa yako ya Hapa kazi. kwa hili hakuna pingamizi kwani watanzania tumeshuhudia ukiwaadhibu hao viongozi kwa sababu ya uzembe wao na kukosa uzalendo kwa taifa. Mr. President hongera sana kwa kunapenda sana viongozi wanaojibika wenye kujituma na wabunifu.

Mr. President unastahili pongezi kwa kuhakikisha watoto wa watanzania wanapata elimu bure.Ingawa kuna changamoto yingi sana katika hili jambo, umejitahidi sana kwa hili na hizi changamoto zitaisha tu kwani hakuna changamoto ambayo inaweza kuwa ya milele bali changamoto hutokea tu kwa kipindi kifupi. Pia kumbuka hakuna jambo lisilokuwa na changamoto.

Mr. President ninakuomba ukiwa kama baba wa cha cha CCM hakikisha wanachama wenye nia mbaya na chama chako na kwa taifa kwa ujumla. Wanachama wako wengi wao walizoea vya kunyongwa leo hii wanapata shida sana kula vilivyochinjwa. Walipenda sana mtelezo bila kufanya kazi. Leo hii wanataka kutuaminisha kwaamba wao ni wasafi kuliko wewe. Kitu ambacho ni uongo mtupu.

Tumekuwa tukiwashuhudia wakifanya madudu mengi sana na kupelekea wananchi wao kuteseka, watu ambao walikosa huruma na uzalendo kwa wananchi na kwa Taifa leo hii wanataka kutuaminisha kuwa wao ni wasafi. Usafi huo wameutoa wapi? wanachuki binafsi
dhidi ya utendaji kazi wako uliojaa weledi na ubunifu mkubwa sana. Walishindwa nini tangu zamani kuwa wazalendo ila wanataka kutuaminishia leo hii kuwa wanapenda nchi hii?

Mr. President, wewe nimti wa matunda, kumbuka ule usemi kwamba mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe. Huwezi kuona mti ambao hauna matunda ukirushiwa mawe hata siku moja. Mbali na hili, chuki zao binafsi na lawama zao ambazo hazina miguu wala kichwa usikubali vikuyumbishe.

NB. Kila mtu ana mapangufu yake ingawa mazuri aliyoyafanya Mr. President yanafunika/yamefunika mapungufu yake yote katika utendaji kazi wake.

Mr. president hii ni Summary ya mambo makubwa uliyofanya kwa taifa letu.

1. Kujenga miradi mikubwa mfano Stigler's Gorge project, Ujenzi wa barabara ya Agakhan to Masaki, Flyover, Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni.

2. Kuanzisha mahakama maalum za kushughulikia ufisadi na kuwafunga wahujumu uchumi.

3. Kuanzisha akaunti ya taifa ya pamoja kwa ajili yakutunza mapato.

4. Elimu bure kwa Watanzania.

5. Kuhimiza suala la uzalendo nchini.

6. Ununuzi wa Ndege.

7. Kuondoa safari za nje ya nchi ili kupunguza matumizi mabaya ya kodi za wananchi.

8. Ujenzi mkubwa wa uwanja wa ndege.

9. Serikali kuhamia mkoani Dodoma.

10. Dhana ya kujiamini na kuthamini vya kwetu na siyo vya wazungu.

11. Kuhamasisha watanzania kufanya kazi na waache maisha ya uvivu, uzembe na kupenda mtelezo(Falsafa ya hapa kazi tu)

Karibuni Tumpongeze Mr. President kwa mapinduzi na mafanikio makubwa nchini. Ingawa kuna watu wenye chuki zao binafsi watapinga hili suala kwa hoja nyepesi na ambazo hazina kichwa wala miguu.
 
Forum statistics

Threads 1,316,458
Members 505,652
Posts 31,891,081
Top