Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2020

babalao 2

babalao 2

JF-Expert Member
4,959
2,000


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...

Pia soma;


https://www.jamiiforums.com/threads...fuli-viva-rais-magufuli-viva-tanzania.970067/
 
N

nkese

JF-Expert Member
2,394
2,000


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
Kuna LA maana kweli,sioni!!!!!!'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N

Nanye Go

JF-Expert Member
5,669
2,000
Hahaha kwenye mafanikio mmesahau yeye ni mgunduzi wa matumizi ya maganda ya korosho, kutengeneza potash eti row producukit ya potassium alisema.
 
mosestz

mosestz

Member
10
45
Mh rais ahsante,Ila
Ila tunaomba upande wa pinzani
Awaache wapumue kidogo,
Maana kuna wabunge tayari
Wamezoe mahakama kaa vile
Nyumbani kwao tu! Mh ipe demokrasi nafasi yake! Wakivunja sheria kwa mujibu wakatiba sawa! Sheria ichukue mkondo wake! Japo mh hata hyo katiba ibadilishwe! Tumeichoka,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iceberg9

Iceberg9

JF-Expert Member
12,723
2,000
Mazuri yanaonekana ila aongeze ajira, taifa lisilo hajiri nguvu kazi, mawazo mapya hao wazee punguza wabaki wachache watakao toa seminar kwa freshers young graduates kuleta morali na ufanisi katika kazi ili kuinua uchumi kitaifa

Happiness is a lifestyle
 
Iceberg9

Iceberg9

JF-Expert Member
12,723
2,000
Pia kuweka vipaumbele ni muhimu sana, hakika kila mradi na mikakati ni muhimu ila kuwe na vipaumbele, vile viliowekewa kipaumbele pambana navyo mheshimiwa rais, chagua sekta yenye changamoto ziadi mfano sekta zenye changamoto ni Madini & Nishati, Afya, Elimu, Kilimo, Uchukuzi, Kazi hizi ni baadhi ya sekta zenye changamoto nyingi ukichagua kwa kuweka kipaumbele mheshimiwa rais tutafikia kule kwenye malengo ya taifa

Happiness is a lifestyle
 
Maneno Meier

Maneno Meier

JF-Expert Member
1,718
2,000
Leo niliwaza miradi hii mipya mikubwa ya maendeleo kama Airbus , Stieglers na SGR ni miujiza ya karne ya Mh Rais, niliwaza ili bongo tuendelee kwa kasi tunahitaji Rais wetu awe na taaluma ya ualimu (discipline mbele "we mhuni kuja hapa, kwanini hujachomekea shati unatuletea bangi hapa si mahali pake kima we, shika chini , pa pa pa! , kimbia mjinga wewe, mara! "sijaona kijana mjinga na legelege kama wewe baba yako si ni professa wewe , mbona we unafeli hivi , kazi kudai pocket money tu na kukazania Instagram na videmu mjinga mkubwa wewe baba yako ni rafiki yangu nitamtafuta nimwambie ujinga wako huku shuleni", mara "we msichana tembea kwa ukakamavu huoni uko smart area , kuja hapa haraka kazi kufuga makucha tu kama shetani ndo mwanzo wa uhuni huu na kutoa mimba za utotoni mjinga kabisa wewe! piga magoti ita jua!!) hizi tabia za walimu kuhakikisha usafi na discipline mashuleni sasa tunashuhudia ndo kiboko ya majizi na mazembe yaliyoko serikalini manake Bwana Mkubwa hakwepeshi anawatumbua tu na huu ni utamaduni mpya uliotukuka , unaohitajika na uliokosekana na unaopaswa kusifiwa na kuenziwa daima milele, nawasihi viongozi wangu waandae hidden policy ya chama chetu Rais lazima awe mwalimu kitaaluma na asitokane na zile koo za mafisadi na zile koo zenye majina ambazo mtu mzito tu akitekwa ndo wako mbele mbele na kiherehere na pia Rais asitokane na zile koo za wale wazee waliochanga pesa mwana TANU namba moja akaenda kuhutubia UN! Wenye akili watanisoma!
Asante mkuu umenikumbusha mbali sana. Rais wa Tanzania ni sawa kama ulivyosema, asiwe mwlimu wala mwana sheria na mtu ambaye amesomea kitu chochote kile chenye neno "management" mwishoni. Kundi hili la wasomi ni destructive sana katika maisha ya binadam ulimwenguni, kwani hawako pragmatic.

Tanzania tuna hitaji Rais kama Magufuli mwenye utaalam wa kisayansi. Mbali na hayo awe na Vision na ujasiri wa kutekeleza malengo yake kama Magufuli alivyo. Asiwe mtu wa kutinga tinga tu nje na kupose na watu kama akina Teresa May na Trump au Macron na Angela Merkel au Putin, awe mzalendo na mpenda watu kama Magufuli na mkweli. Asiwe kama hawa watu, hawa ni mapuppet tu wa wazungu. Hawana lolote.
Tsikeli kabla ya kukutana na Emmanuel Macron alitakiwa kwanza akutane na viongozi wa OAU na SADC
Southern African Development Community :: Member States
badala yake ana kutana na Kibaraka mwenzake Kenyatta na Emmanuel Macron Rais wa Ufaransa, kwa sababu hao ndiyo walio msaidia kuwa madarakani.

Jamaa namwona yuko yuko tu hata Vision hana ya maendeleo ya nchi yake. Yeye badala ya kukaa na wananchi wake kwanza na kuwashukuru kwa kazi waliyo ifanya na kusikiliza shida zao ili ajui wapi kuna Tatizo na alitatue vipi? Yeye ndiyo kwanza anaona umuhimu kukutana na watu wakubwa wakubwa wenzake. Amesha shindwa huyo na hana affinity au afiliation na watu wake. Anawatumikia tu mabosi wake.

Angetoa hotuba kubwa kwa wananchi wake na kuwaeleza malengo ambayo anakusudia kuyafanya ili kuendeleza uchumi na maisha ya wananchi wake, hakuna anacho kufanya ni kutinga tinga na kupose na watu kama hao nililo wataja. Sidhani kama kuna mtu anajua political Agenda yake.

Huo ndiyo ufahari wa Afrika. Nawasikitikia wakongo!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BUMIJA

BUMIJA

JF-Expert Member
3,379
2,000
Sa ingine najiuliza ile kauli mbiu ya viongozi kua VIJANA WAJIAJIRI Ali hali wao wana ajira.Basi wafundishwe ujasiriamali huko mashuleni na vyuoni(Education For Self Reliance)
Mzee kajitahidi lakini vijana wanateseka bila ajira. Vijana kutoka mwaka 2015 mpaka Leo hawana vision wala matumaini juu ya maisha yao. Nadhani kuna kizazi kinakwenda kupotezwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics


Threads
1,424,986

Messages
35,078,036

Members
538,184
Top Bottom