Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2020


babalao 2

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
4,698
Points
2,000
babalao 2

babalao 2

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
4,698 2,000


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...
 
Lord eyes

Lord eyes

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2018
Messages
3,862
Points
1,995
Lord eyes

Lord eyes

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2018
3,862 1,995
Hivi uchumi wa wananchi upo vile kwa serikali ya uchumi wa kati maana ndio tunaelekea sasa 2020 kuwa geniva ya afrika aka donor country!!!!!?
 
K

kingunebe

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Messages
211
Points
250
K

kingunebe

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2019
211 250
Amejitahd kuongeza kujudi kwenye makusanyo ya kodi ikiwa n pamoja na kuwaza namna ya kupata hela kiurahis kutoka kwa wajasiliamali wadogowadogo
Amefanikiwa kuongeza deni la taifa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
N

nkese

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2017
Messages
1,561
Points
2,000
Age
57
N

nkese

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2017
1,561 2,000


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
Kuna LA maana kweli,sioni!!!!!!'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N

Nanye Go

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Messages
2,418
Points
2,000
N

Nanye Go

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2018
2,418 2,000
Hahaha kwenye mafanikio mmesahau yeye ni mgunduzi wa matumizi ya maganda ya korosho, kutengeneza potash eti row producukit ya potassium alisema.
 
mosestz

mosestz

Member
Joined
Mar 1, 2019
Messages
10
Points
45
mosestz

mosestz

Member
Joined Mar 1, 2019
10 45
Mh rais ahsante,Ila
Ila tunaomba upande wa pinzani
Awaache wapumue kidogo,
Maana kuna wabunge tayari
Wamezoe mahakama kaa vile
Nyumbani kwao tu! Mh ipe demokrasi nafasi yake! Wakivunja sheria kwa mujibu wakatiba sawa! Sheria ichukue mkondo wake! Japo mh hata hyo katiba ibadilishwe! Tumeichoka,
16387374_1914118995535479_1162443184086066304_n-jpeg.1045418


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akasankara

Akasankara

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2015
Messages
2,093
Points
2,000
Akasankara

Akasankara

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2015
2,093 2,000
"Katika uhalifu huwa hakuna umoja mkitikiswa kidogo tu umoja wenu unasambaratika,huwa ni unafiki tu siyo umoja harisi ,Mara nyingi umoja harisi hudumu na utokana na haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Rudi darasani kisha rejelea historia nzima ya watu waliosambaratishwa pamoja na kuwa na umoja wao halisi. Mfao kawasome mandika people
 
Marry Ngowi

Marry Ngowi

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Messages
851
Points
1,000
Marry Ngowi

Marry Ngowi

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2013
851 1,000
Leo niliwaza miradi hii mipya mikubwa ya maendeleo kama Airbus , Stieglers na SGR ni miujiza ya karne ya Mh Rais, niliwaza ili bongo tuendelee kwa kasi tunahitaji Rais wetu awe na taaluma ya ualimu (discipline mbele "we mhuni kuja hapa, kwanini hujachomekea shati unatuletea bangi hapa si mahali pake kima we, shika chini , pa pa pa! , kimbia mjinga wewe, mara! "sijaona kijana mjinga na legelege kama wewe baba yako si ni professa wewe , mbona we unafeli hivi , kazi kudai pocket money tu na kukazania Instagram na videmu mjinga mkubwa wewe baba yako ni rafiki yangu nitamtafuta nimwambie ujinga wako huku shuleni", mara "we msichana tembea kwa ukakamavu huoni uko smart area , kuja hapa haraka kazi kufuga makucha tu kama shetani ndo mwanzo wa uhuni huu na kutoa mimba za utotoni mjinga kabisa wewe! piga magoti ita jua!!) hizi tabia za walimu kuhakikisha usafi na discipline mashuleni sasa tunashuhudia ndo kiboko ya majizi na mazembe yaliyoko serikalini manake Bwana Mkubwa hakwepeshi anawatumbua tu na huu ni utamaduni mpya uliotukuka , unaohitajika na uliokosekana na unaopaswa kusifiwa na kuenziwa daima milele, nawasihi viongozi wangu waandae hidden policy ya chama chetu Rais lazima awe mwalimu kitaaluma na asitokane na zile koo za mafisadi na zile koo zenye majina ambazo mtu mzito tu akitekwa ndo wako mbele mbele na kiherehere na pia Rais asitokane na zile koo za wale wazee waliochanga pesa mwana TANU namba moja akaenda kuhutubia UN! Wenye akili watanisoma!
 
toxic9

toxic9

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
10,317
Points
2,000
toxic9

toxic9

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
10,317 2,000
Mazuri yanaonekana ila aongeze ajira, taifa lisilo hajiri nguvu kazi, mawazo mapya hao wazee punguza wabaki wachache watakao toa seminar kwa freshers young graduates kuleta morali na ufanisi katika kazi ili kuinua uchumi kitaifa

Happiness is a lifestyle
 
toxic9

toxic9

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
10,317
Points
2,000
toxic9

toxic9

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
10,317 2,000
Pia kuweka vipaumbele ni muhimu sana, hakika kila mradi na mikakati ni muhimu ila kuwe na vipaumbele, vile viliowekewa kipaumbele pambana navyo mheshimiwa rais, chagua sekta yenye changamoto ziadi mfano sekta zenye changamoto ni Madini & Nishati, Afya, Elimu, Kilimo, Uchukuzi, Kazi hizi ni baadhi ya sekta zenye changamoto nyingi ukichagua kwa kuweka kipaumbele mheshimiwa rais tutafikia kule kwenye malengo ya taifa

Happiness is a lifestyle
 

Forum statistics

Threads 1,285,033
Members 494,367
Posts 30,847,817
Top