Watu wana sema kaleta nidhamu.nidhamu hailetwi kwa kufukuza watu hovyo na kutoa kauli za vitisho. Mngefahamu watumishi wanavyomfanya huyu jamaa mngesikitika sana
Kama mtu huna sifa za kufanya hiyo kazi hupaswi kufanya kuna watu wamesugua got kwa miaka mingi wakisomea fani mbalimbali halafu mtu akae kazini hajasoma ilihali na wasomi wapo ungekuwa wewe ungekubali?
Kuna sehemu jamaa kafanya vizuri lazima tuseme kama unavyo sema kuwa miradi mingi ilikuwa on going lakini unasahau kuwa kama Rais angekuwa na nia ivu hii mirada angeivuruga lakini aljchokifanya ni kuiendeleza tena Kwa kasi ya ajabu.
Kuna kitu mimi nilisha jifunza juu ya watanzania ni kuwa kamwe hawawezi kumsema vizuri Rais mpaka pale atakapo ondoka na hili litakuja kutokea trust me.
 
Mkuu barabara itasaidia mama anaeenda kuifungua afike haraka na salama, pesa zake za ada za watoto wake hatazipeleka tena shuleni ila atanunulia mahitaji mengine kwani ada serikali imefuta na vilevile upatikanaji wa huduma za afya na kwenye mashirika ya umma ni mzuri sasa hivi mwananchi hanyanyaswi tena kwani wafanyakazi wasio na maadiri waliokuwa wanafanya kwa mazoea tu (vyeti) hawapo tena wamebaki wale walio somea fani husika, hakuna kutumbuliwa.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Hakukuwa ma ada shule za msingi, shule za sekondari ada ilikua ni 24,000/-. Hizo huduma za afya ni wapi zimekua nzuri? Juzi hapo Muhimbili watoto wachanga wamekufa kwakukosa hewa, hiyo ndio huduma nzuri ya afya?
 
Hakukuwa ma ada shule za msingi, shule za sekondari ada ilikua ni 24,000/-. Hizo huduma za afya ni wapi zimekua nzuri? Juzi hapo Muhimbili watoto wachanga wamekufa kwakukosa hewa, hiyo ndio huduma nzuri ya afya?
Katika nyanja zote hawawezi kukamilika 100%,.
Unavyosema kuwa ada ilikuwa 24000 =/ unafikiri sasa hivi ipo na unadhani ilikuwa ni ndogo kwa wananchi?
Kufa kwa watoto inawezekana ikawa ni uzembe au vinginevyo lakini na hapo alaumiwe rais, hivi Muhimbili wanaweza wakakosa oxygen equipments kweli!
 
10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
Hosteli za UDSM!!na hili unaita mafanikio?,nchi hii INA vyuo vingi sana vya elimu ya juu,hii hostel mmoja,ni kama tone la maji kwenye bahari,tatizo la makazi kwa vijana wa elimu ya juu bado kubwa sana,
Angekuwa ametatua tatizo lote la makazi kwa wanachuo,ingekuwa sawa!,katika sekta hii bado sana,

Yaani kujenga,nyumba za askali magereza nayo unaita mafanikio,hii ni kitu minor sana,mafanikio,ingekuwa tatizo la makazi kwa askari wore nchini,limetatuliwa japo kwa asilimia 60,na hapa bado pia,
Unazijua nyumba za biskuti?fika Dodoma,hizo ndio nyumba wanazolala askari wetu,ni za udongo,wa kukandika,zimejengwa kwa kuwashurutisha wafungwa,
Rushwa,serikalini,haijaisha,ni kwamba watumishi wamekuwa wahoga,na nidhamu feki,na heshima ya woga,hakuna mifumo ya kuliendereza hili,
Tuambie fisadi gani kesi yake inaendelea ktk mahakama ya mafisadi,acha hizi kesi za watu wa chini,wanaouza mirungi,kumiliki magari 20,
Kesi za escrow,majizi yote yapo mtaani yanakula bata,

Watumishi wamekuwa waoga,wanaogopa kutumbuliwa,na kupoteza ajira,
Amesaidia kupunguza dhuluma ktk ofisi za umma,
 
Rushwa ndio imeingezeka sema haipigwi waz waz!!!! Mm ndo nakwambia na urasimu ni wa kutosha kama unabisha nenda TRA UONE WANAVYOONEA WAFANYA BIASHARA!!!
 
Elimu bure sawa lakini mbona idadi kubwa ya shule bado ni majanga? Kuna wanafunzi hawapati huduma muhimu kwa sababu ya elimu bure. Kuna isue za ukosefu wa maji, chakula, walimu n.k. Naona bado hatukuwa tumefikia ilitakiwa iwepo kwenye plan ya miaka kadhaa then utekelezaji uwepo.
 
Mafanikio mengine makubwa kabisa ambayo ni furaha kwake na watu wake ni kuitokomeza pumzi ya binti asie nahatia. Heko mzee baba
 
Ni kweli mafanikio ni mengi,tatizo kubwa kupungua kwa amani na umoja wa Watanzania.
 
Baadhi ya miradi ambayo mtangulizi hajaianzisha.
1. Uwanja wa michezo dodoma (kazi imeanza).

2. Ukarabati wa viwanja 11 katika mikoa 11.

3. Ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege dodoma .

4. Ujenzi wa ofisi za Nec, twakwimu, makamu wa rais, etc makao makuu dodoma

5. Ujenzi wa barabara ya njia 6 kutoka dar hadi kibaha.

6. Ujenzi wa barabara ya arusha kuanganisha kenya.

7. Ukarabati wa shule kongwe

8. Ukarabati wa vyuo vya ualimu vikongwe.

9. Ujenzi wa bomba la mafuta.

10. Ukarabati wa reli ya kaskazini.
Rambirambire maafa ya wana kagera
 
Mkuu barabara itasaidia mama anaeenda kuifungua afike haraka na salama, pesa zake za ada za watoto wake hatazipeleka tena shuleni ila atanunulia mahitaji mengine kwani ada serikali imefuta na vilevile upatikanaji wa huduma za afya na kwenye mashirika ya umma ni mzuri sasa hivi mwananchi hanyanyaswi tena kwani wafanyakazi wasio na maadiri waliokuwa wanafanya kwa mazoea tu (vyeti) hawapo tena wamebaki wale walio somea fani husika, hakuna kutumbuliwa.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Mbona lile jinga bashitte linalofanya kazi kwa mazoea kutumia jina la mtangazaji wa redio hivi hamulioni lipolipo tuuu na kutafuta kiki.
Mnazani ataendelea mpaka lini?
Mmeshindwa kumng'oa sasa asubiri muda ukifika atajua bashitte ni nani
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake Mpeni.

Nimekaa hapa nikawa natafakari utendaji kazi wa Rais wetu kipenzi “The Man himself President Magufuli”

Ki ukweli kazi kaifanya katika hii miaka yake miwili na nusu kwa sasa, achana na sisi tunaolalamika sijui maisha magumu mara mtaani pesa hakuna napenda kukuhakikishia kama hautaki kufanya kazi lazima tu maisa kwako yatakuwa magumu na utaendelea kumsingizia na kumchukia Mheshimiwa Rais bure.

Hebu jamani tujaribu kuona hapa mafanikio ya Mheshimiwa Rais japo kwa uchache na wale wajuvi zaidi watajaribu kinisaidia kwa kuongeza nyama

1. Tukianza na Sekta ya Elimu

Hili hata ungekuwa kipofu ata uwezi kubishana na mimi kuwa limefanikiwa kwa kiwango cha juu, nadhani tunakumbukumbu MH.Rais aliahidi elimu bure kuanzia Elimu ya msingi mpaka kidato cha nne na amefanya, sasa watoto wetu hatusumbuani maswala ya ada wala michango huko mashuleni kitu kilichopelekea wazazi wengi kupeleka watoto wao shule na ninahakika baada ya miaka kadhaa Tanzania itakua miongoni mwa nchi zenyeidadi kubwa ya wasomi.


Ukiangalia mpaka sasa kunaongezeko kubwa la wanafunzi wanaoandikishwa kujiunga na shule ya msingi. Mfano mwaka 2015 idadi ya wanafunzi wa shule ya msingi ilikuwa ni wanafunzi milioni 8,235… na kwa sasa tunajumla ya wanafumi miliono 10 na kitu unaweza kuona ongezeko lililopo hapo. Shule za sekpondari kwa mwaka 2015 tulikuwa na wanafunzi milioni 1,804056 kwa sasa tunawanafunzi takribani milioni 2,354234 kunaongezeko ku bwa sana hapo pia.

Mbali na kuongezeka kwa wanafunzi vifaa vya kufundishia na nyezo nyingine mashuleni vimeboreshwa mfano mzuri ni madawati, tatizo la madawati sasa limepungua kwa zaidi ya asilimia 80, walimu wa kutosha .



2. Tukija katika Nyanja au sekta ya Afya

Hapa napo hakuna mtui anaeweza kubisha ni kwa kiasi gani MH.Rais kajitaidi kutimiza kile alichokiahidi na badi muda anaomwingi sana kuendelea kuboresha na kukamirisha kile alichowaahidi watanzania, kipindi cha nyuma ilikua nadra sana ukaenda hospital ukamaliza kufaniwa tiba na kuandikiwa dawa ukaipata ile dawa uliyoandikiwa katika dirisha la hiyo hospitali ya serikali, sanasana utaambiwa uende duka lililo maali flani. Kwa sasa hiyo biashara haipo.


Serikali ya Rais magufuli imejitahidi sana katika swala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vingine, mfano MSD imeingina mikataba na umla ya wazalishaji wa dawa 110 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo wazalishaji 10 kutoka hapahapa nyumbani. Upatikanaji wa dawa muhimu kwa sasa umepanda hadi Asilimia 85 ukilinganisha na huko nyuma ambapo upatikanaji wa dawa muhimu haukufika hata asilimia 50.

Bajeti ya dawa na vifaa tiba kwa mwaka 2017-2018 ni bilioni 269 am bayo ni kama mara kumi ya bajeti ya mwaka 2015-2016 ambapo bajeti ilikua bilioni 29 tu.

Uboreshaji wa huduma mbali mbali mfano kwa sasa tunafanya upandikizaji wa figo hapahapa nchini kipindi cha nyuma wagonjwa wenye matatizo ya figo walitakiwa kupelekwa nje ya nchi. Hadi kufikia sasa hivi serikali imefunga mashine za upandikizaji wa figo zaidi ya 140 katika hospitali mbalimbali kitu ambacho ni maendeleo makubwa sana, hii ni kwa uchache tu.


3. Uboreshaji wa njia mbalimbali za usafiri na usafirishaji.

Hapa nitaongelea mifano mikubwa miwili ambayo ni Reli na usafiri wa anga. Tukianza na usafiri wa anga, hapa kila mtu atakuwa ni shahidi kuwa shirika letu la ATCL lilikua limekufa kabisa kilichokuwa kinasubiliwa ni mazishi tu, lakini huwezi kuamini lilivyofufuka ghafla baada ya MH.Rais kukamata madaraka tumeshuhudia haraka sana Rais alinunua ndege mbili aina ya Bombardier Q-400, sasa watu wanafika Kigoma, Dodoma, Katavi n.k kwa ndege kitu ambacho zamani ilikua hamna zaidi zaidi watu walitumia videge vidogo, lakini pia mwaka huu kuna madege mengina yatashuka ili kuimarisha zaidi usafiri wa anga ndani na nje bila kuisahau Boeing 787 itakayoleta balaa mjini.

Viwanja mbalimbali vya ndege vimeboreshwa ikiwemo kiwanja cha Mwanza, Mbeya, Bukoba na Julius. Pia kunaviwanja vipya vimejengwa na vinaendelea kujengwa maenep mbalimbali ikiwemo kile cha Chato.


Njoo kwenye Reli hapa ndio balaa lilipo Standard Gauge Railway ndio hiyo tena ikiwa ya kwanza katika nchi za Afrika mashariki na wengine wameamua kuiga mfano. Aitakuwa ajabu mtu kuishi morogoro lakini akawa anafanya kazi apa Jijini Dar es salaam. Hivi mnataka Rais afanye nini sasa, vitu ambavyo vilikua ndoto lakini sasa hivi ni halisi.



4. Ujenzi wa viwanda

Hili hata sina haja ya kulielezea maana kila mtu habari anayo


5. Vita dhidi ya Rushwa

Ili nalo sitakuwa na haja ya kulielezea naana kila mwenye akili timamu analijua. Wale ambao walikuwa wanaonekana malaika na mkono wa dola hauwezi kuwafikia habari wanayo na moto wanaona jinsi unavyowawakia kwa kujifanya mali ya umma ni ya kwao peke yao. Kwasasa mjini hapa akuna mbabe.


6. Ulinzi wa Raslimali zetu na Amani ya Nchi.

Hili nalo kila mtu ni shahidi, madini yetu kuwa watu walijifanya kama yao walichukua watakavyo na kuenda kuneemesha mataifa yao. Ambaye ana taarifa ni kitu gani kinaendelea apa anaruhusiwa kuniuliza nimpe habari.


Amani na utulivu naona kila mtu anashuhudia ni namna gani vinatamalaki. Akuna cha kuleta vyoko vyoko. Wale wote waliokuwa wakileta fujo fujo kipindi nchi hii ikionekana kama haina uongozi waijua ni nini hasa kinawapata kwa sasa. Kila nchi inautaratibu wake bana.



Nashukuru kwa leo na itaendelea…….
 
Back
Top Bottom