Hakuna kipindi rushwa imekomaa kama wakati huu, tumewazidi hata Kenya kwa rushwa, kaamua kuendesha nchi kama bar yake mambo anajiamulia tu anayoona yeye, ukweli kufeli kuna kiwango huyu kafeli kwa kiwango cha mwisho,
 
Hivi jaman tukiachana na masuala ya kujenga jenga pesa si angepeleka na sector nyingine. Ili mzunguko wa pesa uwe mkubwa.

Maana ukifuatilia makampuni mengi ya ujenzi ni ya foreigners so pesa haibaki nchini. Hivyo uchumi kuzidi kudorora zaidi
 
Watu wana sema kaleta nidhamu.nidhamu hailetwi kwa kufukuza watu hovyo na kutoa kauli za vitisho. Mngefahamu watumishi wanavyomfanya huyu jamaa mngesikitika sana
Na anapojidanganya huyu hajui kuwa watumishi wa umma sio watumishi wa Chama, hawana chakupoteza hata upinzani ukichukua nchi, polisi, walimu, madaktari, watabaki na kazi zao kama kawaida, kwahiyo ajue kabisa 2020 huyu akipata 30% ya kura zote nahama nchi hata kama upinzani utashinda
 
Hivi jaman tukiachana na masuala ya kujenga jenga pesa si angepeleka na sector nyingine. Ili mzunguko wa pesa uwe mkubwa.

Maana ukifuatilia makampuni mengi ya ujenzi ni ya foreigners so pesa haibaki nchini. Hivyo uchumi kuzidi kudorora zaidi
Mkuu hukusikia mwendo ni bidhaa kwa bidhaa debe la mahindi kwa Mbuzi 6. Wewe peleka nyanya debe utamuona doctor.

Ila hujatuambia hujaona mazuri ya Magufuli Kwa nchi hii?
 
Maendeleo ya vitu hata jakaya ameyafanya Magufuli cha maana alichofanya ni kukomesha Rushwa na kuleta nidhamu

Kakomeshaje Rushwa wakat hataki TV zioneshe Matatizo Kama ya Migogoro ya Ardhi ambayo chanzo chake ni Rushwa kwa watendaji?
 
Tuacheni mihemko tumsifu pale alipopatia maana nchi ilikuwa imeoza.
Fikiri mkuu hajaenda hata dubai kuosha macho kwa Uzalendo wake.

Wakati yupo Wizara ya Ujenzi alikuwa anaona kazi ngumu kuliko zote ni kusimamia Ujenzi wa Barabara !

Sasa hivi kapewa kazi ya kutafuta Hela na Makame Mbarawa ajenge Basi ndo Mikelele mpaka Mtaa wa Pili Mbona Mwenzie Jk alikuwa Kimya tu?
 
Ha ha imebidi nicheke. na kelele zote hizi haya ndio kayafanya. Kukomesha rushwa how , nidhamu makazini unaweza kuniambia how, airport mwanza na Dar pamoja na flyovers ni on going projects alizikuta. Alichofanya yeye ni kununua bombardier used 2 ,kujenga hostels ya wanafunzi na kupanua hicho kipande cha barabara ya moroko.
Nyingine tunasikia kila siku ni mikwara , vitisho na ubabe ,kabaki kusema fanyeni kazi. Tutaona hiyo 2020. Hajaanza hata km 50 ya lami toka aingie ikulu
Haya aliyoyafanya na kwa muda aliyoutumia, yule mzee mwenye mvi hata robo asingeweza kuyafanya.

Bombardier used, nyinyi wanafiki ndio mliokuwa mkipiga kelele kwamba nchi yenye watu milioni 50 haina ndege, zinakuja mnaanza kuongea kama walevi wa pombe za kienyeji.

Tatizo lenu la kukaa mbele ya laptop zeni Dar ndio hilo, hamjui wala hamtaki kufungua macho na kuona yanayoendelea nchi nzima. Mkoa wa Mbeya umebakiza vijijini chini ya kumi ambavyo havina umeme.
 
Back
Top Bottom