wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
474
1,000
Na Emmanuel J. Shilatu

Sifa kuu 3 zinambeba vilivyo Mwamba wa Afrika na jabari wa mageuzi ya kiuchumi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mpaka kufikia hatua Watanzania kuamua mwaka 2020 aendelee kutuongoza.

*A: UADILIFU*

Rais Magufuli amesimamia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ambapo wanaotuhumiwa kwa ufisadi Papa na ulaji rushwa wamepandishwa Mahakamani

Pia ameimarisha uwajibikaji, uadilifu na uchapa kazi kwa Watumishi wa umma nchini na kusimama kidete kufufua Mashirika ya umma yaliyokuwa taabani. Mfano shirika la ndege, shirika la simu.

Halikadhalika amefanya uchunguzi wa rasilimali za Taifa na kuweka makubaliano mapya kwenye sekta ya madini.

Rais Magufuli amedhibiti madawa ya kulevya na ujangili wa Tembo na Faru ambapo wameongezeka kuashiria kupungua kwa biashara ya nyara za Serikali.

Kwenye upande wa masuala ya kidiplomasia ameimarisha mahusiano mazuri na nchi jirani.

Haijawahi kutokea kwani Rais Magufuli ameweka uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za Taifa.

*B: UZALENDO*

Baada ya Mwalimu Nyerere anayefuatia ni Rais Magufuli kutoa Elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari ambapo Serikali hutumia Tsh. Bilioni 23 kila mwezi kulipia elimu bure.

Uonevu, ubabe, ubaguzi umepungua na ni sahihi kusema Rais Magufuli amepunguza uwepo wa matabaka ndani ya jamii.

Ni wazo la Mwalimu Nyerere lakini Rais Magufuli amekuja kulitekeleza la ujenzi wa mradi mkubwa wa Mto Rufiji wa kuzalisha umeme zaidi ya Megawatts 2115.

Rais Magufuli amefanikiwa kudhibiti matumizi ya hovyo ya fedha na fedha kuelekezwa zaidi kwenye miradi ya kimaendeleo.

Pia Rais Magufuli yupo imara na amesimamia ukusanyaji na matumizi sahihi ya kodi. Makusanyo yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 800 hadi kufikia Tsh. Trilioni 1.9 kwa kila mwezi.

Waliojipenyeza kwenye ajira Serikalini bila ya sifa amewaondoa. Hivyo JPM amefanikiwa kudhibiti vyeti feki na mishahara hewa na kubaki historia nchini.

Leo hii Watanzania tunajivunia nchi yetu, viongozi wetu, rasilimali zetu na utaifa wetu. Hivyo JPM Ameimarisha UZALENDO nchini.

Hakuishia hapo amerudisha mashamba na viwanda vilivyobinafsishwa na havikuendelezwa.

Leo Taifa linanufaika na madini kwani amedhibiti usafirishwaji wa makinikia na hayaendi kuchenjuliwa tena nje na madini yanauzwa hapa hapa nchini kupitia masoko ya madini yaliyoanzisha maeneo mbalimbali yenye madini. Huu ni uzalendo wa kuigwa wenye tija vizazi na vizazi.

*C: UCHAPA KAZI*

Leo hii Serikali imehamia Dodoma na mpaka Rais Magufuli nae pia amehamia Dodoma. Walisema haiwezekani lakini nia ya dhati na uchapa kazi wa Rais Magufuli na Serikali yake imedhihirisha inawezekana.

Baada ya reli ya Mkoloni yenye zaidi ya miaka 120, leo hii Rais Magufuli ameanzisha Ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme ya SGR ambayo ni reli ya kisasa, yenye kasi na inayobeba mizigo mingi.

Sera ya Tanzania ya viwanda ipo kivitendo. Leo hii kuna ujenzi wa viwanda vipya zaidi ya 3000.

Rais Magufuli aliapa kuilinda katiba ya nchi ambapo kuna uimarishwaji wa amani na Uhuru wa kidemokrasia ndani ya nchi. Mathalani Umoja wa Mataifa (UN) umempongeza Rais Magufuli kudumisha amani na usalama ndani na nje ya nchi.

JPM amesimamia vyema ukuaji wa uchumi uliokuwa na kufikia 7.1%

Kwenye afya napo pamenoga kuna ujenzi wa vituo vya afya kila kata na ujenzi wa Zahanati kila kijiji.

Serikali ya Rais Magufuli imedhibiti maandamano ya kisiasa na ya kijamii (Mf. Wanafunzi, Madaktari) na sasa yamebaki historia.

JPM amenunua ndege mpya 8 za kisasa na Leo hii ATCL imefufuka inachanja anga za kitaifa na kimataifa.

Ameweka mikakati mizito ya kupunguza foleni kwa Ujenzi wa flyover ya Tazara na interchange ya Ubungo.

*Na Shilatu E.J*
 
Sep 21, 2020
20
45

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea. Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika, hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio. Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika namsifu Rais wetu.

Pia soma;
- Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania
Kwa haya aliyo yafanya hakuna budi akipata mitano tena aendeleze alipoishia ingawa demokrasia ndio itakayo amua
 
Oct 6, 2020
24
75
July 1, 2020 is the date that will go down as remarkable day in Tanzania history as the first and starting date for implementation of the fifth and final Government Budget to end the first five years of the fifth regime but more important a day the World Bank recognized Tanzania as a middle-income country, five years before reaching 2025.

In discussing these achievements I would like to remind seven( 7) key success stories which will go down as remarkable international records to interpret these achievements;

#First, I keep in mind that all who were asking and challenging on what kind of nation President Magufuli is building , July 1, 2020, the World Bank have responded! That Magufuli was building a middle income nation.

# Second, Is the record released by the International Monetary Fund(IMF) through the former Director of the Organization, Ms. Christine Legarde when interviewed by Quartz Magazine, in 2017 in Ethiopia.

When asked which African countries are heading to Vietnam industrial revolution, She cited Tanzania, Ethiopia, Nigeria and Kenya. Again this was the answer to those who were questioning whether President Magufuli Government is really building an industrial economy.

# Third record is the one released at the World Economic Forum 2018, where Tanzania was ranked the leading African nation for an inclusive economy in Africa South of Sahara. This record cementing the fact that Magufuli government is indeed a pro-poor government.

# Fourth record is where the Government of Tanzania was ranked 28th out of 186 nations surveyed in the world for effective management of public finances. , this record defeated so many countries in the world. Our competitors in EAC & SADC Blocks were ranked as follow; Kenya (70), Uganda (100), Malawi (106), Mozambique (118), Ghana (61), Botswana (37). This record proves that even the world recognizes President Magufuli is building a disciplined spending government with a great record not only in Africa but in the world. This is according to a report by the World Economic Forum, Executive Opinipn Survey 2019).

# Fifth record, Tanzania was named as the leading nation out of 37 African countries surveyed in the fight against corruption. This is according to The Africa global opinion survey 2019.

We suppose to appreciate that we have come a long way, the era of renting a plane for 43 million dollars but working 6 months and finish the rest 37 months of contract in garage (refer to CAG report April 2020).

Today the government purchases new aircraft bombardier for $ 32 million! This is just a small example to show that as a Nation there are decades we lost!

# The sixth record comes from African Global opinion survey report of 2019 which shows citizen trust to their government has increased tremendously. It revealed that 72%had trust to their government in fighting corruption compare to 13% in 2015 .This is one of the recordings of a major revolution in the world.

# The Seventh Record comes from the number one global Credit Rating Agency, the MOODYS.

According to MOODYS Credit Rating Agency, which own 45% of global market share, rated Tanzania higher than any East Africa country with B1 leaving the rest with B2 ranking in 2017 report. This assessment is the first of its kind in Tanzania since independence.

These are global records and will remain so as President Magufuli international identity let alone the great diplomacy he used to confront COVID19 and leave the rest of the world wondering how it was possible for a corona pandemic that shaken the whole world but failed in Tanzania.

What I am emphasizing here is that while Magufuli achieves such a great international record, it should be noted that he come into power in 2015 when the government was unable desperate and unable even to manage wagebill!.

He received a Government that had to borrow to finance wage bill (desperate government)! but within 5 years he achieved a great record in every sector related to human development !.

He has succeeded in building an economically strong Government in all economic interpretations in the world.

Those of us who were familiar with these records are not surprised to hear Tanzania being declared qualified to enter the middle income economy 5 years before the target year which is 2025.
 
MIMI BABA YENU

Senior Member
Mar 1, 2019
185
500
Katika miaka mitano ya muhula wa kwanza wa uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli licha ya kuwa ni Muumini wa dini ya Kikristo amekuwa akiongoza nchi kwa kushirikiana vema na viongozi na waumini wa dini ya Kiislam pamoja na waumini wa Madhehebu mengine yaliyopo Nchini.

Uongozi wake umekuwa una usawa kwa watu wa dini zote pasipo kuipendelea dini yoyote.

Pia, kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mhe. Rais Magufuli katika kampeni amekuwa akiwasisitiza wananchi kuwachagua viongozi pasipo kutazama itikadi zao za kidini bali watazame sera ambazo zinalenga kuliletea Taifa maendeleo.

Katika kudhihirisha kuwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli abagui dini, amejenga msikiti Wilayani Chato ambao una uwezo wa kubeba waumini 5000 kwa wakati mmoja.

Pia Mhe. Rais Magufuli amewezesha mchakato kujengwa kwa msikiti mkubwa Kinondoni jijini Dar es salaam ambao aliiomba Serikali ya Morocco ijenge, ili waumini wa dini ya kiislamu wapate msikiti mkubwa ambao utawewezesha waumini wengi kuswali mahala pamoja kwa wakati mmoja.

Kadhalika, Mhe. Rais Magufuli alichangisha zaidi ya Shilingi Milioni 40 katika Uzinduzi wa Kanisa la Katoliki Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Chamwino Jijini Dodoma, kutokana na watu wa dini mbalimbali kuchangia fedha za ujenzi wa kanisa hilo.

Hakika tumepata Rais Mcha Mungu na anayewapenda wananchi wote pasipo kubaga imani zao za kidini.

Mungu Mbariki Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Baba Masagu

Senior Member
Aug 30, 2020
129
225

We Tanzanians with nationalism aspects do highly admire and respect the efforts of our lovely President Dkt JOHN Pombe Magufuli which leads our country through so many achievements including few stated above.
We know much of what had happened in these short time of five years.
Big up for JPM and CCM.
We are praying for you to win over 85% in your second term 2020-2025.
God bless us.
 
Sep 22, 2020
85
125

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea. Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika, hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio. Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika namsifu Rais wetu.

Pia soma;
- Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania
Hakika ni mengi ameyafanya bado watu hatutaki kuamini.
Mi nauliza mbona wanaopinga ndio haohao wanaotumia vitu hivyo ???

Swala ni kwamba kumbe wanatukubalineeeh hahahha wataendelea kuisoma namba mpaka wakome mwaka huu.

Kama kuna mtu anaona hajafanya chochote basi wahame nchini waende nchi jirani huko mbona wanaruhusiwa tu jamani.
 
Sep 20, 2020
47

Hana mpinzani huyu Baba, kwa mapenzi ya dhati aliyonayo kwa Taifa letu na kwa sisi wananchi kiukweli anastahili miaka mitano tena.
Nitamchagua Magufuli
 
Sep 20, 2020
73
125
Hana mpinzani huyu Baba, kwa mapenzi ya dhati aliyonayo kwa Taifa letu na kwa sisi wananchi kiukweli anastahili miaka mitano tena.
Nitamchagua Magufuli
Kumbe hata na wewe unalitambua hilo?
#Tulipotokatunapokwenda
#MagufuliNiMafanikio
#AchaKaziIendelee
#hapakazituu

Hakika vijana tukiwa nguvu moja hakika TAIFA hili halitachukuliwa na mabeberu
 
Sep 20, 2020
73
125
Hakika ni mengi ameyafanya bado watu hatutaki kuamini.
Mi nauliza mbona wanaopinga ndio haohao wanaotumia vitu hivyo ???

Swala ni kwamba kumbe wanatukubalineeeh hahahha wataendelea kuisoma namba mpaka wakome mwaka huu.

Kama kuna mtu anaona hajafanya chochote basi wahame nchini waende nchi jirani huko mbona wanaruhusiwa tu jamani.
HASWAaaa ila kwakua watu tunataka mpaka tubustiwe ndio tuelewe

ILa kwa miMi kaMa kijana mzalendo na mpenda maendeleo ninasema aliyoyafanya Magufuli ni mengi sana sina budi 28/10/2020 kumpa kura yangu.
 
Sep 20, 2020
73
125
Katika miaka mitano ya muhula wa kwanza wa uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli licha ya kuwa ni Muumini wa dini ya Kikristo amekuwa akiongoza nchi kwa kushirikiana vema na viongozi na waumini wa dini ya Kiislam pamoja na waumini wa Madhehebu mengine yaliyopo Nchini.

Uongozi wake umekuwa una usawa kwa watu wa dini zote pasipo kuipendelea dini yoyote.

Pia, kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mhe. Rais Magufuli katika kampeni amekuwa akiwasisitiza wananchi kuwachagua viongozi pasipo kutazama itikadi zao za kidini bali watazame sera ambazo zinalenga kuliletea Taifa maendeleo.

Katika kudhihirisha kuwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli abagui dini, amejenga msikiti Wilayani Chato ambao una uwezo wa kubeba waumini 5000 kwa wakati mmoja.

Pia Mhe. Rais Magufuli amewezesha mchakato kujengwa kwa msikiti mkubwa Kinondoni jijini Dar es salaam ambao aliiomba Serikali ya Morocco ijenge, ili waumini wa dini ya kiislamu wapate msikiti mkubwa ambao utawewezesha waumini wengi kuswali mahala pamoja kwa wakati mmoja.

Kadhalika, Mhe. Rais Magufuli alichangisha zaidi ya Shilingi Milioni 40 katika Uzinduzi wa Kanisa la Katoliki Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Chamwino Jijini Dodoma, kutokana na watu wa dini mbalimbali kuchangia fedha za ujenzi wa kanisa hilo.

Hakika tumepata Rais Mcha Mungu na anayewapenda wananchi wote pasipo kubaga imani zao za kidini.

Mungu Mbariki Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania.
KWa mambo aliyoyafanya Dr MAGufuli ni mengi na hayawezi elezeka kabisa.NDIO maana kuna muda hua namfananisha na BABA wa TAIFA hili mwal.Nyerere hawa ni watu wenye maono ya kutosha

KURA YANGU KWA MAHGUFULI
 
Bigbootylover

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
2,828
2,000
Anaandika Sheikh, Dr Yahya Msangi(PHD).
LOME, TOGO.
SANAA YA MAANDAMANO NA SIKUKUU: NYUMA YA PAZIA KUNA WAKUBWA

Ni vyema wenzangu mkaelewa yanayojiri nchi nyingine ili mtafakari kwa makini.

Kumekuwa na harakati za kuandaa maandamano nchi mbalimbali Afrika toka kipite kimbunga cha ARAB SPRING. Kipunga kiklichoanzia Tunisia kikasambaa kwa kasi Misri. Lakini wengi hamjui mlengwa haswa wa kile kimbunga cha facebook na tweeter alikuwa nani. Hakuwa Tunisia wala hakuwa Misri!

Baada ya kumuua Sadam wababe wa kimagharibi walilenga mitutu na makombora yao kwa Algeria, Libya na Syria. Wengi mnajua kuhusu kilichofanywa Libya na sasa Syria. Lakini wengi hamjui kuhusu Algeria.

Algeria ni nchi ya 10 kwa ukubwa duniani (geographically). Nchi kubwa kama hiyo haikosi kuwa na mali asili zinazowatoa mate mafisi makubwa! Lakini pia Algeria imepakana na kina Morocco, Mali, Tunisia, Libya, Niger, Mauritania na Sahara ya Magharibi. Kutokana na hili Algeria inapakazwa kuwa ni mfadhili mkubwa wa vikundi vya kigaidi! Hakuna ushahidi wowote ila hila hii inafanywa ili kupata sababu ya kuivamia na kuivuruga Algeria.

Mfaransa bado hajamsamehe Algeria kwa kiichowakuta enzi ya vita ya ukombozi! Mfaransa bado anayataka mafuta ya Algeria. Mfaransa anaona Algeria ndio inaofadhili wa TOURAG wanaompiga vita kutokana na wizi wa Uranium kaskazini mwa Chad na Mali! Wapiganaji wa kitourag walikuwa wakihifadhiwa na Gadaffi. Watourag wanatetea mali zao na nchi yao iliyotwaliwa kwa mabavu na kampuni ya kifaransa inayochimba uranium! Kuna taarifa zisizo na shaka kuwa umeme woote unaowaka ufaransa unatokana na Uranium inayoibwa Chad na Mali. Mazingira, wanyama na watu wamelemaa kwa athari za uranium mfaransa hajali! Wakubwa wamefumba macho! Mijizi combined! Baada ya Libya kuvamiwa sasa ni Algeria inatafutwa! Ukumbuke Algeria ina utajiri mkubwa wa mafuta! Algiers na Cairo ndio miji pekee Africa in aundergroung transport system ya hadhi ya kimataifa!

Arab spring ililenga Algeria ikaja bahati mbaya akabondwa Tunisia na kipenzi chao Misri! Ndio maana pamoja na arab spring kupamba moto Misri na Tunisia zimekufa kifo cha mende! Waliokuwa nyuma ya Arab Spring walipoona mlengwa kakwepa wakatuliza ngoma! Vijana wa facebook na tweeter wakaumia buree!

Sasa kuna nchi 2 maandamano yanatumika kutaka kuzivuruga. Ni Tanzania na Togo. Kila moja na sababu zake tofauti.

Tuanze na Togo.
Togo ni kanchi kadogo kabisa barani Afrika. Nadhani ni Sao Tome na Principe pekee ndio ndogo kuliko Togo. Wakazi wa Togo ni kama milioni 8 hivi na mji mkuu wa Lome una wakazi takriban milioni moja. Ni mji ambao kwa tuliozoea Dar hauna mikikimikiki kabisa. Togo haina madini isipokuwa ina bandari maarufu toka enzi za ukoloni. Ikitumika kama bandari maalum kwa makoloni ya Ufaransa. Kwa kipindi cha kuanzia mwaka jana Togo imekabiliwa na maandamano mawili au matatu kila wiki! Mjumuiko wa vyama vya upinzani hapa (unaweza kuwaita UKAWA TOGO BRANCH) vimekuwa vikiandaa maandamano haya. Yamesababisha watu kufa na mali kuharibiwa kila yanapoitishwa. Ilishangaza watu ni wapi watu hawa ambao vyama vyao ni dhaifu mno walipotoa fedha za kuendesha maandamano kila wiki? Pia ikashangaza wengi ni kwa nini maandamano haya yamechukua sura ya udini? Baadhi ya mashehe na misikiti imetumika sana. Inashangaza kwa kuwa asilimia 54 ya watogo wanaamini vodoo!

Lakini wengine tunajua chanzo!

Mwaka jana Netanyahu alijitahidi kupitapita nchi mbalimbali za kiafrika na hata kuhudhuria kikao cha wakuu wa nchi za Afrika mjini Addis na kuhudhuria sherehe za kumuapisha Uhuru mjini Nairobi japo hakwenda kiwanjani! Netanyahu huyo huyo aliitisha kikao cha wakuu wa nchi za kiafrika wakati wa kikao cha UN General Assembly mjini New York kikao ambacho Kagame aligoma kuhudhuria! Agenda kuu ya Netanyahu ilikuwa kuomba nchi mojawapo ikubali kuandaa IZRAEL AFRICAN SUMMIT ili tu aonyeshe Izrael inakubalika Afrika na ili kuwadhibiti Wapalestina baada ya Taifa lao kutambulika. Izrael inamezea mate kiti Baraza la Usalama na inadhani Afrika itaunga mkono siku wakiwasilisha ombi. Katika harakati zake hizi alifanikiwa kuishawishi Togo iandae hiyo Summit.

Kabla hata Togo haijaanza maandalizi maandamano yakaanza! Nia ni kuizuia isiandae hiyo Summit na wahusika wanaungwa mkono na mataifa yoote ya kiarabu na baadhi ya mataifa mema ya Ulaya. Wanapinga Afrika kumpa Netanyahu karata ya kuendelea kuikandamiza Palestine na watu wake!

Kweli summit imeshindikana kuandaliwa kutokana na hizi vurugu lakini pia kutokana na mataifa mengi ya Afrika kuiambia Togo utahudhuria wewe na Netanyahu hiyo Summit! Hii ndio hali tete iliyopo Togo hivi sasa. Kuna maandamano ambayo nguvu inatoka nje! kelele za uchaguzi, tume huru, uvunjifu wa haki ni geresha tupu!

Turudi Tanzania
Toka JPM adhibiti uporaji wa kimataifa kwa kiwango cha kutishia maslahi ya nje pameibuka watu ambao kutwa kucha wanawaza maandamano! Huhitaji akili ya ziada kujua ni wao au wanaowalipa! Kwa ilivyo Tanzania wamekwama ila msiwadharau kamwe! Tayari wameanza kuingiza udini kwenye harakati zao! Tumeanza kuona baadhi ya viongozi wa kiroho wakigeuka kuwa wanasiasa! Hawakemei mambo ya kiroho wanakemea mambo ya kisiasa! Utashangaa kiongozi wa kiroho hakemei watu kusoma misa ya wafu mbwa! Hawakemei kiongozi wa kiroho kutoka hadharani na kumtukana kiongozi mwenzao wa kiroho eti ni mjinga na kala maharage! Wao kwao haya ni sawa! tatizo kwao ni katiba ya nchi!

Hapa Togo maandamano yamefikia ukomo! Serikali iliwakusanya viongozi woote wa UKAWA na kuwafungia ndani toka alfajiri hadi usiku wa manane wiki mbili zilizopita baada ya wao kutangaza maandamano tena! Wiki imepita sasa bila maandamano! Waandamanaji waliokuwa wakilipwa wamerejea makwao!

Najua Tanzania leo haikuwezekana ila serikali isidhani yameisha! Kuna watu na mataifa yanatamani amani itoweke wapenye kama walivypenya DRC, Libya, Syria, Iraq, Afghanistan, Somalia, Sudan na kwingineko! Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa sana uliokuwa ukinufaisha wengi! Sasa unanufaisha Tanzania imekuwa nongwa.

Serikali itafute dawa ya kukomesha maandamano! Haiwezekani maandamano yakafanywa ni mchezo wa kitoto! Maandamano yanayoshinikizwa na watu wa nje ni uhaini! Wahusika watendewe kama wahaini!

Najua makala ni ndefu lakini soma!
Hakuna kitu hapo, tumegawanywa tu sasa hivi hakuna umoja tena, viongozi wetu wanatakiwa kutuunganisha na kututendea inavyofaa, uzalendo umeshuka sana kutokana na yale wananchi wanayofanyiwa, hakuna mtanzania anayependa amani iliyopo itoweke lakini hiki kinachoendelea kwa sasa nchini kuna watu wanaona bora tukose wote. Ombi ni viongozi wasimame Kwenye HAKI waone kama Adui ataingia nchi hii, watu hawako tayari tena kuteseka ili wachache wafaidike. Na hapo ndipo viongozi wanapotudanganyia eti kwamba Wapinzani wanatumika! Acheni kutudanganya
 
Baba Masagu

Senior Member
Aug 30, 2020
129
225
KWa mambo aliyoyafanya Dr MAGufuli ni mengi na hayawezi elezeka kabisa.NDIO maana kuna muda hua namfananisha na BABA wa TAIFA hili mwal.Nyerere hawa ni watu wenye maono ya kutosha

KURA YANGU KWA MAHGUFULI

KWa mambo aliyoyafanya Dr MAGufuli ni mengi na hayawezi elezeka kabisa.NDIO maana kuna muda hua namfananisha na BABA wa TAIFA hili mwal.Nyerere hawa ni watu wenye maono ya kutosha

KURA YANGU KWA MAHGUFULI

IMG_7718.jpg

IMG_7719.jpg

IMG_7717.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom