Hata kama ni kampeni, si vema kumdanga mtu mzima mwenye akili timamu ambaye pia si kipofu. Wafanyabiashara wengine ni sisi na tunaona kodi ilivyobana. Ndugu yangu alifunga duka Kariakoo kwa sababu ya kodi kubwa. Katika familia yetu kuna vijana 4 walimaliza chuo bila ajira hadi sasa. Bei za vitu madukani kwa miaka hii ziko juu kuliko 2015, mfano, sukari. Shuleni hakuna walimu wa kutosha kwa kuwa hakuna walimu walioajiriwa kipindi hiki cha miaka 5. Wana vijiji waliahidiwa mlioni 50 kila kijiji hawakupewa hivyo hawana furaha, komputa mpakato walizoahidiwa? Hawana furaha. Wafanyakazi hawakupandishwa mishahara wala madaraja hivyo hawana furaha. Uchumi wa kati ni suala kisomi ambalo mwananchi wa kawaida halielewi kwa kuwa haliakisi maisha yao moja kwa moja. Uchumi wa kati na maisha magumu.... ! Hata bima yua afya kwa wanayoitumia wamepunguza aina za dawa na baadhi ya huduma zinazolipiwa na bima, zahanati vijijini hakuna dawa za kutosha, na hakuna waganga na wauguzi wa kutosha na kila skta iko hoi.
Watu hawaji kwenye mikutano yenu kwa hiari zao. Shule zinafungwa na wanafunzi wanatakiwa wavae kiraia wahudhurie, ofisi zinafungwa na wafanyakazi wanatakiwa kuhudhuria kwa lazima, malori yanakodiwa kuleta watu kutoka mbali ambapo wale wa mbali sana hupewa elfu 5 ya kula na kadhalika. Magazeti yote, radio zote, tv zote mnatumia ninyi. Hata mango yote ya uraisi ni ninyi tu, hivyo watu hawafuriki kwa sababu ya furaha na kuridhika. Hali ni mbaya ila basi tu!
popote ulpo agza chakula ntakuja kulpa umeongea fact saaaaan✌️✌️✌️
 
Mkuu nilichosikia mitaani ni kwamba wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, graduates na wanavyuo, October 28, 2020, eti WANA JAMBO LAO. :D

Hapa napeleleza jambo lipi?

Everyday is Saturday...............................:cool:
Baada ya uchaguzi,huu msemo wenu utakuwa hivi " 2025 TUNA JAMBO LETU" 😂😂😂😂
 
CCM inatumia nguvu kubwa kupata ushindi kwa kujiharibia yenyewe, sehemu waliposhinda upinzani ndo vijana, wamama, bodaboda, wababa wananufaika kwa mikopo, hongo na maendeleo mfano Arusha, Mbeya, Moshi, Iringa nenda Mwanza walipomchagua Wenje na sasa vijana wanalia wamesaulika sasa hapo utamshawishije mtu achague CCM akose maendeleo Kama kijijini hata Sasa hivi kawe watu wanakula kwa Ngwajima kwasababu ya upinzani na kwenye ngome ya upinzani hela nje nje.
 
CCM inatumia nguvu kubwa kupata ushindi kwa kujiharibia yenyewe, sehemu waliposhinda upinzani ndo vijana, wamama, bodaboda, wababa wananufaika kwa mikopo, hongo na maendeleo mfano Arusha, Mbeya, Moshi, Iringa nenda Mwanza walipomchagua Wenje na sasa vijana wanalia wamesaulika sasa hapo utamshawishije mtu achague CCM akose maendeleo Kama kijijini hata Sasa hivi kawe watu wanakula kwa Ngwajima kwasababu ya upinzani na kwenye ngome ya upinzani hela nje nje.
Ni kweli ukiwa ccm mambo safi
 
WanaJF, Takwimu hazidanganyi kwa wale waliosoma takwimu za kimataifa ni dhahiri tupo uchumi wa kati.

Kampeni za CCM zimepelekea maelfu ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara kujaza viwanja na kufurika.

Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania sasa wanapatiwa elimu bora kuliko wakati wowote ule tangu uhuru wa Taifa hili, wanafunzi hawa wanaajirika na kukubalika kimataifa.

Leo hii wafanyakazi wa serikali na wale wa sekta binafsi wamepunguziwa kodi kwa asilimia kubwa sana kuanzia mwezi July 2020. Punguzo la kodi limeongeza uwezo wa jamii kuuza na kununua.

Upande wa wafanyabiashara kodi zimekuwa rafiki zaidi ukilinganisha na miaka mitano kabla ya JPM, Wafanyabiashara wanaruhusiwa kulipa kodi kwa majadiliano na Mamlaka ya mapato TRA.

Aidha, Maelfu ya wanafunzi wameajiliwa serikalini kuanzia mwaka 2014. Sekta ya afya zaidi ya madaktari mia sita wameajiriwa,Karibuni zaidi ya ajira elfu kumi na tatu za walimu zimetangazwa.

Kwa upande wa wakulima mambo ni mazuri zaidi, Wakulima wa nafaka na mikunde serikali imeimarisha uhimilivu wa bei hivyo bei kutoyumbishwa na madalali wachache,Hali hii imepelekea wakulima kulima na kuuza kwa wakati,Zao la korosho limeimarika kwa kipindi cha miaka mitano baada ya serikali kuingilia kati watu waliotaka kushusha bei kwa manufaa binafsi,Serikali iliamua kununua korosho zote na kulipa kwa wakati.

Ni furaha,na Upendo kila kona ya nchi hii,Mzunguko wa pesa ni mzuri kwa wajasiriamali walio wengi na hii imepelekea kila mtu kula ,kununua na kufanya atakalo bila kuvunja katiba ya nchi.

Tutashinda kwa mbinu za kisasa zaidi kwa maendeleo ya watanzania wote.

Hoja hujibiwa kwa hoja bali si kwa matusi,Mwenye kupinga alete takwimu zake hapa JF.

Je, hatupo uchumi wa kati?
Je, wanafunzi graduate wa udaktari na ualimu hawajaajiriwa?
Fake ID nyingi za MATAGA mmeshalipwa posho zenu? Maana tunasikia mmelalama ukata!!

Hayo mambo yako ya kijinga andikiaa Meko huko sis sio wajinga mbuzi wewe
 
Kama kuna mafanikio mbona kuzuia watu wasitoe dukuduku lao? Mbona kuzuia wakosoaji wake wote wasiseme alikoharibu? Uharibifu ni mwingi sana kuliko mafanikio. Katika kipindi hichi cha Magufuli ndio kipindi deni la Taifa limepaa kuliko nyakati nyingine zote tena wizi na rushwa vimepamba moto, miladi mingi yenye mikataba ya kifisadi imefanyika chini ya Magufuli uku uchumi wa nchi ukisinyaa, uchumi wa mtu mmoja mmoja ukishuka kwa kasi ya ajabu uku haki za kirahia zikiendelea kuporwa.
Kwa uandishi wako tu wa hili neno urahia badala uraia inaonyesha wazi kuwa hata hujui kinachoendelea nchini ila tu unafata upepo kama bendera

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
CCM inaamini kwamba uzalendo kwa nchi ndio msingi wa maendeleo ya
kweli ya Tanzania ambayo yataletwa na Watanzania wenyewe
IMG-20200930-WA0180.jpg
 
66 Reactions
Reply
Back
Top Bottom