Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2020

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,098
2,000

Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

============
emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Namsifu Rais wetu...

Pia soma;
- Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania
 

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,098
2,000
Inafika mahali unashindwa kuelewa watanzania wanataka nini hasa?

Kama ni maendeleo yanaonekana kwa macho, tena hayana vyama pande zote za nchi watu wameneemeka.

Huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu imeboreshwa mara dufu, miundombinu ndio usiseme.

Treni ya Moshi - Arusha imerejea, ndege kadhalika meli na vivuko vimehuishwa.

Ninapotafakari watu hawa wanataka wafanyiwe nini nakumbuka maneno ya baba wa taifa mwalimu Nyerere kwamba ili nchi iendelee inahitaji Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi bora.

Watanzania tunafeli wapi hadi kukumbatia siasa za kishabiki?

Au kuna watu wameamuwa kuwa na fikra za kipinzani tu? Maana hata shetani hapingi kila jema liletwalo na Mungu.

Niishie hapo.
Mbona wilaya ya Magu mkuu wako kasema hapeleki maendeleo kisa n Mbunge wa upinzani na kodi wanalipa je n kona ipi unayosema?
 

Baba Masagu

Member
Aug 30, 2020
21
45
Mbona wilaya ya Magu mkuu wako kasema hapeleki maendeleo kisa n Mbunge wa upinzani na kodi wanalipa je n kona ipi unayosema?
Unaropoka tu. Fanya tathmini kwanza utaona maendeleo yalivyoelekwa kila kona ya nchi hii bila kujali mbunge ni wa chama gani . Hebu angalia hapo dar basi kidogo .
Upinzani wa kukataa hata ukweli ni upuuzi
 

kunogasana

Member
Nov 10, 2019
32
95
Nahisi kuna tatizo baadhi ya maeneo, au hawajaelewa nini mgombea wetu alimanisha jana kuhusu kufunga mkono mwalimu self
IMG-20200908-WA0038.jpg
 

magufuliforpresident

Senior Member
Aug 18, 2015
159
225
Katika Masuala ya jumla na ya kimataifa Tanzania imeweza kuongeza mapato, kutoka wastani wa shilingi bilioni 850 hadi shilingi Tilioni 1.5, Kuongeza makusanyo ya madini kutoka shilingi bililioni 160 hadi shilingi bilioni 528 mwaka 2019/2020. Kadhalika kuongeza makusanyo ya Halmashauri kutoka takribani shilingi bilioni 379 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 713.3 mwaka 2019/20. #MIAKAMITANOYAMAGUFULI
 

CCMkuelekeaUchaguzi

Senior Member
Aug 18, 2015
176
225
“Kumekuwa na ongezeko la mapato kwa Wachimbaji wakubwa. Mwaka 2016 waliuza dhahabu kilo 17,587.15 yenye thamani ya Dola za Marekani Mil 607.3 sawa na shilingi tilioni 1.4, Serikali ilipata Mrabaha wa thamani ya Dola za Kimarekani Mil 23.4 sawa na shilingi bilioni 53.81. Hadi mwezi Mei, Mwaka 2020 wameuza Kilo 21,652.77 zenye thamani ya Dola za Kimarekani Mil 949.8 sawa na shilingi tilioni 2.2 na kutoa Mrabaha wenye thamani ya Dola za Kimarekani mil 56.8 sawa na shilingi bilioni 130.64 “ #kazizaidi
 
Aug 18, 2015
82
125
Katika Sekta ya Kilimo, ufugaji na Uvuvi kwa Miaka mitano iliyopita Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufuta Tozo 114 kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi. Katika kipindi kijacho Serikali imejipanga kutengeneza machinjio ya kisasa, kuendeleza na kujenga Maghala ya kuhifadhi na Vituo vya kuchakata mazao. (Ilani ya Uchaguzi Uk 33-56)
Adjustments.jpg
 

jo mose

JF-Expert Member
Aug 5, 2020
1,725
2,000
Pale mtetezi wa wanyonge anapowaletea umasikini wanyonge uleta shaka juu ya uzalendo wake. Mtetezi wa wanyonge katu hawezi Kuwasomesha namba wanyonge ili wawe masikini ili wamuabuduhttps://youtu.be/N7QJEFijpb4
 

Sammio_tz

Member
Dec 30, 2017
9
20
Pale mtetezi wa wanyonge anapowaletea umasikini wanyonge uleta shaka juu ya uzalendo wake. Mtetezi wa wanyonge katu hawezi Kuwasomesha namba wanyonge ili wawe masikini ili wamuabuduhttps://youtu.be/N7QJEFijpb4
Hii ni kauli ambayo ni mbaya Sana, Kwa Nini kuongoza wanyonge tuu badala ya kuongoza watu wenye uwezo wa kujinasua kimaendeleo ili tuwe Katika viwango vya kutotumika na wanasiasa Kwa maslahi yao binafsi, so disgusting kuita wanyonge!
 

Mpenda maendeleo Tz

New Member
Sep 20, 2020
4
0
Hii ni kauli ambayo ni mbaya Sana, Kwa Nini kuongoza wanyonge tuu badala ya kuongoza watu wenye uwezo wa kujinasua kimaendeleo ili tuwe Katika viwango vya kutotumika na wanasiasa Kwa maslahi yao binafsi, so disgusting kuita wanyonge!
NAfikiria kwanza,lakini bado mawazo yako yananipa mashaka kidogo.Japo nchi hiii inampa kila mtu uhuru.
 

Mpenda maendeleo Tz

New Member
Sep 20, 2020
4
0
Katika Sekta ya Kilimo, ufugaji na Uvuvi kwa Miaka mitano iliyopita Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufuta Tozo 114 kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi. Katika kipindi kijacho Serikali imejipanga kutengeneza machinjio ya kisasa, kuendeleza na kujenga Maghala ya kuhifadhi na Vituo vya kuchakata mazao. (Ilani ya Uchaguzi Uk 33-56) View attachment 1564651
WASITUGAWE
Serikali ya Ccm Imedhamiria kuendelea kuwa nchi isiyofungamana na upande wowote ili kuweza kutetea na kulinda masilahi ya nchi yetu kwa kuzingatia misingi tunayoiamini;Kuimarisha utumishi wa umma unaozingatia weledi, nidhamu, uadilifu, bidii na maarifa katika kazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom