Mafanikio ya miaka mitano ya CCM, wateule wa Rais Magufuli hawatatui kero za Wananchi. Hapa tatizo lipo wapi?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
4,213
2,000
Mimi Idugunde huwa sipendi unafiki hata kidogo. Ni kweli CCM imefanya makubwa kipindi hili cha awamu ya kwanza ya uongozi wa JPM.

Lakini kuna kasoro moja kubwa sana imejitokeza kwenye utawala wa huu. Maana kila anapofanya ziara zake Rais Magufuli huwa anakutana na watu ambao wana kero ambazo zingeweza kutatuliwa na wateule wake. Jambo la kujiuliza hao wateule wake hawajui majukumu yao?

Jambo lingine ambalo watu wanajiuliza je Rais Magufuli alikuwa anateua watu ambaoa hawajui majukumu yao? Maana kama mkuu wa nchi ni aibu kuwa unateua mtu ambae anapewa ukuu wa wilaya au ukuu wa mkoa huku hawezi kutekeleza majukumu yake.

Ni aibu kubwa sana rais yupo kwenye kampeni alafu unaona wakina mama wanamlilia mpaka wanazimia kama ilivyotokea kule Musoma. Pia ni aibu kubwa kuona rais akikataa kusikiliza kero ya mwananchi wake kama ilivyotokea pale Nyashimo Nassa. Lakini aibu hii yote ni sababu wengi wa wateule wa rais hawajui majukumu yao na kazi zao.Maana kama mkuu wa mkoa huwezi kutatua kero za wananchi inakuwa mkuu wa nchi amteue mtu kama huyu.

Rais Magufuli pamoja kuwa upo kwenye kampeni,tambua kuwa wateule wako hawana uwezo wa kuwatumikia wananchi. Hivyo usikatae kusikiliza kero za wananchi kwa kisingizio cha kampeni wakati wewe bado ni rais wa JMT.
Idugunde, msema kweli.
 
Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
12,925
2,000
Kwa sababu kila kitu Magufuli wao anataka kuonekana ametatua yeye, hivyo wanaacha mambo kama yalivyo ili mpenda sifa aje kuyatatua.
 
Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,614
2,000
Kwa sababu kila kitu Magufuli wao anataka kuonekana ametatua yeye, hivyo wanaacha mambo kama yalivyo ili mpenda sifa aje kuyatatua.

Uko sahihi bro.
Tatizo siyo wateule wa Jiwe baali ni yeye mwenyewe......Huyu Magufuli anataka KAZI ZOTE AFANYE YEYE: Kama hujajua Magufuli ndio Mihimili yote: Bunge, Mahakama na Serikali.
Kazi zote za Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Wakuu Mikoa&Wilaya ni yeye......Yeye ndiye anapanga Bajeti na kutoa kibali Nani alipwe na asilipwe toka Hazina.......Dikteta Uchwara Waheed!
 
Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
4,793
2,000
Mimi Idugunde huwa sipendi unafiki hata kidogo. Ni kweli CCM imefanya makubwa kipindi hili cha awamu ya kwanza ya uongozi wa JPM.

Lakini kuna kasoro moja kubwa sana imejitokeza kwenye utawala wa huu. Maana kila anapofanya ziara zake Rais Magufuli huwa anakutana na watu ambao wana kero ambazo zingeweza kutatuliwa na wateule wake. Jambo la kujiuliza hao wateule wake hawajui majukumu yao?

Jambo lingine ambalo watu wanajiuliza je Rais Magufuli alikuwa anateua watu ambaoa hawajui majukumu yao? Maana kama mkuu wa nchi ni aibu kuwa unateua mtu ambae anapewa ukuu wa wilaya au ukuu wa mkoa huku hawezi kutekeleza majukumu yake.

Ni aibu kubwa sana rais yupo kwenye kampeni alafu unaona wakina mama wanamlilia mpaka wanazimia kama ilivyotokea kule Musoma. Pia ni aibu kubwa kuona rais akikataa kusikiliza kero ya mwananchi wake kama ilivyotokea pale Nyashimo Nassa. Lakini aibu hii yote ni sababu wengi wa wateule wa rais hawajui majukumu yao na kazi zao.Maana kama mkuu wa mkoa huwezi kutatua kero za wananchi inakuwa mkuu wa nchi amteue mtu kama huyu.

Rais Magufuli pamoja kuwa upo kwenye kampeni,tambua kuwa wateule wako hawana uwezo wa kuwatumikia wananchi. Hivyo usikatae kusikiliza kero za wananchi kwa kisingizio cha kampeni wakati wewe bado ni rais wa JMT.
Idugunde, msema kweli.
Tatizo hawafanyi wao wapo kama maroboti na hakuna murndelezo. Kuna mpuuzi mmoja kule temeke ati unasema limewajaza watu pale zakhem ili kutafuta kero zao sasa unajiuliza TEMEKE KULIKUWA NA MKUU WA WILAYA. GONDWE ANATAKA KUAMINISHA WATU KWAMBA MTANGULIZI WAKE HAJAFANYA LOLOTE
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom