Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Matokeo ya Uchaguzi wa Marudio yakiendelea yanaonyesha CCM ikipata ushindi mwingine wa kishindo kama Chaguzi nyingine zilizopita na hivyo kuongeza shinikizo legitimacy crisis kwa Upinzani nchini. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani hadi sasa, kumeshafanyika Chaguzi za Marudio zifuatazo na matokeo yake:
- Mwezi Januari 2017: CCM - majimbo 01 na kata 19; CHADEMA - 01
- Mwezi Novemb 2017: CCM - kata 42 na CHADEMA - kata 01.
- Mwezi Januari 2018: CCM - majimbo 03 na CHADEMA - kata 00.
- Mwezi Februari 2018: CCM - majimbo 02 na kata 08; CHADEMA - kata 00.
- Mwezi Agosti 2018: CCM - majimbo 01 na kata 79; CHADEMA - kata 00.
- Mwezi Septemba 2018: CCM - majimbo 02, kata 23; CHADEMA - kata 00.
Katika jumla ya Kata 174, CCM imezoa kata zote isipokuwa mbili pekee.
Upinzani wamekuwa wakilalamika kuwa, Serikali inatumia vyombo vya dola, pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuvikandamiza Vyama vya Upinzani. Yes, katika akili za kiubinadamu, unaweza ukajikuta ukasahau kiini (core) cha tatizo na kushughulika na sporadic effects za hilo tatizo.
Swali la kujiuliza: Hivi barani Afrika, Tanzania ndiko kwenye Tume ya Uchaguzi pekee? Tanzania ndiko kwenye Vyombo vya Dola pekee? Kama viko kila Nchi kwa nini kuna malalamiko yasiyoisha juu ya uonevu? Kwani Wapinzani katika Nchi nyingine za kiafrika walifanyaje? Mbona hapa Afrika Mashariki, Tanzania imeongoza kidemokrasia mwaka 2017 tena kipindi hivi cha Magufuli wanayemuita dikteta?
Tanzania Tops Region in Democracy Index
Uzoefu barani Afrika unaonyesha wazi kuwa, hakuna serikali iliyokuwa ikilaumiwa kwa udikteta, ilipoondolewa madarakani, basi mambo yalibadilika kuwa ya kidemokrasia.
Mambo haya yalianzia kwa:
- Ghana: Kwame Nkrumah - 1966. Walifurahi kupinduliwa kwake lakini waliompindua nao walipinduliwa mwaka 1972.
- Uganda: Milton Obote - 1972. Waganda awali walimfurahia Idd Amin, baadaye je?
- Uganda: Obote & Tito Okello - 1986. Walimfurahia Yoweri Museveni, leo je?
- Zambia: Kenneth Kaunda - 1993. Walimfurahia sana Frederick Chiluba, baadaye je?
- Zaire: Mobutu Sesse Sekou - 1996. Walimfurahia Laurent Kabila, baadaye, je?
- Congo: Denis Sassou Nguesso - 1993. Walifurahia Pascal Lisouba na baadaye tena huyo huyo Nguesso.
- Ivory Coast: Robert Guei & Laurent Gbagbo 2002 - 2010. Alikuja Alassane Ouattara but what next?
- Rwanda: Juvenile Habyarimana. Walimfurahia Paul Kagame, what next?
- Burundi: Pierre Buyoya - 1998. Walimfurahia Pierre Nkurunzinza, leo je?
- Tunisia: Zine Ben Ali - 2011. Walifurahia mno but mpaka leo hali haija-settle tena.
- Misri: Hosni Mubarak - 2011. Walifurahia sana kupinduliwa kwake, wakoje sasa?
- Libya: Muamar Gaddafi - 2011. What next? Leo hii kupinduliwa kwa huyu jamaa has become among the grave mistakes politics have ever made in our modern times. Angalia jinsi wahamiaji wanavyowa-haunt wazungu huko Ulaya.
- Misri: Mohammed Morsi - 2013. Walimfurahia sana Abdul Fattal el Sisi, leo je?
- Sudan/South Sudan: Al Bashir - 2010. Walimfurahia sana John Garang, leo wakoje?
Tunaweza kuchambua vyema na mifano mingi zaidi iliyopo hapa barani Afrika.
Kamwe hakuna guarantee kuwa, kwa aina ya maendeleo ya sasa ya Tanzania, Chama kingine kikiingia madarakani kutakuwepo na demokrasia tunayoifikiria na tuliyosoma vyuoni - never.
Demokrasia namba moja ya Tanzania ni maendeleo ya kiuchumi. Bahati mbaya maendeleo ya kiuchumi ni suala la usimamizi zaidi kuliko suala la makubaliano. Demokrasia haiwezi kuleta maendeleo ya kiuchumi bali maendeleo ya kiuchumi ndiyo yanaleta demokrasia.
Refer to Maslow's Hierarchy of Needs.
Muwajue wananchi wenu wanachotaka. Hawaoni issue nyie hata mkiibiwa kura coz halijawahi kuwa tatizo lao kuu. Tatizo lao kuu ni ajira, afya, maji, barabara nzuri, elimu na the sort. Tujifungue macho, hamuwezi kufikiria - mmeshiriki chaguzi ndogo sita tangu Rais Magufuli aingie madarakani, huku mkilalamika kuonewa kila leo, kwa nini wananchi hawawasiklizi?
Ushauri wangu, shirikianeni bega kwa bega Serikali, one day wananchi watachambua mchele na pumba. "An Organisation normally reflects the Society's behavior."