Mafanikio ya awamu ya Serikali ya awamu tano sekta ya afya. Huduma ya upasuaji bila malipo yanufaishaa zaidi ya wananchi 1000 Kanda ya Ziwa

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Zaidi ya wakazi 1000 wa Kanda ya Ziwa wamenufaika na matibabu ya bila malipo hasa kwa upande wa upasuaji unaofanywa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania. Hayo yamebainishwa na Rais wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania, Dkt. Catherine Mung’ong’o wakati wa siku ya kuhitimisha zoezi la upasuaji lililofanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 03 hadi 07 Juni 2019 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Amesema kuwa lengo la upasuaji huo ni kupunguza idadi ya wahitaji wa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu toka Kanda ya Ziwa, nakuongeza kuwa zoezi hilo limefanyika kwa ushirikiano baina ya Chama hicho, Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bungando na Madaktari wengine.
Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa huduma hii ya upasuaji inayotolewa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania imekuwa ikifanyika kila mwaka katika mikoa mingine huku ni ikiwa ni mara ya kwanza katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Kwa upande wake Kiongozi wa Chama hicho Kanda ya Ziwa ambaye ni Daktari Bingwa wa Upasuaji toka Hospitali
Zaidi ya wakazi 1000 wa Kanda ya Ziwa wamenufaika na matibabu ya bila malipo hasa kwa upande wa upasuaji unaofanywa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania. Hayo yamebainishwa na Rais wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania, Dkt. Catherine Mung’ong’o wakati wa siku ya kuhitimisha zoezi la upasuaji lililofanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 03 hadi 07 Juni 2019 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Amesema kuwa lengo la upasuaji huo ni kupunguza idadi ya wahitaji wa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu toka Kanda ya Ziwa, nakuongeza kuwa zoezi hilo limefanyika kwa ushirikiano baina ya Chama hicho, Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bungando na Madaktari wengine.
Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa huduma hii ya upasuaji inayotolewa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania imekuwa ikifanyika kila mwaka katika mikoa mingine huku ni ikiwa ni mara ya kwanza katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Kwa upande wake Kiongozi wa Chama hicho Kanda ya Ziwa ambaye ni Daktari Bingwa wa Upasuaji toka Hospitali ya Rufaa Bugando, Dkt. Olivia Kimario amesema kuwa zoezi hilo ni utaratibu uliowekwa na Chama cha Madaktari hao ambapo mwaka huu wamehudumia katika mikoa ya Mwanza , Shinyanga , Mara na Geita.
Katika hatua nyingine Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hilo la upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu Chama hicho kitatoa huduma bure za upasuaji kwa wagonjwa wenye matatizo ya Mdomo Sungura litakalofanyika tarehe 10 na 11 Juni 2019 bila ya malipo.
ya Rufaa Bugando, Dkt. Olivia Kimario amesema kuwa zoezi hilo ni utaratibu uliowekwa na Chama cha Madaktari hao ambapo mwaka huu wamehudumia katika mikoa ya Mwanza , Shinyanga , Mara na Geita.
Katika hatua nyingine Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hilo la upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu Chama hicho kitatoa huduma bure za upasuaji kwa wagonjwa wenye matatizo ya Mdomo Sungura litakalofanyika tarehe 10 na 11 Juni 2019 bila ya malipo.

1126454
 
Back
Top Bottom