Mafanikio ya ATCL: Safari za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Guangzhou China zaanza

Tiket zitapatikana Online! Air tanzaniae ticketing kama mashirika mengine duniani basi.
 
Nacheka kuona waliokuwa wanaponda ndege sio kipaumbele, leo wanasema iyo root itawasaidia sana wafanyabiashara.

Nimegundua watanzania wengi hatujui tunachokitaka ila tunayo mengi tunayoyatamani na hatuna mipango kabisaaa ya kuyapata ayo matamanio yetu.

Najaribu kuwaza sana kuwa ikitokea Kiongozi aamue kufanya mambo fulani kwa kutusikiliza 100% ataondoka madarakani hajafanya lolote,
 
Hakuna kitu kinaboa kama kukaa kwenye ndege bora gari unachungulia nje ukisalimia miti
... halafu ikianza ku-suffer turbulence ndio balaa kabisa hakuna utulivu! Na kaeneo hako kuanzia India/Sri Lanka eastwards kana turbulence za kufa mtu hasa msimu wa Monsoon!
 
PICHA : Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) leo alfajiri limezindua rasmi safari za moja kwa moja Kutoka Dar es salaam hadi Guangzhou, China baada ya kuahirishwa mara kadhaa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo janga la Corona.

Uzinduzi huo umeongozwa na Mhandisi. Dkt. Leonard Madaraka Chamuriho, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi.

Hizi ni picha kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3, Raia wa China wakiwa kwenye maandalizi tayari kuanza safari.

C1.jpg
C2.jpg
 
Kila la kheri kwa Ndege tunayoiendesha kwa fedha zetu za Kodi

Tunaiombea Safari njema lakini Ndege yetu hiyo ya Maonyesho ni vizuri tutafute Kampuni ya Kigeni yenye uzoefu tuwakodishie

Sisi kama Nchi ambayo Watoto wetu wanasoma huku wamekaa sakafuni tulikosea sana na hatukujua vipaumbele vyetu

Tulikurupuka sana ndio Maana Wazungu na Waarabu huwa wanatushangaa na kusema Mwafrika hajui anataka nini
 
Back
Top Bottom