Mafanikio tuliyopata watanzania baada ya miaka 50 ya uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafanikio tuliyopata watanzania baada ya miaka 50 ya uhuru

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by kamanzi, May 19, 2011.

 1. k

  kamanzi Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Leo sina muda wa kutosha ila nataka kuweka wazi mafanikio ya Tanzania tangu tupate uhuru. Yafuatayo ni mafanikio halisi na sababu za kujivunia uhuru wetu wa miaka 50:

  i) Pamoja na kuwa na mito na maziwa mengi nchini, bado watanzania TUMEFANIKIWA kuishi kwa maji ya mgao.

  ii) Pamoja na kuwa na gesi ya songosongo, mito na makaa ya mawe mengi, bado watanzania TUMEFANIKIWA kuishi kwa umeme wa mgao.

  iii) Pamoja na kuwa na madini pekee ya tanzanite, watanzania TUMEFANIKIWA kuzidiwa na wakenya kwenye mauzo ya madini hayo.

  iv) Pamoja na kuachiwa msingi wa wa umoja na amani baada ya miaka 24 ya uongozi wa Nyerere, watanzania TUMEFANIKIWA kuingia katika mizozo ya kidini na ukabila kwa sasa.

  v) Pamoja na kuwa na rasilimali za kutosha katika kila nyanja, watanzania TUMEFANIKIWA kubaki kama nchi ya mwisho toka chini kwa umaskini duniani na baadhi ya nchi zinazotuzidi kiuchumi ni pamoja na Somalia nchi isiyo hata na serikali.

  vi) Pamoja na kujua kwamba CCM ni wapuuzi na majambazi, watanzania TUMEFANIKIWA kuendelea kuwaweka madarakani mwaka hadi mwaka.

  vii) Pamoja na kuwa na madaktari na nyaraka zinazoonyesha wazi kuwa ukimwi hauna tiba, watanzania TUMEFANIKIWA kumtengeneza babu wa Loliondo na kuamni kuwa dawa yakle ni muarobaini tosha

  Ningeendelea zaidi ila kwa kukosa muda, naomba kuwatakia watanzania wenzangu HONGERA YA MAFANIKIO yatokanayo na miaka 50 ya Chama Cha Majuha.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kuna mafanakio ya kuuza ardhi kwa wahindi na maponjoro wengine ilhali sisi wenyewe tunauziana plot kwa milioni 9, Watu wanaishi kwene makazi holela na kuvamia maeneo. kana kwamba nchi ina uhaba wa ardhi. Na suala la upangaji miji mpaka leo ni ndoto. Sasa sijui ni maendeleo ganmi huletwa kwene makzi yasiopimwa.

  Kuna wakti mi nadhani ni bora tumrejeshe mkoloni. Pamoja na kwamba watakuwa wanatunyonya lakini wapo systematic. Huduma basic haziwezi kukosekana. Enough with chama cha nguruwe wasio na haya.
   
Loading...