Mafanikio tulionayo yanachangiwa na kazi nzuri za madiwani na wabunge wa ccm" Dkt Bashiru

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Messages
856
Points
1,000

Egnecious

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2015
856 1,000
DKT. BASHIRU: MAFANIKIO TULIONAYO YANACHANGIWA NA KAZI NZURI ZA MADIWANI NA WABUNGE WA CCM

15 Oktoba, 2019

Dkt. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM akitokea Mkoa wa Lindi kurudi Dar es salaam amepitia Ofisi ya CCM wilaya ya Mkurunga Mkoani Pwani na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa na sekretarieti ya wilaya hiyo.

Katika kikao hiko, Katibu Mkuu ameipongeza kamati ya siasa kwa ujenzi wa ofisi mpya ya wilaya unaoendelea na ubunifu mkubwa wa vitega uchumi vinavyozunguka ofisi hiyo.

Katibu Mkuu akizungumza na wajumbe hao, amewataka wanachama na wananchi wote kuelewa kuwa, mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana katika serikali ya CCM ya awamu hii ya tano yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na Madiwani na Wabunge wa CCM.

"Hatuwezi kutaja na kufurahia mafanikio tulionayo sasa katika awamu hii ya tano bila kuwasifu madiwani na wabunge wote wa CCM ambao wamekuwa chachu kubwa ya kufanikisha utekelezaji huo kuanzia bungeni mpaka kwenye mabaraza ya madiwani, hivyo ni lazima tukawapa utulivu wa kutenda zaidi majukumu hayo." Dkt. Bashiru amesisitiza

Pia katika kikao hiko, Katibu Mkuu amezitaka kamati za siasa za mikoa na wilaya kuendelea kuwaeleza wanachama na mashabiki wa CCM umuhimu wa kujitolea hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.

"Waambieni wanaCCM wote na mashabiki wa CCM, kipind hiki cha uchaguzi ni kipindi cha mapambano, sio kipindi cha kudai fedha za posho, tukianza kulipana posho kipindi hiki tutashindwa mapema." Dkt. Bashiru ameongeza.

Aidha, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kumkabidhi gazeti la UHURU YA KIJANI toleo maalum la kila mwezi Mwenyekiti wa CCM wa wilaya kwa niaba ya Viongozi na wanachama wote wa Mkuranga na kuwashauri walinunue kwa wingi ili kupata maarifa zaidi ya itikadi, sera na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ziara hii, ni muendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwa viongozi kuendelea kuwa karibu na wanachama na wananchi kwa ujumla.

Imetolewa na;
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
MAKAO MAKUU DODOMA
IMG-20191015-WA0032.jpeg
IMG-20191015-WA0033.jpeg
 

Forum statistics

Threads 1,381,210
Members 526,018
Posts 33,792,612
Top