Mafanikio niliyoyapata toka nijiunge JamiiForums mwaka 2012

mbota

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
833
500
Heri ya mwaka mpya wadau wote wa JamiiForums.

Hakika leo nimekaa na kutafakari toka nimejiunga Jamiiforums je kuna mabadiliko yoyote kwenye maisha yangu kiujumla yani Kiuchumi, Kiroho, Kijamii na Kimwili.

Jibu nikuwa kuna mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yangu hivyo nasema ASANTE kwako wewe mdau na uongozi mzima wa Jamiiforums.

Mafanikio niliyopata kwa ufupi kutokana na mada za humu nimeweza kuwa Mfugaji wa kuku wa mayai ambapo sasa imekuwa sehemu ya kipato changu, pia nilipata ushauri wa rangi ya suti (designs) niliyofungia ndoa mwaka 2017.

Pia nimeweza kuwa na ufanisi hasa kwenye swala la teknologia ya computer mfano Microsoft excel nakumbuka kuna mdau alianzisha group la Telegram ambapo alikuwa anafundisha free kule. Pia nilishanunua vitu kama redio, TV nk kutokana na Jamiiforums.

Pia kuna baadhi ya mambo ya afya ambayo sikuyajua kabla ya JamiiForums mfano ni hii homa ya ini ambapo nimedhamiria mwaka huu lazima nipate vipimo pamoja na familia kwa ujumla.

Kuna mengi sana nimejifunza na naendelea kujifunza kila siku hivyo mdau jua unapo share jambo huku kwa namna moja au nyingine unamtoa mtu mmoja sehemu fulani hivyo tuendelee kushirikiana mwaka huu 2020, uwe mwaka bora kwetu.

NB: Hata wewe unaweza kutushirikisha mafanikio unayopata kutoka hapa JamiiForums.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mbota

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
833
500
Maserati ulinisaidia sana Mkuu
20200104_170943.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom