Mafanikio kwa kwenda kwa mganga wa kienyeji

Jeff

JF-Expert Member
Sep 26, 2009
1,293
199
Hivi kuna uwezekano kweli wa kupata mafanikio kupitia nguvu za giza kama vile kupata kazi,mke unayemtaka au mafanikio mengine ya maisha kwa kwenda kwa wataalam wa kienyeji? kweli mtu anaweza kufanikiwa kupata kazi anayoihitaji kulingana na elimu yake kwa kwenda kwa mganga wa kienyeji?
nipeni uzoefu wenu na maisha haya
 
Nashauri kwamba research hii ianzie kwako halafu urudi JF uje utupe data, kwa sasa mimi sifahamu chochote.
 
.....Wapo watu wanafanikiwa na kuwa matajiri, lakini kamwe hawawezi kuishi kwa raha na utajiri huu wa kishirikina, juju zina masharti mengi.
.......Tafuta elimu/ujuzi wako mzuri upate kazi nzuri na kuwa tajiri au na uwezo mzuri wa jasho lako mwenyewe., hapo utafurahia maisha vizuri.
 
Mafanikio yanayopatikana kwa kutumia nguvu za giza au kwenda kwa waganga wa kienyeji siyo mafanikio yatakayokupa raha ya nafsi, mwili na roho.

Wakati wote ni kuwa kinachofanyika; unapata mafanikio yasiyo rasmi (artificial benefits on the expense of long term suffering).

Nikushauri tu kuwa mtegemee Mungu aliyekuumba na amekuwezesha kuwa na uzima mpaka sasa. Kamwe usitegemee akili zako au kumtegemea mwanadamu kwa lolote. Tumaini lako liwe katika Mungu aliyeziumba mbingu na nchi na umuombe yeye.
 
Mafanikio yanayopatikana kwa kutumia nguvu za giza au kwenda kwa waganga wa kienyeji siyo mafanikio yatakayokupa raha ya nafsi, mwili na roho.

Wakati wote ni kuwa kinachofanyika; unapata mafanikio yasiyo rasmi (artificial benefits on the expense of long term suffering).

Nikushauri tu kuwa mtegemee Mungu aliyekuumba na amekuwezesha kuwa na uzima mpaka sasa. Kamwe usitegemee akili zako au kumtegemea mwanadamu kwa lolote. Tumaini lako liwe katika Mungu aliyeziumba mbingu na nchi na umuombe yeye.

ok,future bishop nashukuru kwa mawazo yako yenye kutia nguvu thanks
 
Hivi kuna uwezekano kweli wa kupata mafanikio kupitia nguvu za giza kama vile kupata kazi,mke unayemtaka au mafanikio mengine ya maisha kwa kwenda kwa wataalam wa kienyeji? kweli mtu anaweza kufanikiwa kupata kazi anayoihitaji kulingana na elimu yake kwa kwenda kwa mganga wa kienyeji?
nipeni uzoefu wenu na maisha haya

Ni bora hayo maisha uyakose kuliko kuyapata. Ndugu yangu unatafuta balaa kubwa kumiliki mali za kishetani, gharama yake ni kubwa na mbaya kuliko unavyofiki.
 
Mafanikio?? Neno mafanikio lina mapana makubwa sasa ni katika mtizamo gani unatizama. Kwani masikini huoa kama tajiri, mcha Mungu nae kimwili hufa kama kafiri, wafalme katili huzeeka nao hufa kama ilivyo kwa manabii, kwenye nyumba za wanadamu iwe ni matajiri ama masikini, watwana ama watumwa, wachaMungu ama makafiri, weupe ama weusi yanapatikana majamvi ya misiba kwa zamu kama ilivyo ada. Na kile kinachoitwa mafanikio ktk wanadamu ukiweza kukitizama kwa jicho la tai ni matokeo ya ukatili dhidi ya utu maana ili mmoja aweze kuwa tajiri wa vitu ni lazima pia wengi wa wanaomzunguka wawe masikini wa hivyo vitu. Utajiri wa namna hii unatafutwa hata kwa kulitumia jina la Mungu juu ya zile zinazodhaniwa kuwa madhabahu takatifu na kwa watu wanaodhaniwa watakatifu. Nasema hii ndio ramli haswa kwa mtu kumdanganyia Mungu huku akiwa na nia yeke binafsi mfukoni ya kujitajirisha kupitia hao watu. KWA MTIZAMO WANGU KUFANIKIWA NDIO HUKU, 'KUMCHA MUNGU IKIWA YA KWAMBA UNA KITU AMA IKIWA HUNA KITU!!!'
 
kumcha bwana ni mwanzo wa maarifa;Usiulize jibu kama zinaitwa nguvu za gizai
inamaana hata matokeo yake ni ya kigizagiza .
 
Kwenda kwa mganga wa kienyeji ni kitu kimoja, kutumia nguvu za giza ni kitu kingine.Naomba utamaduni wa imani zetu za kiasili kabla ya ujio wa Ukristu, tusiute nguvu za giza, ni sehemu ya mila na tamaduni zetu, zikitumiwa kwa nia njema, huitwa tiba asilia/mganga wa kienyeji, na zikitumiwa kwa nia mbaya, ni uchawi, ulozi na wapiga ramli........................................................................................................................................................................................................................................Dola ya Axim ilikuwa na mafanikio makubwa sana kabla ya ujio wa wazungu. Mkama Rumanyika wa Karagwe alikuwa na uwezo wa kuita mvua, kupiga radi nk. Kinjekitile aligeuza risasi maji kwenye vita vya majimaji. Mkwawa shujaa ilikuwa ukimkaribia, anavanish into thin air, hata lile fuvu linalodaiwa ni la Mkwawa, sio, alimvisha mavazi yake, mmoja wa walinzi wake, akamshoot ili kuwapoteza maboya Wajurumani na waliingia line, mwenyewe alivanish tuu.........................................................................................................................................................................................................................................Kuna mambo ya mila na mizimu ambayo kidini yote ni nguvu za giza, watu wanafanikiwa sana kwa kudumisha mila zao, ndio maana wachagga mpaka kesho, Desemba ni Kuhiji mgombani, huko wanatishwa mbege, wanamwaga makaburini, wanakunywa mpaka damu kwa jina la kisusio!. Wanafanikiwa mambo yao supper.Wapo pia wanaomtegemea Mungu huyu huyu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, ni Mungu wa Israel, wengine wengi tunadandia tuu na tunafanikiwa.........................................................................................................Wako wahindu wanaoabudu budhiism, mungu wao ni Budha, masanamu, wako wanaabudu ng'ombe, panya nyoka, na wanafanikiwa. Wachina wengi ni wakomunisti, hawaabudu mungu yoyote, wao ni kuchapa kazi tuu na wanafanikiwa............................................................................................................................................................................................................................Wako matajiri wa kiarabu/kipemba, wanatumia nguvu za majini, maduka yao yanajazwa bidhaa, majini yawatia wateja kwea wingi, biasharas zinashamiri, wanafanikiwa.............................................................................................................................................................................................................................Hoyo yote ni tisa tuu, kumi mafanikio ya kweli ni kuamini kwa dhati kile unachoamini, na utafanikiwa tuu, just belive in yourself, uwezo wa mafanikio uko within yoursef ni wewe kuamua tuu kwa that na ikiwezekana sema kwa sautui " I KNOW I CAN, BE WHAT I WANNA BE'
 
Kaka naona una hamu na mashetani na majini yapo mengine yanataka kuzaa na wewe kisha kuwa tajiri au kupata mafanikio ila na wewe unakuwa ni nusu shetani! Acha kabisa mambo ya waganga wa kienyeji kwa nini wao wakufanye wewe ufanikiwe wakati wao wapo kwenye hali duni? Wanatafuta roho yako waingamize sababu ya tamaa zako za maendeleo/utajiri wa chapchap Achaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom