Maeneo yeye dhahabu Tanzania na hali ilivyo kwenye maeneo hayo

Wandugu hebu tufanye kucatalog maeneo yote inakopatikana na kuchimbwa dhahabu Tanzania. Nasikia kuwa sehemu nyingi zenye udongo mweusi(iron) na mwekundu (iron oxide) huwa ni rahisi kupatikana madini ya dhahabu. Sasa Tz kuna maeneo mengi sana yana dhahabu, tujuzane maeneo hayo na hali ya uchumbaji inavyoendelea

1. Geita. Huku nafikiri ndiyo kunaongoza kwa maswala ya uchimbaji wa dhahabu Tanzania.

2.Chunya, Mbeya. Huku wanaita Lupa gold belt/field. Huku kuna eneo kubwa sana lenye dhahabu na uchumbaji wake siyo mkubwa kama Geita.

3. Mara.

4. Tanga, Handeni huku wamegundua miaka si mingi.

5. Mpanda, Katavi

6. Iringa, huku waligundua miaka ya karibuni na sijui kama bado wanachimba.

7................
Iringa sehemu gani mkuu?
 
Kuna Economic geologist hapa? au geologist yeyote.

Nataka kufahamu mawili matatu.
 
Watu wa dar na dhahabu wapi na wapi jamani😄😄 ila wachache tu wanaoijua na kuishika, wengine wanaambulia kuiona kwenye runinga na mapicha 😄



🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
 
Hata Wazungu walichuma Africa wakajenga na kuiendeleza Ulaya kwahiyo hapo hakuna cha kushangaza sana Mkuu

(Kama nimeelewa uzi wako lakini)
 
Watu wa dar na dhahabu wapi na wapi jamani😄😄 ila wachache tu wanaoijua na kuishika, wengine wanaambulia kuiona kwenye runinga na mapicha 😄



🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
Kama ambavyo zinasambaa taarifa zilizochambuliwa kuhus kulima matikiti na mapapai, ingependeza na taarifa kuhusu uchimbaji wa dhahabu zingesambaa hivyo. Watu wenye mitaji wanaojishughulisha na dhahabu wana mkwanja mrefu sana. Nimekaa sehemu wanachimba kama mwaka nimeona mambo yao.
 
Na sasa bei yake iko juu sana. Kuna raia wanahela mbaya kupitia dhahabu, ule uchimbaji wa kuokoteza na bei kilanguzi havipo tena. Sifa zimuendee mwenda zake(Mnyonge mnyongeni)
Yes..kwenye dhahabu alitutetea sana wachimbaji wadogo .ingawa kulikua na utitiri wa kodi....!ss hv mwenye kisu ndo anavusha mpakani kiulaniiii
 
Kama ambavyo zinasambaa taarifa zilizochambuliwa kuhus kulima matikiti na mapapai, ingependeza na taarifa kuhusu uchimbaji wa dhahabu zingesambaa hivyo. Watu wenye mitaji wanaojishughulisha na dhahabu wana mkwanja mrefu sana. Nimekaa sehemu wanachimba kama mwaka nimeona mambo yao.

Aise.. ..sema serikali yetu haiaminiki, unakatiwa kaeneo, end of the day unaambiwa eneo hili limechukuliwa.. ..wazungu wanapewa kipaumbele kuliko wazawa, wanakatiwa maeneo makubwa na yenye dhahabu, sisi walala hoi tunaachiwa makapi.. ..



🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
 
Hali inaendelea vizuri tu. Nadhani jibu umepata, au unahitaji ujue nini zaidi?
Hayo maeneo yana ufukara wa kutisha,kuanzia Kahama,Kakola,ushirombo,Nyandwiga,Kerezia,Geita,ukifika vijijini utaamini unachokiona,
Mwanza,Geita,Kahama ilibidi iwe miji iliyoendelea kwa Miundombinu,na madhari maana madini yameanza kuchimbwa tangu 80s,
 
Back
Top Bottom