Maeneo yenye baridi kupita yote Bongo land

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
838
1,358
Haya maeneo ni kiboko katika sekta ya kuwa na baridi Kali katika nchi hii
1. Makete
2. Njombe
3. Mbulu
4. Lushoto
5.Ngara
Kama unahisi Kuna pengine sema hapa , Ila haya ni balaa ,kwingine kupo pia,
 
Nimetoka Makete majuzi, tangu nimeenda sijawahi hata kuoga.

Nimerudi home mdomo umeungua nimekuwa mweusi tii.

Ukipewa chai ya moto utagugumia tu ila baadaye unakuja kugundua umeungua.
 
Mbeya, Umalila.
Aisee nimekaa sehemu za baridi ila Mbeya Umalila ni kiboko! Yani hakuna sehemu bongo kama ile. Baridi ilikuwa inasoma -8c
 
Haya maeneo ni kiboko katika sekta ya kuwa na baridi Kali katika nchi hii
1. Makete
2. Njombe
3. Mbulu
4. Lushoto
5.Ngara
Kama unahisi Kuna pengine sema hapa , Ila haya ni balaa ,kwingine kupo pia,
Hukutakiwa kuisahau Iringa kwa ujumla wake, baada tu ya kuwataja hao watoto wake wa muda mrefu Makete na Njombe.

Kitu Mufindi baba!! Wenyewe wanaita "Mfindi" Nako si haba! Ukifika kila mtu amevaa likoti huku akina mama/dada wakitupia raba mguuni!! Ni shida!! Bado msimu wa Nyahenge!!!
 
Back
Top Bottom