Maeneo ya wamachinga lazima yawe na kikomo cha umachinga

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,269
12,565
Kwakuwa serikali haiwezi kuwa na maeneo kwa machinga woote nchini hivyo Maeneo wanayopewa wamachinga ni kwaajili ya wafanyabiashara wadogo wasiokuwa na mitaji mikubwa ya kufanya biashara kubwa.

Sio sawa kwa machinga kufanya biashara yake eneo hilo milele, ni lazima mmachinga apewe muda maalum wa kufanyabiashara eneo hilo kukuza mtaji wake tu na kuhamia sehemu nyingine ambayo ni rasmi ili kupisha wengine wenye mitaji midogo pia watumie eneo hilo kukuza mitaji Yao pia.

Mfano, sio sawa mtu kuhodhi kizimba kwenye jengo la machinga complex kwa miaka 10 hadi 20 au milele. Ina maana huyu mtu biashara yake haikui? Lazima aondoke baada ya miaka 5 hivi ili kupisha wengine nao wakuzie mitaji Yao hapo. Vinginevyo tutakuwa na watu wasiolipa Kodi stahili milele hata kama wana hela nyingi.
 
Wapewe Mashariti ya kufanya biashara kwenye eneo hilo. Lisiwe ni eneo la kutunzia familia, kujenga nyumba Wala kusomesha watoto, bali liwe eneo la kukuza biashara yako ili ahamie mitaani kama wafanyabiashara wengine
 
Kuna mtu alikuwa anauza vitunguu chini pale Msimbazi barabarani kwa miaka 20 sasa, ameoa, amejenga na kununua mifugo mingi kijijini kwao lakini hahami kwenye eneo lile hadi leo. Nadhani hii sio sahihi kwa definition ya machinga.
 
Umewaza jambo muhimu mno maana bila kuwawekea ukomo watafanya biashara miaka yao yote bila kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom