Maeneo ya kuzikia Dar sasa ghali kuliko kiwanja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maeneo ya kuzikia Dar sasa ghali kuliko kiwanja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 18, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  NI ukweli usiopingika kwa waafrika, kwamba kujinunulia jeneza, eneo la kuzikwa au sanda wakati uko hai, ni uchoro.

  Lakini jijini Dar es Salaam, hali ni tofauti, baadhi ya watu wameanza kuyatafuta maeneo ya kuzikwa wakiwa hai na kuyanunua kwa gharama kubwa kuliko hata viwanja vya kujengea nyumba.

  Eneo ambalo sasa linatafutwa kwa udi na vumba na kwa gharama yeyote kwa ajili ya kuzikana ni eneo yaliko makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam ambako baadhi ya watu wameanza kuyanunua kwa ajili ya kuzikiwa kabla ya kufa.


  Eneo hili la kuzikia katika makaburi hayo yaliyoanza kutumika kabla ya uhuru na hasa baada ya vita Kuu ya pili ya dunia ya mwaka 1945, sasa linapatikana kwa kati ya Sh 1,000,000 na Sh3,000,000.

  “Awali makaburi haya yalikuwa yanatumiwa na Jumuiya ya Madola (Common Wealth) ambayo yalianzishwa miaka ya 1940 na mwanzoni walikuwa wakizikwa wazungu peke yao,” anasema mmoja wa wafanyakazi wa makaburi hayo, aliyejitambulisha kwa jina la Nasoro Lehagasi.

  Lehagasi anasema ukitazama baadhi ya maeneo ndani ya makaburi hayo, utaona kuna makaburi yenye muundo unaofanana na ukiangalia majina, utagundua kuwa waliozikwa hapo ni wazungu. Hiyo ni kwa sababu makaburi hayo mwanzoni yalikuwa ni ya jumuiya ya madola.

  Hata hivyo, alisema baada ya uhuru, watanzania walianza kuyatumia kwa kuzikana na yalikuwa yakipendwa sana kwa sababu tayari yamezika watu wengi maarufu.

  “Mara baada ya uhuru, watanzania nao walianza kuyatumia, wakati huo nafasi ilikuwa kubwa na hakuna aliyetegemea kama itakuja kujaa kama uonavyo sasa na kila mtu alipofiwa alikuwa anachagua eneo hili la makaburi kwa sababu mbalimbali ikiwemo umaarufu wa watu waliozikwa humu,” anasema huku akiyaonyesha kwa kidole makaburi hayo ambayo yalikuwa mbele yake.

  Kwa mujibu wa Lehagasi umaarufu wa watu waliozikwa katika makaburi ya Kinondoni, ulisababisha eneo hili liwe lulu, kwani kuanzia miaka ya 1980 watu walianza kununua maeneo katika makaburi hayo na kuyahifadhi kwa ajili ya mazishi yao na ndugu zao.

  “Watu walikuwa wananunua wakati mwingine mpaka nusu ekari kwa ajili ya kuzikana. Walinunua kwa Sh 100,000 hadi Sh1,000,000 kulingana na sehemu yenyewe,” anaeleza Lehagasi.

  Lehagasi anasema kwa sasa mtu ambaye tayari alikwishanunua eneo, anaweza kuliuza kwa zaidi ya Sh3 milioni.

  Juma Maige ambaye Mtunza Makaburi wa Manispaa ya Kinondoni, anasema kwa kipindi chote ambacho amekuwa akilinda eneo hilo la makaburi ameshuhudia mengi ya kustaajabisha kwani pamoja na watu kujinunulia maeneo ya kuzikiwa, lakini pia migogoro ya kugombania maeneo hayo pia hutokea mara kwa mara.

  “Tangu nimeanza kazi hii mwaka 1984 nimeshuhudia mambo mengi. Watu wanakuja kununua na kuhifadhi maeneo yao ili waje kuzikwa baadaye na wenyewe wanasema wanafanya hivyo kwa sababu siku za usoni kutakuwa na ugumu wa kuyapata,” anasema Maige na kuongeza:

  “Wakati mwingine watu huingia katika migogoro kwa sababu ya kutoweka alama katika maeneo ya kuzikia wanayoyamiliki pamoja na uzembe unaofanywa na baadhi ya wachimba makaburi.”

  Hata hivyo, Maige anabainisha kuwa sasa hivi hakuna nafasi katika makaburi hayo ya Kinondoni kwani zilikwishajaa tangu mwaka 1995.

  “Pamoja na kuwa unaona kuna nafasi bado ndani ya eneo hili, lakini zote tayari zina watu ambao walishanunua kitambo. Lakini, kinachofanyika ni kwamba, kama mtu ana ndugu, jamaa au rafiki, hutumia eneo lake kumzika na ndiyo maana unaona kuna sehemu makaburi yana majina yanayofanana yamejipanga katika safu moja,” anasema Maige.

  Anatolea mfano Wahindi wa jamii ya Wabahai ambao mara baada ya Uhuru walimwomba Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere eneo lao maalumu ambalo watalitumia kuzikana na mpaka sasa limehifadhiwa kwa ajili yao tu.

  “Unaona kibao kile pale (kinasomeka: Makaburi ya Wabahai, Baraza la Kiroho la Kijiji la Wabahai Dar es Salaam), pale ndipo wanapozikwa Wabahai na bado kuna nafasi, lakini imehifadhiwa kwa ajili yao,” anasema Maige.

  Anafafanua zaidi na kusema, watu wengi wanadhani kujihifadhia eneo la kuzikwa ni kujitengenezea mikosi, lakini, sivyo ilivyo. Mtindo huu upo tangu zamani wakati wa Farao huko Misri.
  Wale wanaojua Biblia wanatambua hilo. Sio kitu cha ajabu na inapendeza ndugu wakizikwa katika eneo moja ili hata ukitaka kufanya usafi au kumbukumbu yoyote inakuwa rahisi kwako.

  Mwanamume mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, anakiri na kusema kuwa, yeye ni mmoja kati ya watu walionunua na kuhifadhi maeneo ya kuzikiwa katika makaburi ya Kinondoni.

  “Nilinunua eneo 1992, nia ya kufanya hivyo ilikuwa ni kutaka kuzikwa sehemu ambayo ndugu zangu wapo wengi, lakini pia, hii inasaidia kuepusha gharama za usafirishaji. Ndugu wote mkizikwa hapa hakuna haja ya kusafirisha mwili wa marehemu,” anasema.

  Anaongeza na kusema kuwa anawafahamu watu wengi walionunua na kuhifadhi maeneo ya kuzikiwa kwa siri, lakini tabia hiyo ipo na inaendelea hadi sasa ambapo maeneo mapya ya makaburi yameanzishwa huko Tegeta.

  Lakini Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda ameliambia Mwananchi Jumapili kuwa taarifa za kuuzwa na kuhifadhiwa kwa maeneo ya kuzikana katika makaburi ya Kinondoni, hazina ukweli kwani sheria za ardhi haziruhusu mtu kumilikishwa eneo la umma hasa la makaburi.

  “Nimewahi kusikia tetesi kama hizo, lakini nilipofuatilia niligundua kuwa hazina ukweli kwa sababu lile ni eneo la makaburi ambalo ni la kila mtanzania,” anasema.

  Meya huyo anasema, inaruhusiwa mtu kuchangia kwa kuwapa chochote wale waangalizi wa makaburi kwa ajili ya ulinzi, jambo ambalo ni la kawaida, lakini sio kununua eneo na kulimiliki moja kwa moja kwa ajili ya mtu kuzikiwa ama ndugu zake.

  Hata hivyo, Mwenda ameeleza kuwa akipata ushahidi kuhusu eneo hilo kununuliwa na watu binafsi, atahakikisha haki inatendeka kwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika.
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sema "Ashahadu AnLaa iLlaha iLa Llah" Na kaburi haliku cost senti tano.
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  neno "Ashahadu AnLaa iLlaha iLa Llah"manaake nini sasa hivi haya maneno huwa ni ya kiarabu au lugha nyingine maana huwa sidhani kama watu wote huwa wanayaelewa huwa nayasikia sana misibani hasa kwenye maazishi na kwenye ku RIP
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Maana yake: "Nashahadia kuwa hapana Mungu apasae kuabudiwa ila Allah".
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mzee umebobea kwenye kiswahiri yaani nimefurahi sana NASHAHADIA!!!kweli nimekubali kiswahili ni kiarabu!
   
 6. N

  Ndevu mbili JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kila mtanzania!! Anayo haki ya kuzikiwa maeneo ya umma.
  Je kuna ukweli kila mtanzania atazikiwa hasa maeneo kama hayo?
  Hata pale kisutu si oni huo ukweli!
  Hata gharama za kuchimbia kaburi gharama ni kubwa kutegemea hizo nyumba za milele.
  Tena pale kinondoni niliwahi kuambiwa ni vigogo tu ndio wanazikwa hapo!
  Sina hakika vile sipo huko .
  Naomba kuyuzwa pia.
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  halafu miaka ya mbele kunakuwaga na mtindo wa kuhamisha makaburi ili kitu fulani kijengwe utasikia hili eneo limekwishanunuliwa mnatakiwa kuhamisha na haya makaburi huwa sipendi sana mtindo huu
   
Loading...