Maeneo manne yanayoashiria matumaini ya ugunduzi wa rasilimali ya Mafuta nchini Tanzania

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
1 (1).jpg

Serikali ya Tanzania ametaja maeneo manne yanayoashiria matumaini ya ugunduzi wa rasilimali ya Mafuta nchini kwa siku za usoni kupitia shughuli za utafiti zinazoendelea.

Maeneo aliyoyataja ni pamoja na ya ukanda wa Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika na Kitalu cha Eyasi Wembere chenye ukubwa wa kilometa za mraba 19. 2.

Kitalu hicho kinapita katika mikoa ya Arusha, Manyara, Simiyu, Shinyanga na Tabora.

Dk Kalemali ametoa kauli hiyo jana Jumatano Oktoba 2, 2019 Jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Mafuta na Gesi.

“Kuanzia eneo la Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, maeneo ya Pwani ya Tanga pamoja na Kitalu cha Eyasi Wembere, tunashukuru timu ya wataalamu ya Uganda inayosaidiana na Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kusaidia ushauri,” amesema Waziri Kalemani.

Akifungua Mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wanaokuja katika sekya ya Mafuta na Gesi.

-MPEKUZI-
 
Vizuri sana. Hivi zile trillion za mapipa ya gesi na mafuta zilizovumbuliwa pale kusini zimefikia wapi
 
KAMA MAFUTA NA GESI VITAKUWEPO KWA WINGI KWENYE ARDH YETU, BASI UTASHUHUDIA WATU WEUPE WAKIJIKARIBISHA KWETU KWA KILA MBINU. OLE WETU TUKATAE!! HAKUNA RANGI TUTAACHA KUONA
 
Kama serikali ingekuwa inawekeza yenyewe katika dili za uchimbaji kwa kushirikisha watalaamu wa ndani. Hii nchi ingekuwa kama dubai
 
Back
Top Bottom