Maeneo hatari dar

Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
128
Wadau JF nimeipata hii kutoka Michuziblogspot tunaweza kushea.

mitaa nyeti jijini dar:

Kijitonyama, Sinza na Mikocheni:
Mitaa ya Sayansi, Makumbusho na Maeneo ya Mikocheni Rose Garden ni hatari sana kwa kina dada na kina kaka ambao huninginiza mabegi ya laptop na mapochi makwapani mwao.

Kuna kundi la vijana linatumia magari kukwapua mabegi na mapochi hayo.
Wanachofanya ni kwamba dereva anapunguza mwendo na kukusogelea kisha abiria aliokuwa nao hukwapua mikoba hiyo na kukimbia.
Simu pia huibiwa kwa mtindo huo.

Mbagala:
Mitaa yote ya Mbagala Charambe, Hadi Kiburugwa hi hatari sana kwa kuwa kuna kundi la vibaka linaloitwa Mbwa Mwitu. Kundi hili hupora fedha, simu na kila ulichonacho hadi viatu. Ukikutana nao wanakushambulia kwa vipisi vya nondo na kukuibia huku wakikuacha huna fahamu.

Giraffe Hotel:
Kwenye maegesho ya hoteli hii ni hatari sana kwa wenye tabia ya kuacha mali za thamani ndani ya magari yao.
Kuna kundi la vijana likishirikiana na walinzi wa hoteli hiyo, huvunja vioo vidogo ya nyuma sehemu ya kiti cha abiria, hung'oa power windows na kuchukua kila wanachoweza.
Hoteli imekuwa ikijibu wanaoibiwa kuwa hapa kwetu Parking is at owners risk.

Posta ya zamani na mpya:
Maeneo haya ni hatari kwa wanaotumia daladala na wale wanaogesha magari sehemu mbalimbali za katikati ya jiji hili. Watumia daladala wa Posta huibiwa pesa na simu zao zilizomo kwenye mikoba na mifukoni wakati wakiwa wanagombania magari mida ambayo usafiri huwa mgumu. Wenye magari huibiwa vitu kama power windows na laptop ikiwa utaacha ndani ya gari. Na wezi wakubwa ni vijana wanaozagaa maeneo ya maegesho.

Bonde la Jangwani, Salenda Bridge na Bonde la Kigogo:
Maeneo haya ni hatari kwani hamna makazi, hivyo vibaka hutumia mwanya huo kufanya uhalifu mchana kweupe, na usiku maeneo haya ni hatari zaidi. Ukipata pancha maeneo ya jangwani nakushauri utembelee ringi hadi eitha Faya au Magomeni Mapipa ambapo pana watu na pana usalama. Vibaka hutokea kwa staili ya kukupa msaada na mwisho wa siku hukuacha ukiwa huna kitu na huku gari yako ikiwa skrepa.

Sea View, Ocean Road na Viwanja vya Golf Gymkhanna Club:
Maeneo haya kuna vibaka hatari sana ambao hushambulia kwa kikundi na kupora mali zote na kukuacha ukiwa majeruhi. Maeneo haya yametulia sana na yanaonekana ni salama sana kwani yako jirani na ikulu, lakini hayana usalama wowote na ni hatari kabisa.
Usipite maeneo hayo kwa miguu mida ya kuanzia saa kumi na mbili na nusu giza likiwa linaingi, maana utakumbwa na dhahama.


Daraja la Mlalakuwa, karibu na makao makuu JKT
Hapa watu wamesema weeeee wamechoka. Yaani watu wanavyoporwa kila siku kijua kikizama inaanza kuaminika kwamba wapiga loba ni askari wa hapo JKT ama wanashirikiana na hao vibaka. Wakazi wanajiuliza iweje sehemu nyeti kama hiyo pawe na vibaka? Wanatokea wapi?



TUTAFIKA kweli?
Afande Kova upooooooooo????
NB: Sehemu ambazo hazijatajwa, ikiwa hata mikoani na visiwani, msaada tutani wadau



 
napenda kuzungumzia self defence kama raia wa kawaida. nikiwa na bastola na nikavamiwa na vibaka wenye mapanga naruhusiwa kuitumia papo kwa papo au inakuwaje hapa, sina uzoefu na matumizi ya silaha wala sheria za kumiliki mabunduki/mabastola etc.
 
Kwani huyu afande kova hajui kama hayo ni maeneo hatari akaongeza ulinzi ?
 
napenda kuzungumzia self defence kama raia wa kawaida. nikiwa na bastola na nikavamiwa na vibaka wenye mapanga naruhusiwa kuitumia papo kwa papo au inakuwaje hapa, sina uzoefu na matumizi ya silaha wala sheria za kumiliki mabunduki/mabastola etc.
Mkuu hiyo ndiyo kazi ya silaha yaani kujilinda, kama ulivyosema mwenyewe selfdefence. Na ni hatari zaidi kukubali kupigwa mapanga wakati una silaha kama hiyo kwani wakifanikiwa kukunyang'anya utakuwa umewapandisha kiwango. Kutoka vibaka na kuwa majambazi. Tumia tu mkuu itadhihirika kwamba ulikuwa unajitetea kwani mapanga yatakuwepo eneo la tukio.
 
Kwani huyu afande kova hajui kama hayo ni maeneo hatari akaongeza ulinzi ?

Usishangae dada siku hizi siasa hadi jeshini. Wakifanikisha tukio moja kama hilo la juzi barabara ya nyerere na kawawa watalitangaza, hadi mtu utashawishika kuamini kwamba kweli jeshi tunalo! Kumbe sanaa tupu.

Malalamiko kama haya yameshatolewa muda mrefu, muulize huyo Kova kuna mikakati gani imeshafanyika kwa ajili ya kudhibiti mambo haya, hakuna majibu itakuwa siasa nyingine.
 
Mzee wa Giraffe hotel sisi wateja tunaojitahidi kunyanyua waafrika wenzetu kwa kuwaletea viworkshop na mikutano kama tabia ndiyo hiyo basi hatutaki lawama tutasogea mbele Belinda, Belinda Annex au hata White Sands.

Tafakari!
 
Back
Top Bottom