Maendeleo yoyote ndani ya taifa siyo ya chama fulani, ni dira ya Taifa zima

sopinta

Member
May 28, 2020
46
125
Tukiwa tunaelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Taifa, vyama vya siasa vinajukumu kubwa la kuelezea utekelezaji wa dira ya taifa, utekelezaji wa diplomasia ya ndani ya nchi na diplomasia ya nje ya nchi ikiwa pamoja na diplomasia ya uchumi, pamoja na demokrasia ya taifa, nchi nyingi duniani zinasimamia dira ya taifa bila kujali sera za chama au Rais wa chama fulani. Inapotokea chama tawala au Rais aliyemadarakani akaingiza mambo yake bila kujali dira ya taifa tayari hilo ni tatizo.

Vyama vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu, hakuna kura za huruma pindi mtakapo ingia katika majukwaa na kutangaza sera binafsi, labda tu kapigwa au kanyanyaswa, zungumzeni maendeleo juu ya dira ya taifa, kwa vyama ambavyo hamjapata ridhaa ya kuongoza mnaweza kuzungumza juu madhaifa katika utekelezaji wa dira ya taifa, kwa mfano kama taifa linatekeleza miradi fulani ya kitaifa, ni vyema kuzungumza juu ya madhaifu katika miradi hiyo tena ni raisi sana.

Kwa mfano, katika ngazi ya familia kama Baba au Mama anakazana na ujenzi wa majumba, kununua magari ya kifahari wakati watoto wanaisha kwa tabu yani wamefunga mikanda mpaka kitundu cha mwisho na viuno vimekua kama vya nyigu, jua hiyo ni pointi kwa ila husituambie habari kutekwa, kupigwa hizo sio hoja, tengeza hoja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom