Maendeleo yatakuja baada ya kusafisha uozo

wabuyaga

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,681
588
Wakubwa tuache unafiki huu wa kipumbavu. Nikiwa nina maana hii:

1. Nani hajui kuwa hii nchi ilifikia mahali ambapo haiwezi kulinganishwa na nchi nyingine yoyote ile hapa DUNIANI kutokana na UOZO MTUPU!

2. Hata angekuja mtu kutoka sijui wapi nikiwa na maana kutoka katika chama chochote cha siasa hataweza kufanya chochote bila kuondoa kwanza UOZO HUU

3. Ukweli unauma ila lazima tukubali kuwa hatua ambazo Mhs Rais alianza nazo ni sahihii kabisa.Kwa yule anayekataa ni MNAFIKI tu.

4. Kwa wale wanaojiita sijui Prof au Dr inabidi waache kufanya taaluma zao zionekane kama zinaweza kununuliwa gurioni. Hapa kila kitu kinaeleweka ni wapi pana dosari au panakwenda sawa. Haitakiwi kuwa na hizo titles ili kujua ni wapi pana kosa pamoja na UOZO.

5. Kwa kifupi Mhs Rais amefanya vizuri katika kutafuta maendeleo sahihi na endelevu ya nchi yetu. Anayekataa akatae kwa sababu zake za KINAFIKI ila ukweli ni HUO. Tunamuombea asonge mbele na tunazidi kumuombea.

6. Kama Mhs Rais anaweza akakosea hiyo isiwe sababu ya kufuta yale mengi mazuri anayofanya. ikumbukwe kuwa (An error is no longer a mistake if it can be corrected). Nikiwa na maana swala la mikutano bado linajadiriwa na hilo halijawa kosa kwani bado kuna correction kabla ya tarehe 1.09.2016

Mwisho, kwa wale wenye vichwa vya ajabu njooni muanze kunitukana. Ila kumbuka kuwa ukweli ni huo. Mhs Rais anafanya vizuri kwani nchi ilikuwa imejaa UOZO kwani jina jingine nashindwa kulitamka. Hakuna kiongozi yeyote anaweza kuiokoa nchi yetu bila kupitia njia alizo anza nazo mhs Rais. Ni ukweli na hata kama UNAUMA

Wenu
Wabuyaga nikielekea Stockholm Sweden.
 
Aliyetengeneza UOZO hawezi kusafisha UOZO vizuri, yaani ccm.
Mkuu nafikiri umenielewa. CCM ilitengeneza uozo sawa. Lakini tuwe wakweli na sio kuchukulia vitu kijuujuu. Huyu bwana naona mbali nakuwa katika mtumbwi ule ule lakini anaonyesha kuwa atafanya kazi. Kumbuka baba wa Taifa aliwahi kusema: Watanzania wanataka mabadiriko na watayapata kupitia CCM, na wasipoyapata watayatafuta nje ya CCM. Kwa hiyo bado kuna uwezekano mkubwa wa Mhs Rais kufanya kweli. Mkuu tukubaliane kuwa UOZO ulifanywa na walio pita na yeye kama waziri asingeweza kufanya chochote kwani UOZO ulishakuwa na fangus.
 
Majizi Chadema ndio yanayompinga Magufuli ili awaachie mwanya wapige hela..

Wapuuzwe
Mkuu hawa jamaa lazima waelezwe UKWELI ili waelewe. Hata mtoto mdogo anajua kuwa Mhs Rais amekutana na UOZO wenye FANGUS. Bila hivyo angekuwa mbali. Na hii kazi si ajabu ikachukua hata miaka miwili. Performance yake kuhusu maendeleo ni baada ya hapo.
 
Nani aliyesema JPM anafanya vibaya 100%, hata JK ana mazuri yake na mabaya yake. Tunachotaka Uhuru wa kutoa maoni/hoja uheshimiwe na Serikali, na hizo hoja au maoni izifanyie kazi au ikiona ni zakipuuzi ipotezee wananchi wa pime. Mfano Wanachuo wa UDOM wananchi walikuwa upande wa JPM na kuwapotezea UKAWA walipojaribu kuwatetea.
 
Mkuu mimi sitafuti huo ukuu wa kata. Kama kusoma nimesoma. Na nimesomea Ujerumani. Kama kufanya kazi nimefanya kazi na makampuni makaubwa yenye heshima hapa ulaya na na USA. Kama unataka references zangu kuna watu wanaweza kukueleza mimi ni nani. inabidi tufike mahali tuache ujinga wa kinafiki. Huyu mhs Rais amefanya vizuri kama ni makosa yanaweza kurekebishwa lkn ukweli ni huo kuwa nchi ILIKUWA IMEOZA. Na nyie mnaopinga eleza ni kitu gani mungeweza kufanya KWANZA kama mungepata URAIS? Ninarudia kama Mhs Rais ameteleza mahali fulani basi isiwe ndo kumhukumu kuwa hafai. Wale walio uacha UOZO mnawatukuza kwa lipi? Kuruhusu maandamano? Je ni wangapi walipigwa na kupoteza maisha yao pale Arusha wakati wa mkutano wa kisiasa? Ukweli ni huo tu. Mhs Rais asilimia kubwa is doing very fine.
Acha kujisifu ujinga, kila mtu huku ana Maisha yake toa hoja acha kutoa biography za kijinga, tuko hapa JF kujuana au kutoa hoja na michango mbalimbali kwa hoja zinazoletwa hapa! Kila mtu akianza kujielezea yeye ni nani hapa patatosha? Kizibau wewe
 
Acha kujisifu ujinga, kila mtu huku ana Maisha yake toa hoja acha kutoa biography za kijinga, tuko hapa JF kujuana au kutoa hoja na michango mbalimbali kwa hoja zinazoletwa hapa! Kila mtu akianza kujielezea yeye ni nani hapa patatosha? Kizibau wewe

Wapi nimejisifu? Nilitaka nikueleze wewe unayefikiri najikomba sijui nipate ukatibu kata! shame on you. Watu wanaongea vitu vya maana wewe uko kwenye UTANI na UNAFIKI. Tufike mahali tuwe wakweli na kukubali hali HALISI. Mhs Rais anafanya vizuri katika mambo yaliyo mengi katika kutafuta mahali pa kuanzia, kwani UOZO ulishakuwa na FANGUS.
 
Huwezi kueleweka coz watu wanataka wakilala, wakiamka wawe kwenye nchi ya asali na maziwa..!!
 
Huwezi kueleweka coz watu wanataka wakilala, wakiamka wawe kwenye nchi ya asali na maziwa..!!

Mkuu basi kama ni hivyo kuna haja ya kulaani kabisa hasa serikali ya awamu ya NNE. How comes mtu anaamka asubuhi na kufunga tai na suti anafanya deal jioni anarudi na 1 mil. Hayo ndiyo wanayataka wapiga domu humu JF! Ninarudia Mhs Rais anafanya vizuri SANA na hao wanao kataa wana ajenda zao ambazo hata Mhs Rais ameisha zijua. Na wajue harudi nyuma. Swala la kuandamana linajadirika na hii isichukuliwe kufunika mazuri anayofanya Rais.
 
Mkuu basi kama ni hivyo kuna haja ya kulaani kabisa hasa serikali ya awamu ya NNE. How comes mtu anaamka asubuhi na kufunga tai na suti anafanya deal jioni anarudi na 1 mil. Hayo ndiyo wanayataka wapiga domu humu JF! Ninarudia Mhs Rais anafanya vizuri SANA na hao wanao kataa wana ajenda zao ambazo hata Mhs Rais ameisha zijua. Na wajue harudi nyuma. Swala la kuandamana linajadirika na hii isichukuliwe kufunika mazuri anayofanya Rais.
Nakubaliana na wewe kiongozi, kuna mahali serikali iliyopita ilikosea sana. Mtu anaamka saubuhi, anapiga dili, jioni anarudi na 1m. Then tutake maendeleo ya kufumba na kufumbua, haiwezekani kabisa.
 
Nakubaliana na wewe kiongozi, kuna mahali serikali iliyopita ilikosea sana. Mtu anaamka saubuhi, anapiga dili, jioni anarudi na 1m. Then tutake maendeleo ya kufumba na kufumbua, haiwezekani kabisa.
TUKO PAMOJA. Labda kwa kuongezea, hata hao wapinzani si kwamba hawafanyi kazi zao vizuri, la hasha! Lakini inabidi kufika mahali kukubali kuwa Mhs Rais ameanza vizuri na kuwa KOSA lake liwe specified na well addressed ili walio wengi waone UKWELI. Lakini siyo kosa moja kuonyesha Mhs Rais hajafanya kazi. Kichekesho MKUU: Labda watu wafanye political scientific simulation ili waweze kujiridhisha kuhusu WAPINZANI wangeanza na kipi kama wangelikuwa MADARAKANI!!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom