onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,346
- 1,303
Kipindi Cha uchaguzi kuanzia serikali za mitaa Hadi uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais kauli mbiu ya CCM ilikuwa Ni kuichagua kuanzia ngazi zote ili maendeleo yapelekwe kwa wananchi. Bahati nzuri walipora ushindi na Sasa nchi nzima Ni CCM kwa zaidi ya 90%.
Cha ajabu Barabara zile zilizokuwa na nafuu bado hazijafanyiwa ukarabati na mbaya zaidi nyingine hazipitiki. Hospitalini upungufu mkubwa wa dawa na madaktari na wauguzi, shule zimekosa miundombinu rafiki na vifaa vya kufundishia achilia mrundikano wa wanafunzi chumba kimoja. Kwingineko kote vilio kila asubuhi na jioni. Ajira bado tabu eti Hadi mtu ujitolee ndipo ufikiriwe. Jamani tuchukue mathalani mtu alihitimu 2015 na leo 2021 sijui kwa kujitolea alikuwa anaishije Kama siyo danganya Toto .
Kwa kuwa viongozi wote Ni CCM kuanzia mabalozi wa nyumba 10, wenyeviti wa vijiji/ mitaa, madiwani, wabunge, wakurugenzi, mapolisi, wabunge na wakuu wa mikoa bila kuwasahau mawaziri na rais Sasa tuelezeni tatizo. Sera na ilani yenu mliyoipigania na kulazimisha watanzania waipokee ifanye kazi la sivyo jiuzuluni.