Maendeleo yako ndiyo ya tanzania!

Simple

JF-Expert Member
Feb 6, 2009
249
121
Nilipata kujifunza ya kwamba Maendeleo ni mfumo na sio tukio, yaani kimombo wanasema ' Development is a Process, not an event'.

Hakuna anayepinga kwamba watu wa Tanzania wamepiga hatua kidogo kimfumo na kibinafsi yaani kwa mtu mmoja mmoja, lakini hatua zenyewe ni ndogo mno ukilinganisha na rasilimali watu na nchi.

Wakati umefika tukubaliane kwamba wananchi wa eneo husika hawafaidiki na rasilimali zao walizopewa na Maulana.

Binafsi sio mwanachama wala shabiki wa chama chochote cha kisiasa, lakini sera ya majimbo ya Chadema, ni sera endelevu sana kimaslai ya watanzania na Tanzania yenyewe. Ndugu Zitto wa Chadema ameeleza vizuri kwenye majibu yake na JF. CCM ikitaka inaweza kuiiga hii sera, cha muhimu waTanzania tufaidike na nchi ipige hatua stahiki.

Kila kona ya Tanzania ina mali, tena mali tele mpaka unaweza kushangaa Maulana alivyokuwa wa muweza, anza Mtwara,Kigoma, Katavi, Mara.Kilimanjaro,Tanga au mkoa wowote ule, Rasilimali ni nyingi, cha muhimu ni ufanisi 'competitiveness', vitendea kazi thabiti ' machinery' na Uongozi na siasa safi na endelevu kwa Watanzania wote.

Tunahitaji kuitumia 2015 kama 'turning point' au Mwanzo wa mwisho, Kama ni CCM, ije na Sera makini na endelevu hata kama inakopi kwa Chadema,sasa 2012, ili ifikapo 2015 tujilizishe yupi tunataka atuongoze. Na Chadema waendelee kutueleza na vitendo tuvione sasa hivi, kama kuna sera nzuri za CCM, wao pia ruksa kukopi.

Thamini Kura yako!!. KURA NDO KULA! Usikubali hata balozi wa nyumba kumi awe Kiraza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom