Maendeleo ya watu na sio vitu. Hii ina tafsiri ipi?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wana bodi,

Naamini wote tupo salama. Kuna kila sababu ya ku mshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote pamoja na ku muomba atuvushe salama katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Nimeji kuta kwa namna moja au nyingine kwenye kundi la watu ambalo lina Jiuliza maswali mengi kuhusu vipaumbele vya rais John Joseph Pombe Magufuli katika awamu yake ya kwanza ya miaka mitano. Vitu ambavyo vime jadiliwa sana ni pamoja na yeye kujenga uwanja wa ndege Chato, sehemu ambayo wananchi wanaweza kuwa na changamoto nyingi zenye umuhimu zaidi na kujenga flyover Ubungo Dar Es Salaam. Uhakika ni kwamba wana Chato hawa hitaji uwanja wa ndege ila wanaoishi Dar Es Salaam wata hisi kwamba flyover ime wasaidia sana.
Wanao fikiria kwamba vyote havikuwa vya muhimu wange stahili kufahamu kwamba kazi ya uongozi ni ngumu sana, kwa wakati wowote unaweza ukawa na mambo zaidi ya mia moja yanayo hitaji utekelezaji wako ila uka shindwa kufikia malengo yako yote kwa ukamilifu. Vile vile ni muhimu ku fahamu kwamba rais yeyote atakaye weza kuweka ki paumbele ku rekebisha miundo mbinu ya nchi nzima na kuweza ku kamilisha kila kitu kwa wakati ata kuwa ame tusaidia sana.

Tuki angalia upande wa pili, Mhe Tundu Lissu ame endelea na kampeni zake aki himiza "maendeleo ya watu na sio vitu" katika kuwa kwamua wananchi kiuchumi. Swali ambalo lazima tuji ulize ni: Maendeleo ya watu yana kuja kwa njia zipi?. Tanzania tunai fahamu wote tuna ishi hapa, njia pekee za ki halali zilizopo za mtu yoyote kuji kwamua ki uchumi ni ku ajiriwa au kuji ajiri mwenyewe. Njia pekee na halali ya ku kwamua wananchi ki uchumi ni ku ongeza ajira na njia za kuji ajiri wenyewe. Hali ya ajira nchini ina eleweka vile vile miundo mbinu yaku muwezesha mtanzania wa kawaida kuji ajiri na kupata kipato cha kawaida ni migumu sana.

Nafikiri badala ya Mhe Tundu Lissu ku ahidi kwamba ata leta maendeleo ya watu, ange eleza zaidi jinsi ambavyo ataweza kutekeleza ahadi hiyo.

Tafakari,
Jumanne njema
 
Back
Top Bottom