Altae04

New Member
Sep 11, 2021
4
2
Teknologia ni moja ya mandeleo makubwa yalioweza kuinua mataifa mengi kiuchumi kwa kuanzisha miradi mbali mbali inayoweza kuimarisha hali ya nchi kwa mfano teknologia imetumika kuvumbua kama ndege na meli ambazo zimesaidia sana kuinua uchumi wa nchi moja hadi nyengine, watu husafirisha bidhaa kutoka taifa moja kwenda jengine kwa kutumia miundo mbinu ya teknologia ya kisasa hatuwezi fananiza teknologia ha karne ya 18 na karne ya 21 ni tofauti kabisa, Ila vipi teknologia imesaidia kuinukuwa kwa uchumi wa nchi mbali mbali dunia na vipi imeleta hasara

Teknologia imewezesha mwanadamu kuishi mda mrefu kwa kuboresha huduma za kimatibabu na kugundulika vifaa vya kisasa vinavyoweza kufanyika huduma za kimatibu rahisi na inapelekea binaadam kuwa na matumaini ya kuishi mda mrefu ambapo atafanya kazi itakayoweza kupata faida yeye binafsi na serikali kwa pamoja kutokana mtu huyo ataweza kulipa kodi na nchi itaweza kuwa kubwa kiuchumi, na kutokana maisha kuwa marefu mambo mengi yataweza kuboreshwa ili ije kuwasaidia hapo baadae

Teknologia imepelekea kukua kwa uchumi katika dunia, ambapo mataifa yamejikita katika uzalishaji wa bidhaa mbali mbali kutokana na mahitaji ya watu katika eneo husika, kwa mfano kugundulika njia za kisasa za kilimo kumefanya watu kuishi na matumaini ya kuiona kesho kutokana chakula kupatika kwa mda muafaka, hivyo basi teknologia imesaidia wakulima kuinuka kiuchumi kutoka chini mpaka juu ambapo mazao huzalishwa kwenye ubora wa hali ya juu, na kuuzwa kwa bei nafuu ili kila mtu aweze kukidhi mahitaji ya upatikanaji wa chakula, hii ni tofauti na zamani ambapo teknologia ilikua ndogo, baadhi ya watu hawakuweza kununua vyakula kutoka bei kubwa ambapo wakulima hutumia mda mrefu kuzalisha mazao na baadae huuza kwa bei kubwa ambapo njaa iliweza kuenea maeneo mengi na watu walishindwa kuzaliana kutokana hawajui nini watukala kesho,kwa sasa watu wanaweza kuzaliaza kwa sana wakijua upatikaji wa chakula na mahitaji mengi ni rahisi mno

Aidha sio teknologia imesaidia kuinua maendeleo ya kiuchumi,kisiasa na jamii bali pia imeweza kuharibu jamii kutokana na haya maendeleo ya kiteknologia kwa kizazi cha sasa, ambapo waathirika wa hii teknologia ni vijana zaidi kuliko wazee, vijana hutumia mda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kwa kupoteza mda wao kwa mambo yasio na mantiki kwa wao,kwa mfano kijana anaweza kuangalia (Videos za ngono) ambazo itaweza kumpelekea huyo kijana kujichua na baadae hupelekea kupata madhara mbalimbali kama kwa wanaume hupelekea kusinyaa kwa uume, kuelegea kwa baadhi ya viungo, na hata kushindwa kufanya tendo la ndoa, pia vile vile vijana wanaweza wanaweza kutumia mda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kwa kufuatilia mambo yasiyo na faida baada ya kufanya kazi au kufuatilia fursa mbali mbali zinazotolewa kupitia mitandao au kusoma maandiko yanayochapishwa ambayo yatawaisaidia kwa njia moja ama nyengine kama vile nafsi za ajira,fursa za kusoma,kushiriki mashindano nakadhalika.

Teknologia pia imepelekea kukosa ajira kwa baadhi ya watu kutokana kwa kugundulika teknologia ambayo imeweza kutengeza vifaa vya kisasa vinavyosaidia kuzalisha kwa wepesi na haraka zaidi, Watu wengi wamekua wakilalamika kukosekana kwa ajira katika jamii, ambao watu hawa inaweza kuwapelekea wao kujingiza katika biashara ambazo sio halali kama vile uuzaji wa madawa ya kulevya, kuuza viungo vya binaadam na kadhalika, Hata hivyo kukosekana kwa ajira baadhi ya watu wamekua wakitafuta njia mbadala ya kujikwamua kimaisha, mfano mtu anaweza kutengeneza application la kuagiza chakula popote pale mtu alipo anaweza kuletewa kwa wakati na mteja kuchagua bidhaa anayohitaji ikiwa ni chakula gani atachagua.

Kwa kumalizia, Vijana tunatakiwa zaidi tujikite katika kufiria mbeleni zaidi tusitosheke na kile tulichojifunza madarasani tunaweza tumia akili,maarifa na ujuzi tulio nao kutatua changamoto mbali mbali kwa kutumia teknologia ya kisasa ambapo kuna fursa nyingi zinapatika katika motandao, na tuwe miongoni mwa watu wanaotumia teknologia kuingizia kipato, pia watu wasijikite na kuridhika na kitu kwamba elimu yako itakusaidia kupata ajira bali utakiwa ufikiri kwa umakini ni njia ipi nzuri ya kuitumia teknologia kwa kutumia elimu uliyo nayo, Na mtu anaweza jihamasisha mwenyewe kuwa na anaweza kugundua vitu tofauti tofauti kwa kutumia teknologia ambayo itakayo pelekea uchumi wa nchi kukua na kuinunua fursa mbali mbali kwa vijana wengine.
 
Mkuu andiko zuri isipokuwa kwa kizazi hiki cha teknolojia na ambacho akili zake zinaendeshwa na Mbowe na Lissu kwenye jamhuri ya Twitter na Space- hutawaona.
 
Mkuu andiko zuri isipokuwa kwa kizazi hiki cha teknolojia na ambacho akili zake zinaendeshwa na Mbowe na Lissu kwenye jamhuri ya Twitter na Space- hutawaona.
Kila kitu kinaweza ikiwa utaweka nia na juhudi ya kulifanya jambo lako kuwa la kipekee kwa kutumia teknogia pia na kuwepo tiyari kwa namna yeyote ile iwezekanavyo.
 
Back
Top Bottom