Maendeleo ya Tanzania kwasasa yanategemea huruma za Mungu tu!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,826
2,000
Tanzania imefikia wakati hatuwezi kutegemea wasomi au viongozi kwa kuendeleza nchi yetu bali mungu tu!. Ukiangalia vizuri
(1) Kilimo kinategemea mvua ambayo inabidi tumuombe mungu kwasababu hakuna mikakati ya misingi ya kilimo cha umwagiliaji. Kilimo kwanza ni deal za watu za matrekta lakini hakuna jitihada za kufundisha wananchi umwagiliaji. Mvua isikonyesha tunaomba mungu na misaada kwa nchi kubwa.
(2) Umeme: Umeme wetu unategemea sala ili mungu alete mvua kwasababu pesa ya genereta zimeliwa na viongozi na shirika ka Tanesco linaenda kwa hasara
(3)Shule: Kama ujasali vizuri siku ya mtihani wa form six au four mbona utakuwa hatarini kwasababu elimu yetu inategemea mtihani moja tu.
(4)Afya: Tanzania ukipata heart attack huko kijijini huwezi kupona! hii inatisha sana hatuna fire, hatuwezi kufanya upasuaji kitu kilichobakia ni kusali!
Kuna mengi ndugu zangu kama mikataba n.k lakini nchi yetu inaenda kwa uwezo wa mwenyezi mungu tu!
 

KunjyGroup

JF-Expert Member
Dec 7, 2009
352
170
Nakubaliana nawewe 100%.
Tatizo kubwa hatuna viongozi kwenye moyo wa uzalendo. Sisiem imejaa walafi na wanafiki. Hamna jipya ndie maana miaka 49 ya uhuru hatuna cha kujivunia
 

MWANALUGALI

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
601
0
Ndo maana Kakobe, Mwingira, Lwakatare, Mwakasege na wengine wengi wa namna hiyo wanapata wafuasi wengi sana!!!!!!! Yesu ni Jibu
 

mams

JF-Expert Member
Jul 19, 2009
614
195
Hakika ndivyo. Cha ajabu hakuna chochote kinachotolewa na Tanesco wala Mamlaka za maji kama dawasco kwa ajili ya shukrani kwa huruma zake mnyazi mungu. Zaidi ni malalamiko mto Ruvu umepungua au kina cha maji mtera kiko chin. Kwa kuwa wamehiari kuishi kwa kudra za mnyazi mungu basi wamjengee nyumba za ibaada.
 

LGMJAMII

Member
Nov 5, 2010
44
0
100% Ndugu yangu, yaani kukosa MUNGU SIJUI hata sisi tungekuwepo kwani baadhi ya viongozi wa nchi wamefikia hatua hata ya kukubali kuanzisha Project huku wakijua kuwa zina madahara kwa Wtanzania na Mazingira pia...
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,068
2,000
Hakika ndivyo. Cha ajabu hakuna chochote kinachotolewa na Tanesco wala Mamlaka za maji kama dawasco kwa ajili ya shukrani kwa huruma zake mnyazi mungu. Zaidi ni malalamiko mto Ruvu umepungua au kina cha maji mtera kiko chin. Kwa kuwa wamehiari kuishi kwa kudra za mnyazi mungu basi wamjengee nyumba za ibaada.

Mkuu mungu si mjinga. Kama unajiibia wewe mwenyewe unategemea mungu akusaidie vipi. Wezi tunawajua halafu tunaendelea kuwasifia, majambazi tunawajua tunaendelea kuwachekea, so Mungu atausaidie vipi.

Tunatakiwa kuonesha kuwa hatutaki hayo then ndio tuanze kuomba msaada, tunayapenda haya ndio maana tuko hivi.
 

mfarisayo

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
5,161
2,000
Hapa tusimtwishe mungu msalaba ni wetu wenyewe kwa kukubali tisheti, kofia na kanga tumejikaanga
 

Mkorosai

Member
Nov 17, 2010
65
0
CCM wametudanganya sana kiasi cha kutosha mpaka sasa taifa limechanganyikiwa halina dira, vipaumbele wala mikakati ya maendeleo!! Kila kitu ni zimamoto tu. CCM wameua fikra za watanzania.
 

amanibaraka

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
285
250
... And is it different in other african countries?
... And do you think things will change if a certain party comes to power?
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,211
2,000
Umenena kila siku ni afadhali ya jana, sijui nchi hii wangepewa wazungu ingekuwa, ingawa wanakuja pale kigamboni kutoa mfano jinsi ya watu wa dunia hii wanavyopaswa kuishi, waache tu waje watupe mfano na maji ya bahari hii yatabadilishwa kuwa na matumizi mengi maana mito yetu ya janguani imejaa sumu kwa ufupi dAR HATUNA MTO, tuache hiyo Petroli bei juu, kila kukicha wenye mabasi hawafikilii kingine hila ni ngomo tu , sasa hii kufuru tangu mkuu huyu achukue againi, suakri haishikiki, maharage ya mia nne sasa bora hata ya samki kauzi ya kungatia ugali kama sio kula, alafu useme kilimo kwanza, hiki ni kilimo kuanza, au kwanza, kinaanzia wapi ikiwa watanzania wanatumia disel au petrol kulima kwa petrol hipi, au gesi iliyopanda mpaka kufikiria mkaa upya, tunaishi kama wazee wa kanga moja, yaani ukitaka kutoka nje unaomba ufunike mambo ndio uende kwa jirani kuomba chumvi na kauzu alafu ukirudish mke ndio aende mtoni!!
 

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
3,363
1,195
Kwa kumtegemea Mungu ...what is so wrong about it??

Mbona inaonekana kama kumtetegemea Mungu ni Kosa? Kivipi?
 

Kipre tchetche

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
238
0
M2 anakwambia wezi wote nawajua wauza
unga wote nawajua kwa nini hawakamati
au ndio miradi ya wakubwa haiingii akilini
kesho yupo kwa wafadhili wanatoa michango
Yao wezi wanatia ndani unasikia nimewapa
muda wajirekebishe utafikiri anaongea na
watoto wa chekechea .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom