Maendeleo ya Kweli Yataletwa na Watanzania: Kampuni ya Mafuta ya Total Yazindua Kituo cha Kwanza cha Watanzania, Total Tegeta Service Station

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alisema, Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe kwa kumiliki njia kuu za uchumi na uzalishaji mali, ili faida yote itakayozalizwa, ibaki nchini.

Katika kulitekeleza hili, Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa mambo mapya kuhusu umiliki wa vituo vya mafuta vya Total, ambapo imekuja na mpango kamambe uitwao DODO, kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta vya Total.

Fuatilia taarifa hii.
, ,

06/01/2019. Mwaka Mpya na Mambo Mapya, Total Yaja na Kitu Kipya, Yaipongeza Tanzania Kuendelea Kuwa Nchi ya Fursa, Yawataka Watanzania Kuchangamkia Fursa.

Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa kuwaletea Watanzania kituo kipya cha mafuta cha aina yake, na kummpongeza rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kwa kuendeleza mazingira wezeshi ya uwekezaji, kuifanya Tanzania kuendelea kuwa ni miongoni mwa nchi za Afrika inayoongoza kwa uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji na kuleta maendeleo, na kuwataka Watanzania kuzichangamkia fursa hizo na kuzitumia kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamo Rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika ya Kaskazini, Kati na Afrika ya Mashariki, Jean Philippe Torres, wakati wa uzinduzi wa kituo kipya na cha kwanza cha mafuta cha Total ambacho kinamilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100% kwa mtindo unaoitwa DODO, cha Total Tageta Service Station kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki (jana).

Bwana Torres amesema Tanzania inazo fursa nyingi sana na uwekezaji ambazo kama zitachangamkiwa, zitataleta maendeleo makubwa kwa Watanzania na taifa kwa ujumla, na maendeleo hayo yatakuwa na manufaa zaidi, endapo fursa hizo zitachangamkiwa na Watanzania wenyewe na makampuni ya Kitanzania, kitu kinachotakiwa ni kwa Watanzania kuangaziwa fursa zilizopo, kisha wahamasishwe kuchangamkia fursa hizo kwa kujengewa uwezo wa kimitaji, kiutaalam, kitekinolojia na kiuendeshaji, kuweza kuzitumia fursa hizo kuchochea maendeleo ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

Amesema Kituo cha Mafuta cha Total Tageta ni mfano hai wa kuigwa, ambapo Mtanzania mmiliki wa eneo hilo, ameangaziwa fursa, na yeye kuchangamkia fursa hiyo, hivyo Total Tageta Service Station ndicho kituo cha kwanza cha kujengwa Tanzania kwa kumilikiwa na Mtanzania na kuendeshwa na Mtanzania kupitia utaratibu wa Kampuni ya Total kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta unaoitwa DODO.

Akifafanua kuhusu DODO, Mkurugenzi wa Sheria na Ushirikiano wa Makampuni wa Total Tanzania, Marsha Kileo Msuya, amesema DODO ni kifupi cha maneno “Dealer Owned, Dealer Operated” ambapo kampuni ya Total inawawezesha Watanzania wenye nia ya kufanya biashara ya mafuta, kwa kuwaangazia fursa na kuwajengea uwezo wa kumiliki vituo vya mafuta vya Total na kuviendesha wenyewe, Total wao wanawapatia viwango vya ubora wa kimataifa wa vituo vya Total, misaada ya kitaalamu, kuwapatia wasimamizi wa ujenzi wa viwango vyao, na mwisho kuwapatia jina kubwa la Total na bidhaa za Total kwa utaratibu wa kibiashara unaoitwa franchise, hivyo vituo hivyo vya DODO, vina jina kubwa la Total, lakini vinamilikiwa na kundeshwa na watu binafsi Watanzania wa kawaida wenye kuchangamkia fursa.

Kwa upande wao, wamiliki wa kituo hicho cha Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo, ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, kwa Total kutambua fursa walionayo, wakawaita kuwaonyesha fursa hiyo, na wao bila kuchelewa, wakaichangamkia fursa hiyo, ambapo kampuni ya Total wakawajengea uwezo wa kimitaji, kitaalamu na kiuendeshaji, sasa wao ni wamiliki wa kituo hicho. Mama Mary Lymo amemshukuru Mungu na mume wake Vincent Lymo kwa kuwawezesha kuchangamkia fursa hiyo.

Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total

Total Kimataifa ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa kimataifa na ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi zaidi ya 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.
01Total Tageta Launch Press Photos.jpg
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (kushoto) akipokelewa na Meneja wa Sheria, Mawasiliano na Mahusiano wa Bibi Marsha Kileo Msuya (kulia) kuja kuzindua wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni mmiliki wa kituo hicho, Bw Vincent Lyimo
02Total Tageta Launch Press Photos.jpg

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wakijiandaa kukata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
03Total Tageta Launch Press Photos.jpg

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wakikata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
04Total Tageta Launch Press Photos.jpg

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, mara baada ya kukata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
05Total Tageta Launch Press Photos.jpg

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wakirejesha vikatio mara baada kukata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
06Total Tageta Launch Press Photos.jpg

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres akipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
07Total Tageta Launch Press Photos.jpg
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres akijaza mafuta ya kwanza, mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
08Total Tageta Launch Press Photos.jpg

09Total Tageta Launch Press Photos.jpg
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na wamiliki na menejiment ya Total Tageta mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Pembeni yake ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
10Total Tageta Launch Press Photos.jpg

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na wamiliki na menejiment na wafanyakazi wa kituo kipya cha Total Tageta mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Pembeni yake ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
Wajameni, haya mambo mazuri ya Total kwa Tanzania, hawakuanza leo!.

P
 
Pia habari hii imeripotiwa na media mbalimbali kama ifuatavyo
 
Attachments

  • Photo 1-The Guardian, 07-01-19. Pg.2.pdf
    424.5 KB · Views: 24
  • Photo 2-Daily News, 07-01-19, Pg. 2.pdf
    534.9 KB · Views: 18
  • Photo 3 and Story 1, Majira, 07-01-19. Pg. 12.pdf
    809.1 KB · Views: 27
  • Photo 4 and Story 2. Nipashe, 07-01-19. Pg. 10.pdf
    736.1 KB · Views: 23
  • Photo 5. Mtanzania, 08-01-19. Pg. 7.pdf
    393.8 KB · Views: 24
  • Photo 6, Story 3. Mtanzania 07-01-19. Pg. 2.pdf
    511 KB · Views: 22
  • Photo 7, Story 4. Habari Leo, 07-01-19. Pg. 2.pdf
    975.7 KB · Views: 24
  • Photo 8, Story 5. Tanzania Daima, 08-01-19. Pg. 2.pdf
    732.6 KB · Views: 27
  • Story 1, Daily News Pront Page and Pg. 19. 07-01-19..pdf
    864.1 KB · Views: 26
  • Story 6 Daily News, Story 7 Citizen, 07-01-19. Pg. 3 and 19..pdf
    775.8 KB · Views: 22
  • Story 8 Uhuru, 08-01-19, Pg. 22.pdf
    835.4 KB · Views: 25
Pascal sjakuelewa! Kituo cha mafuta tu kama tunavyoviona vya total nchi nzima. Total ni kampuni ya wafaransa, sasa mtanzania kuwa na kituo cha total cha kuuza mafuta ndiyo iwe habari kubwa. Labda sijaelewa. Kuna vitu pale Kongowe kinaitwa Muro, ni mwafrika, so what is strange with total. Nieleweshe please wala sina nia ya kukejeli, NO!
 
Pascal sjakuelewa! Kituo cha mafuta tu kama tunavyoviona vya total nchi nzima. Total ni kampuni ya waingereza, sasa mtanzania kuwa na kituo cha total cha kuuza mafuta ndiyo iwe habari kubwa. Labda sijaelewa. Kuna vitu pale Kongowe kinaitwa Muro, ni mwafrika, so what is strange with total. Nieleweshe please wala sina nia ya kukejeli, NO!
Ufaransa.
 
Kudos! Ni Depot au filling station? Kitahudumia hata ndege zetu? Hivi sheria inasema filling stations zinatakiwa/ vituo viwe umbali (Km) ngapi toka vingine kwa Dar as Salaam na Highways?
Wanabodi,

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alisema, Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe kwa kumiliki njia kuu za uchumi na uzalishaji mali, ili faida yote itakayozalizwa, ibaki nchini.

Katika kulitekeleza hili, Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa mambo mapya kuhusu umiliki wa vituo vya mafuta vya Total, ambapo imekuja na mpango kamambe uitwao DODO, kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta vya Total.

Fuatilia taarifa hii.

06/01/2019. Mwaka Mpya na Mambo Mapya, Total Yaja na Kitu Kipya, Yaipongeza Tanzania Kuendelea Kuwa Nchi ya Fursa, Yawataka Watanzania Kuchangamkia Fursa.

Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa kuwaletea Watanzania kituo kipya cha mafuta cha aina yake, na kummpongeza rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kwa kuendeleza mazingira wezeshi ya uwekezaji, kuifanya Tanzania kuendelea kuwa ni miongoni mwa nchi za Afrika inayoongoza kwa uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji na kuleta maendeleo, na kuwataka Watanzania kuzichangamkia fursa hizo na kuzitumia kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamo Rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika ya Kaskazini, Kati na Afrika ya Mashariki, Jean Philippe Torres, wakati wa uzinduzi wa kituo kipya na cha kwanza cha mafuta cha Total ambacho kinamilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100% kwa mtindo unaoitwa DODO, cha Total Tageta Service Station kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki (jana).

Bwana Torres amesema Tanzania inazo fursa nyingi sana na uwekezaji ambazo kama zitachangamkiwa, zitataleta maendeleo makubwa kwa Watanzania na taifa kwa ujumla, na maendeleo hayo yatakuwa na manufaa zaidi, endapo fursa hizo zitachangamkiwa na Watanzania wenyewe na makampuni ya Kitanzania, kitu kinachotakiwa ni kwa Watanzania kuangaziwa fursa zilizopo, kisha wahamasishwe kuchangamkia fursa hizo kwa kujengewa uwezo wa kimitaji, kiutaalam, kitekinolojia na kiuendeshaji, kuweza kuzitumia fursa hizo kuchochea maendeleo ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

Amesema Kituo cha Mafuta cha Total Tageta ni mfano hai wa kuigwa, ambapo Mtanzania mmiliki wa eneo hilo, ameangaziwa fursa, na yeye kuchangamkia fursa hiyo, hivyo Total Tageta Service Station ndicho kituo cha kwanza cha kujengwa Tanzania kwa kumilikiwa na Mtanzania na kuendeshwa na Mtanzania kupitia utaratibu wa Kampuni ya Total kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta unaoitwa DODO.

Akifafanua kuhusu DODO, Mkurugenzi wa Sheria na Ushirikiano wa Makampuni wa Total Tanzania, Marsha Kileo Msuya, amesema DODO ni kifupi cha maneno “Dealer Owned, Dealer Operated” ambapo kampuni ya Total inawawezesha Watanzania wenye nia ya kufanya biashara ya mafuta, kwa kuwaangazia fursa na kuwajengea uwezo wa kumiliki vituo vya mafuta vya Total na kuviendesha wenyewe, Total wao wanawapatia viwango vya ubora wa kimataifa wa vituo vya Total, misaada ya kitaalamu, kuwapatia wasimamizi wa ujenzi wa viwango vyao, na mwisho kuwapatia jina kubwa la Total na bidhaa za Total kwa utaratibu wa kibiashara unaoitwa franchise, hivyo vituo hivyo vya DODO, vina jina kubwa la Total, lakini vinamilikiwa na kundeshwa na watu binafsi Watanzania wa kawaida wenye kuchangamkia fursa.

Kwa upande wao, wamiliki wa kituo hicho cha Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo, ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, kwa Total kutambua fursa walionayo, wakawaita kuwaonyesha fursa hiyo, na wao bila kuchelewa, wakaichangamkia fursa hiyo, ambapo kampuni ya Total wakawajengea uwezo wa kimitaji, kitaalamu na kiuendeshaji, sasa wao ni wamiliki wa kituo hicho. Mama Mary Lymo amemshukuru Mungu na mume wake Vincent Lymo kwa kuwawezesha kuchangamkia fursa hiyo.

Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total

Total Kimataifa ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa kimataifa na ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi zaidi ya 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika. View attachment 990824View attachment 990825View attachment 990826View attachment 990827View attachment 990828View attachment 990829View attachment 990830View attachment 990831View attachment 990832View attachment 990833
 
Asante total n ufaransa. Nieleweshe la ajabu ni nini kuwa na kituo cha total? Hivi kimegharimu kiasi gani?
Zamani hivyo vituo unapewa tu uendeshe biashara lakini wamiliki wanakuwa wenyewe Total,Puma etc. Ukienda kinyume anapewa mwingine. Sasa hicho hapo ni cha mmiliki kabisa Total wanakuwezesha kinafikia kiwango chao cha kimataifa ila mmiliki ni huyo Mchagga unaemuona.
 
Pascal. Hiyo siyo furusa kama unavyosema. Yani unatakiwa uwe na eneo lako (kiasi gani inahitajika kumiliki site inayofaa) unapewa watalaam ili wakushauri kujenga kwa vigezo vya total (garama ya ujenzi ni yako hii itakuwa kiasi gani?) Kisha wao wanaweka nembo yao. Mafuta unanunua kutoka kwao au wanakukopesha ili ulipe baada ya kuyauza ( hii inaitwa networking market) hapa wanahama kwa namna ya KIJESUSI wa kiuchumi. Kekundu kekundu! Wajinga ndiyo waliwao. Mitaji yote waliyowekeza watahamisha na vituo walivyokuwa wanamiliki watawauzia watanzania kwa namna ya wazawa kumiliki uchumi.
 
Zamani hivyo vituo unapewa tu uendeshe biashara lakini wamiliki wanakuwa wenyewe Total,Puma etc. Ukienda kinyume anapewa mwingine. Sasa hicho hapo ni cha mmiliki kabisa Total wanakuwezesha kinafikia kiwango chao cha kimataifa ila mmiliki ni huyo Mchagga unaemuona.
Kumbe ilikuwa monopoly policy ya total , nimeelewa sasa! Walikuwa wana hire stations zao kwa watu! OK
 
Pascal sjakuelewa! Kituo cha mafuta tu kama tunavyoviona vya total nchi nzima. Total ni kampuni ya waingereza, sasa mtanzania kuwa na kituo cha total cha kuuza mafuta ndiyo iwe habari kubwa. Labda sijaelewa. Kuna vitu pale Kongowe kinaitwa Muro, ni mwafrika, so what is strange with total. Nieleweshe please wala sina nia ya kukejeli, NO!
Nafikiri total ni France

Sent from my SM using Tapatalk
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom