Maendeleo ya kweli Tanzania yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Paskali ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, kanuni kuu ya kwanza ya mwandishi wa habari, ni to seek the truth and to tell nothing but the truth!. Hivyo kama mwandishi wa habari mzalendo, ni mwandishi wa kundi la kina Tomaso, hatuamini kwa maneno matupu hadi tushuhudie na kujiridhisha kuwa huu ndio ukweli wenyewe halisi.

Preamble
Hili ni bandiko kuhusu Tanzania kupata maendeleo ya kweli, yataletwa na elimu, na ukweli. Tukiwa wakweli hatuwezi kudanganya. Tukiwa na elimu, hatuwezi kudanganywa, na hata tukidanganywa, hatuta dangayika!.

Maneno Mengi, Uwongo Mwingi, Ukweli ni Upi?.
Tangu kuibuka kwa sakata la mchanga wa makinikia ya dhahabu ya kampuni ya Acacia, kumesemwa mengi na kunaendelea kusemwa mengi, mengine ni kweli, mengine ni uwongo, na mengine ni maneno maneno tuu, hayana ukweli, hivyo kuna uwezekano kuna sehemu tunadanganywa na tunadanganyika, kuna sehemu tunadangaya na kujifariji na udanganyifu wetu kwa kujipa too great expectations kama kila Mtanzania kumiliki Noah, ukweli ukija kupatikana, ikikutikana ni uongo, kutakuwa na kibarua kigumu kuwaelewesha Watanzania kuwa Noah zilikuwa ni hadithi hadithi tuu!.

Ili Tanzania tuweze kupiga hatua za kweli za maendeleo ya ukweli, jambo kubwa la kwanza ni kuthamini ni elimu na ukweli, lazima tuuthamimi elimu na ukweli, kwa kuwekeza kwenye elimu, na kuitumia
elimu hiyo kutuwezesha kuutafuta ukweli, tuupate ukweli na tuuseme ukweli na kuwa wakweli daima. Truth is Everything.
Tulidanganywa Tukadanganyika!
Huko nyuma kwenye kashfa ya Richmond, Watanzania tulidanganywa, tukadanganyika, mwisho wa siku tukaumia na tunaendelea kuumia!. Kwenye Kashfa ya Samaki wa Magufuli, tulidanganywa, tukadanganyika, tukaumia na tutaendelea kuumia. Kwenye kashfa ya EPA, tulidanganywa, tukadanganyika, tukaumizwa, lakini hata baada ya kuwabaini majizi ya EPA, badala ya kuyashughulikia kikamilifu kwa mujibu wa sheria, tukaamua kujidanganya ili kujifariji, lakini mwisho wa siku tukaumia!. Kwenye kashfa ya Escrow nako tulidanganywa, tukadanganyika na tukaumizwa na hadi leo tunaendelea kuumizwa!. Hivyo kwenye hili sakata la mchanga wa makanikia ya dhahabu ya Acacia, Watanzania, tusikubali kudanganywa tena, tukadanganyika, au tukaamua kudanganya ili tuu kujifurahisha, lazima tutafute ukweli bayana usio tia shaka na tuambiane ukweli, hata kama unauma vipi, huo ndio ukweli wenyewe na siku zote, ukweli utasimama daima!. Viwango vya dhahabu kwenye makinikia tulivyo elezwa hadi kutoa bili ya deni la dola billion 190, ni vikubwa mno!. Kama ni kweli, then Tanzania ndio nchi inayoongoza duniani kwa uzalishaji wa dhahabu per cubic area, ila dhahabu yote hiyo imekuwa ikiibiwa hivyo kuingizwa sokoni unrecorded kuwa ni dhahabu kutoka Tanzania, and that being the case kuwa viwango hivyo ni vya kweli, then kila Mtanzania ni ukweli anastahili na anapaswa kumiliki Noah.

Kwa Nini Tunadanganywa na Kudanganyika?.
Wakoloni walipokuja Mwadui. walizikuta almasi zinaokotwa mtoni kama mawe mviringo ya mtoni, mababu zetu wa Usukumani, walizitumia kuchezea bao. Mzungu kuziona akajua hizi ni almasi, alirudi kwao, akatutengenezea gololi za rangi rangi, kisha akawaletea mababu zetu wa Usukumani kwa kuwagawia gololi na kubadilishana na almasi, wakazikusanya almasi zote na kutuachia gololi, wakaondoka zao huku mababu zetu wakifurahi sana na kuchekelea jinsi wazungu wanavyowapenda, na kuwathamini kwa kuwaletea zawadi nzuri za gololi, kumbe walifanya mazuzu!. Watanzania katika zama hizi za utandawazi na dunia kijiji kimoja, tusikubali kufanywa

Bila Elimu na Utafiti, Tutaendelea Kudanganywa na Kudanganyika!.
Kumbe mababu zetu walidanganywa, ila hawakujua kuwa wamedanganywa!. Ukiwa hujui, lazima utadanganywa tuu!. Hivyo ndivyo Watanzania tulivyodanganywa na hawa mabeberu, kwa kutokujua. Ukiwa hujuwahi kuonja embe maisha yako yote, ukiletewa pera na kuambiwa pera ndilo tunda tamu kuliko yote, ukilionja na kuliona utamu wake, utaamini ni kweli, ni mpaka utakapo onja embe dodo, ndipo utagundua kumbe pera sio tamu kuliko yote, sasa tamu kuliko yote ni embe. Ukija kuonja nanasi, utagundua kumbe ni nanasi, ukija kuonja tende ni tende, ukija kuonja asali, ndipo utagundua tamu kuliko vyote ni asali!.

Hivi ndivyo Tanzania inavyofanyiwa kwenye rasilimali zetu karibu zote, madini, utalii, mazao, na sasa gesi ya asili!, tunadanganywa na kudanganyika kwa sababu hatujui!.

Jee ni Kwanini Hatujui Hadi Tudanganyike?.
Tunadanganywa na kudanganyika kwa sababu hatujui!, kwa nini hatujui?, ni kwa sababu hatutaki kujua, tumeridhika na kudanganywa kama wale babu zangu Usukumani. Huwezi kujua bila kujifunza, ukionja pera na kuridhika ndicho kitu kitamu kuliko vyote, usipojaribu kuonja embe, nanasi, tende na asali, akitokea mtu kukuambia asali ndio tamu kuliko vyote, utambishia na kumuita muongo, huku uking'ang'ania pera ndilo tamu kuliko!.

Ili kuweza kujua, ni lazima kwanza ujifunze, elimu, elimu, elimu, ili kupata watu walioelimika, huwezi kuwadanganya wakadanganyika. Ukielimika utaweza kufanya uchunguzi na utafiti, yaani research. Nchi zote zilizopata maendeleo ya kweli, zinawekeza kwenye alimi na zinaenaendelea kuwekeza kwenye elimu na kufanya utafiti ili kujenga uwezo, capacity building. Wenzetu katika bajeti zao, wako very serious wanatenga asilimia fulani kwa elimu na asilimia fulani kwenye utafiti. Tungekuwa na elimu, tusingeingizwa kwenye mikataba ya kinyonjaji ya rasilimali zetu ambayo ni wizi mtupu!.Tungefanya utafiti kabla, kwenye Richmond, tusingedanganywa. Tungekuwa na elimu ya madini kwenye dhahabu tusingedanganywa, na tungefanya utafiti kwenye mchanga pia tusingedanganywa, na sasa hatuna elimu ya gesi, nako tunadanganywa na tunaibiwa. Tangu tumepata uhuru, tumekuwa tunapigana vita na adui ujinga, enzi za Mwalimu Tanzania tulipiga hatua kwa kutoa elimu bure tangu msingi hadi chuo kikuu, tukaanzisha UPE, Elimu ya watu wazima na kisomo cha ngumbaru, ulifikia wakati Tanzania tuliongoza bara la Africa kwa literacy levels. Tangu Magufuli na awamu yake ya 5, rais Magufuli, anamuishi Nyerere kwa vitendo kwa kuendeleza pale Mwalimu alipoishia, Magufuli anatoa elimu bure mpaka kidato cha 4, na kutoa mikopo ya elimu ya juu. Pia tumeanisha kutenga asilimia fulani kwa utafiti, japo sijui utekelezaji wake ukoje lakini we are on a right track.

Japo tunajinasibu kuwa Tanzania tunafuata diplomasia ya uchumi, kiukweli ni kwa maneno mengi kuliko matendo. Japo tuna balozi zetu mahali pengi, huko ubalozini hatuna waambata wa kiuchumi, huko nchi zote wanakochenjua mchanga wa makinikia ya dhahabu, kote tuna balozi zetu, zingeishatufanyia economic intelligence, kwa kufanya utafiti hata kujua tuu kontena moja la makinikia linanunuliwa kiasi gani, au kama wao wana toza tuu gharama za uchenjuaji, ni kiasi gani na baada ya kuchenjuliwa hao wenye mchanga, wanapata nini na nini kinapatikana kwenye mchanga huo?. It must be something valuable to justify kuingia gharama zote hizo kusafirisha mchanga.

Nani Mkweli Kati ya Tume za Magufuli na Acacia?.
Kwa kawaida ukweli huwa ni mmoja tuu, hakuna kweli mbili. Wenye mchanga wao ambao sisi ndio wezi wetu, wanadai wao ndio wakweli, hawaibi, na kwa sababu wao ndio huchenjua, wanasisitiza walichoandika ndicho hicho hicho kinachopatikana. Huu ndio ukweli wao!. Tume za Rais Magufuli, zimepima sampuli za mchanga ule, na kukuta ni dhahabu ni mara kumi ya viwango vya declarations za Acacia, hivyo kuamini wao Tume ndio wakweli, hawa Acacia wamekuwa wakituibia miaka hii yote!. Kati ya wawili hawa, kuna matatu,
1. Mmoja ni mkweli na mwingine ni muongo.
2. Wote ni waongo ukweli ni mwingine
3. Ukweli halisi.

Real Life Scenario ni kama ifuatavyo.
1. Jee Acacia ni Wakweli ua ni Waongo, Wezi Wakubwa Hawa?!.

Kwa vile Acacia ndio huuchimba huo mchanga, na kuupeleka kuuchenjua huo mchanga, wao ndio wanaweza kuwa wakweli number moja, kuwa huo ni mchanga wa kweli, wanacho declare ni ukweli mtupu na ndicho kinachopatikana, lakini pia kwa vile wanajua sisi hatujui na hatuwezi kujua, inawezekana kabisa wanaacha dhahabu nyingi ili kutuibia, hivyo hawa Acacia ndio waongo na ni wezi wakubwa hawa!.

2. Tume ya rais Magufuli, Wanaweza Kuwa Wakweli Wamewabaini Acacia ni Wezi!.
Tume ya Magufuli wanaweza kuwa ndio wakweli, kupitia vipimo vya sampuli, wamegundua dhahabu yetu ni mara 10 ya viwango vya declarations za Acacia walivyo decrare, hivyo wamewashutukia wezi hawa waliotuibia kwa miaka mingi. Ila pia, kwa vile Tume haijakwenda kuuchenjua huo mchanga na kuthibitisha takwimu zao, inawezekana kabisa, baada ya rais Magufuli kutonywa kuwa tunaibiwa kwenye hivyo utafiti wa tume sio kuchunguza kilichomo bali ni kumtafuta mwizi, sasa inapotokea hajamkamata mwizi, ili usionekane hujafanya kazi, unaamua kupiga kelele za uongo za mayowe ya mwizi! mwizi!, kisha unarudisha majibu ya uongo kuwa tulimuona mwizi, tukamkamata ila ametuponyoka na kuturoka. Hivyo Tume za rais Magufuli zimepika data kwa kutoa matokeo ya kutunga ili kumfurahisha rais Magufuli, hivyo tume ni waongo!. Ili kujua nani muongo, nani mkweli, ni baada ya kutoka matokeo ya uchenjuaji.
3. Inawezekana wote ni waongo, kwa Acacia kupewa vipimo na wachenjuaji ambao ndio huwaibia Acacia kwa kuwalipa dhahabu kidogo, na tume kwa kutochenjua, vipimo huonekana vikubwa lakini katika uchenjuaji, kinachopatikana ni kidogo, hivyo kujikuta walisema uwongo kwa ujinga tuu wa kutojua.
Jee Tutapataje Ukweli.
Kwa vile nia yetu ni kuujua ukweli ili tusidanganywe na tusidanganye, njia ya kuujua ukweli halisi kuhusu thamani halisi ya makinikia haya ni moja tuu, tuutaifishe mchanga wote tukauchenjue mahali tunapopajua sisi, ila kuwepo mwakilishi wa Acacia, kisha tuthibitishe kinachopatikana, kikiwa ni kile kile kiwango cha Acacia, then Acacia ni wakweli, tume ndio waongo, tutawaomba radhi na kuwalipa fidia na kuwaruhusu kuendelea kusafirisha mchanga wa dhahabu. Ukiwa kiwango kweli ni kikubwa, then tume ni wakweli, Acacia ni majizi, tutapigiana hesabu ya containers zote zilizosafirishwa tangu container la kwanza, watulipe fidia kwa wizi wote waliotuibia kwa miaka yote hiyo kila Mtanzania apewe Noah yake!.

Hitimisho.
Wakati tunasubiri ukweli halisi utaopatikana kwa utafiti, nashauri kwa kipindi hiki cha kusubiria ukweli halisi, tujitahidi tuweke akiba ya maneno, tupunguze kuwaaminia sana hawa wanasiasa wetu, walituingiza chaka kwenye Radar, Richmond, EPA, Escrow, Samaki wa Magufuli, hivyo hata hapa kwenye makanikia, wanaweza kutuingiza chaka, na pia tusiwanyooshe watu vidole kuwa ni majizi, kisa tuu fulani kasema, ikikutikana sio wezi, tutaweka wapi sura zetu?!,.

Hivyo this time around Watanzania wenzangu ambao ni wazalendo, lets seek the truth, and the truth will set us free, tusidanganywe tena, tukadanganyika, ila nasi tusidanganye!.
Jumapili Njema.
Paskali.
 
Wazo lako linafikirisha. Mwingine atasema elimu ipi tunayotaka kama tuna mabingwa wa jiolojia kama prof. Muhongo na wengine wengi? Elimu ilikuwa tatizo wakati wa uhuru, leo haipaswi kuwa tatizo. Nakuunga mkono kwenye kutenga hela ya utafiti. Bado pesa inayotengwa ni ndogo kuliko inayotengwa na majirani zetu wanaotuzunguka.

Hata hivyo naona ni busara kushikamana kama nchi, kuliko kuwa na wasiwasi na kuwaogopa zaid wazungu wakati tunajua fika wametuibia wazi wazi (mrahaba 4%) na kwa kificho. Tumuunge mkono rais, kama amekosea hewala. Walau yeye ameonyesha ujasiri wa kuwaambia hawa wawekezaji uchwara kuwa tumechoka kuibiwa.
 
Wasomi wa kiwango cha juu nchi hii ndio wametuweka matatani na sasa tuko njia panda hatujui nani wa kumuamini. Je tumuamini Prof Mruma? Tumuamini Profesa Muhongo? Je tumuamini msomi wa Harvard Andrew Chenge? Nazir Karamagi? William Ngeleja? Zitto Kabwe, Werema list ni ndefu sana.

Ila ukweli unabaki kuwa nchi zote zilizopata maendeleo toka kwenye rasilimali zake ni zile ambazo zilitumia raia wake kuchimba na kuuza rasilimali hizo, kupitia haya makampuni ya kimataifa tunaliwa tu, asilimia nne ni ndogo mno jamani
 
Mkuu Pasco mimi kwa kuanzia nataka kuona mikataba yote tangu awamu ya tatu hadi sasa inawekwa hadharani ikiwemo hii ya ndege toka Bombardier na Boeing. Kuwe na jopo la wanasheria, wachumi na Wabunge wenye kuweka maslahi ya nchi yetu mbele waiangalie mikataba hii kwa kina kuanzia ile ya sasa na kurudi nyuma na kutoa mapendekezo yao nini kifanyike ili kuhakikisha hatupigwi tena katika hii mikataba, na pia waje na pendekezo la njia mbadala la kuhakikisha kunakuwepo na transparency kubwa sana kwenye mikataba yote nchini pale tu inapoanza kujadiliwa hadi inaposainiwa ili kuepusha huku kupigwa kwa miaka chungu nzima sasa ambako kumeligharimu Taifa matrillioni ya shilingi.
 
Wazo lako linafikirisha. Mwingine atasema elimu ipi tunayotaka kama tuna mabingwa wa jiolojia kama prof. Muhongo na wengine wengi? Elimu ilikuwa tatizo wakati wa uhuru, leo haipaswi kuwa tatizo. Nakuunga mkono kwenye kutenga hela ya utafiti. Bado pesa inayotengwa ni ndogo kuliko inayotengwa na majirani zetu wanaotuzunguka.

Hata hivyo naona ni busara kushikamana kama nchi, kuliko kuwa na wasiwasi na kuwaogopa zaid wazungu wakati tunajua fika wametuibia wazi wazi (mrahaba 4%) na kwa kificho. Tumuunge mkono rais, kama amekosea hewala. Walau yeye ameonyesha ujasiri wa kuwaambia hawa wawekezaji uchwara kuwa tumechoka kuibiwa.

kushikamana katika ujinga? wakati hiyo mikataba inasainiwa si alikua anasema ndioooo, mara ngapi alikua akisimama bungeni na kuwasifia viongozi wajuu yake kua ni wachapa kazi kwelikweli? leo hii Muhongo anahukumiwa kwa makosa walioyafanya akina mkapa? mi naweza shikamana nawewe kwenye mambo ya maana au hata kwenye kupeana burudani ndani ya sita kwa sita na sio hizi kiki za cheap popularity.......
shikamaneni wenyewe ndani ya giza lililopo katika kichaka cha ujinga uliokubuhu
 
kushikamana katika ujinga? wakati hiyo mikataba inasainiwa si alikua anasema ndioooo, mara ngapi alikua akisimama bungeni na kuwasifia viongozi wajuu yake kua ni wachapa kazi kwelikweli? leo hii Muhongo anahukumiwa kwa makosa walioyafanya akina mkapa? mi naweza shikamana nawewe kwenye mambo ya maana au hata kwenye kupeana burudani ndani ya sita kwa sita na sio hizi kiki za cheap popularity.......
shikamaneni wenyewe ndani ya giza lililopo katika kichaka cha ujinga uliokubuhu
Wewe jamaa huna usingizi, so unabisha ili upate kampan ya kukesha. Mim naenda na hoja, ubishi wa School Debates sina.
 
Shida ya nchi hii ina wapumbavu wengi mno....

Ina wajinga na mazezeta wengi mno.... wengi huendeshwa na upepo na uwezo wa kufikiri ni duni sana!

Akili ndogo zimetufanya kutekwa na upepo na si facts...

Kila nikiiona Symbion pale Ubungo na nikikumbuka saga la Richmond nasikia hata kinyaa kuwatazama baadhi ya watu!!
 
Watanzania sasa ifikie hatua tuache mihemko ya kisiasa. Viongozi wa serikali wanapofanya maamuzi ya kisiasa watanzania tutafakari sana sio kuunga mkono tuu pasipo tafakuri. Serikali inaongozwa na binadamu, na bidadamu siku zote si mkamilifu. Kumkosoa kiongozi wako anapokosea sio mwiko. Uzalendo halisi ni kukosoa panapoonekana kuna dosari kwa maslahi ya taifa, na inapobidi toa pongezi panapostahili.
Nchii hii tuna wasomi wengi tu -wamejaa katika kila tasnia. Serikali isijikite tuu katika kusikiliza maoni na ushauri wa wasomi wake, waangalie hata ushauri wa wasomi walio nje ya serikali. Hili suala mikataba mibovu ya madini ilishasemwa sana na baadhi ya wasomi na wanasiasa hapa tanzania. Leo serikali inakumbuka shuka kulishakucha na kuamua kuchukua maamuzi amboya moja kwa moja yataathiri uchumi wa taifa na kuopotezea nchi sifa kwa wawekezaji. Kama wasomi na wanasiasa wangesikilizwa mambo haya yangelikuwa yamekwishafanyiwa kazi, tena kwa ufanisi.
Kwa upande wangu binafsi nadiriki kusema Serikali imefanya uamuzi usio makini na usiozingatia matakwa ya kitaalamu katika hili sakata la makontena ya mchanga.
 
Wewe jamaa huna usingizi, so unabisha ili upate kampan ya kukesha. Mim naenda na hoja, ubishi wa School Debates sina.

wewe je una usingizi? unajua nilipo mrembo? dunia duara pengine we kwako usiku mi mchana.... anya way kama umechoka pumzika baby na kesho nayo ni siku.... te eamo mi vida. ami me encanta la manera de tus razones, creo que eres una mujere intelegente y fuerte que tenga buenas noches. adios amigita mia.
 
Preamble
Hili ni bandiko kuhusu Tanzania kupata maendeleo ya kweli, yataletwa na elimu, na ukweli. Tukiwa wakweli hatuwezi kudanganya. Tukiwa na elimu, hatuwezi kudanganywa, na hata tukidanganywa, hatuta dangayika!.


Paskali hutabiriki, juzijuzi tu hapa umemtetea aliyezungusha ukasema jambo la muhimu ni uwezo wake wa kuthubutu hata kama alizungusha, hebu tushawishi kaka
 
Ila ukweli unabaki kuwa nchi zote zilizopata maendeleo toka kwenye rasilimali zake ni zile ambazo zilitumia raia wake kuchimba na kuuza rasilimali hizo, kupitia haya makampuni ya kimataifa tunaliwa tu, asilimia nne ni ndogo mno jamani


Naafikiana nawe 100% kuwa uvivu wa viongozi wetukatika kufikiri ni moja ya vyanzo vya haya yote, kama wangefikiri kwa kina muda wao wote wangeelekeza kusimamia rasilimali zetu wenyewe badala ya kuhongwahongwa huenda tungekuwa mbali,
 
Hivi inawezekana kuwa tulipata uhuru mapema mno tukiwa hatuna uwezo wa kujitawala?
Ndio. Wengi wanaweza wasielewe kwamba tulipata uhuru mapema kabla hatujapata uwezo wa kujitawala. Uwezo wa kujitawala hatafsiriwi kwa kuangalia ukubwa wa nchi, wingi wa watu na wingi wa wasomi. Uwezo wa kujitawala unaangaliwa katika misingi mikuu mitatu.
  1. SIASA SAFI. hii ni pamoja ma democrasia iliyokomaa, sio democrasia uchwara. Siasa safi haifuati democrasia ya kuambiwana nci za magharibi. siasa safi ni pamoja na kuwa na wanasiasa makini wenye kujitambua, sio wanasiasa wa kupinga kila kitu.
  2. UONGOZI ULIOTUKUKA. Nchi inakuwa katika wakati bora inapokuwa na viongozi walio makini, sio watawala wabinafsi. katika uongozi uliotukuka viongozi wakuwa watumishi, wanatumikia umma kwa uzalendo wa hali ya juu. uongozii unaoongoza kwa nidhamu iliyotukuka.
  3. UMOJA WA KITAIFA. Kamwe taifa halitakuwa tayari kujitawala kama ndani ya taifa hakuna umoja, mshikamano na amani. Taifa lisilokuwa na migogoro ya kisiasa na kijamii linakuwa limepevuka tayari kwa kujitawala.
Hivyo basi ni hakika kabisa Tanzania (ukipenda tanganyika) ilipata uhuru ikiwa bado haijapata uwezo wa kujitawala, na madhara yake ndio kutumbukia kwenye ukoloni mamboleo.
 
Ndio. Wengi wanaweza wasielewe kwamba tulipata uhuru mapema kabla hatujapata uwezo wa kujitawala. Uwezo wa kujitawala hatafsiriwi kwa kuangalia ukubwa wa nchi, wingi wa watu na wingi wa wasomi. Uwezo wa kujitawala unaangaliwa katika misingi mikuu mitatu.
  1. SIASA SAFI. hii ni pamoja ma democrasia iliyokomaa, sio democrasia uchwara. Siasa safi haifuati democrasia ya kuambiwana nci za magharibi. siasa safi ni pamoja na kuwa na wanasiasa makini wenye kujitambua, sio wanasiasa wa kupinga kila kitu.
  2. UONGOZI ULIOTUKUKA. Nchi inakuwa katika wakati bora inapokuwa na viongozi walio makini, sio watawala wabinafsi. katika uongozi uliotukuka viongozi wakuwa watumishi, wanatumikia umma kwa uzalendo wa hali ya juu. uongozii unaoongoza kwa nidhamu iliyotukuka.
  3. UMOJA WA KITAIFA. Kamwe taifa halitakuwa tayari kujitawala kama ndani ya taifa hakuna umoja, mshikamano na amani. Taifa lisilokuwa na migogoro ya kisiasa na kijamii linakuwa limepevuka tayari kwa kujitawala.
Hivyo basi ni hakika kabisa Tanzania (ukipenda tanganyika) ilipata uhuru ikiwa bado haijapata uwezo wa kujitawala, na madhara yake ndio kutumbukia kwenye ukoloni mamboleo.
" Hear say" moja nilisikia wakati Wwa harakati za kudai uhuru, Nyerere alikaribishwa chai na queen Elizabeth kwa mazungumzo. Malkia alimsifia kuwa sugar bowl, milk container na tea spoons vyote ni dhahabu ya Tanganyika. Haya yalimsononesha sana Nyerere.
 
" Hear say" moja nilisikia wakati Wwa harakati za kudai uhuru, Nyerere alikaribishwa chai na queen Elizabeth kwa mazungumzo. Malkia alimsifia kuwa sugar bowl, milk container na tea spoons vyote ni dhahabu ya Tanganyika. Haya yalsononesha sana Nyerere.
bila shaka alifikiri nyumbani Tanzania Ikulu anatumia vyombo vya silver, glass na ceramic! Ngozi nyeupe ilishasepa na dhahabu yote
 
Back
Top Bottom