Maendeleo ya kiuchumi yatafikiwa kwa kutekelezaji halisi wa sera ya madaraka wilayani

nyatofundi

Member
Apr 3, 2012
15
7
Serikali za mitaa ni serikali kamili katika ngazi ya chini yaani Halmashauri. Sera ya madaraka mikoani iliyopo ingeleta matokeo chanya ya maendeleo ya kiuchumi kwa watu kama ingepeleka madaraka hayo katika ngazi ya halmashauri kuanzia mapato na matumizi yake.

Sasa hivi, madaraka hayo yanapelekwa katika utekelezaji wa vimiradi vidogo na ukusanyaji wa mapato kwa vyanzo vichache na visivyo na mapato makubwa. Matokeo yake halmashauri husubiri fedha toka serikali kuu ambayo inatoka kwa walipa kodi wa maeneo yao kupitia TRA. Pesa toka serikali kuu huwa ni ndogo isiyokidhi mahitaji ya wakazi wa kila Halmashauri.

Matokeo yake huduma za jamii kutolewa kwa viwango vya chini na si za kudumu. Mfano ujenzi wa shule za kata ni wa ulipuaji shule nyingi hazitadumu kwa miaka 20 ijayo, wakati shule tulizorithi toka ukoloni majengo yao bado ni imara hadi sasa. Barabara nyingi za mitaani yaani ndani ya halmashauri husika ni ndoto kuja kuwekwa lami kwa miaka 10 ijayo, maana fedha za barabara kutoka serikali kuu ni kiduchu mno hazin uwiano na mahitaji n.k.

Nchi zilizoendelea na zinazoinukia kuendelea kila halmashauri inajitegemea na inawajibu wa kukusanya mapato yake yote na kutumia kwa mujibu wa sheria ndogo zao ambazo huandaliwa kwa kufuata katiba ya nchi. Mfano Beijing Municipality, China chini ya Meya wake taasisi kama TRA, DAWASCO, TANROAD, SUMATRA,HOSPITALI NA MASHULE vina wajibika kwake, mapato yote anadhbiti yeye na kubakiza 75% Beijing na 25% kwenda serikali kuu kuendeshea serikali ya jumla maana sera ya china inaamini watu na mahitaji yapo katika halmashauri na sio kwenye wizara kule hakuna watu.

Ifikirie DSM, kama TRA ingebakiza 75% pale kweli meya angeshindwa kujenga flyovers? Kisingizio cha kwamba, sehemu nyingine ni maskini watashindwa kuishi ni uvivu wa kufikiri maana kila mahali kuna raslimali nikuuhangaisha ubongo kidogo tu hasa wa mbunge kuzitumia raslimali zilizopo na matokeo kila mahali patazalisha kuliko kusubiri 70% ya mapato toka DSM yatawanywe nchi nzima ni methodology ya zamani mno, hata wakoloni waliotuachia mfumo huo hawautumii.

Viongozi wetu wabadilike wakitembea huko, wajifunze wasiishie kununua suti tu. KWA SERA HII ILIYOPO KUPATA MAENDELEO NCHI HII ANGALAO KUFIKIA NDOTO YA NCHI YA WATU WA KIPATO CHA KATI YAANI KUUPUNGUZA UMASKINI KWA KIWANGO CHA KURIDHISHA NI NDOTO.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom