SoC01 Maendeleo ya jamii hutokana na jamii kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana

Stories of Change - 2021 Competition

Denis1729

Member
Sep 9, 2021
34
109
Maendeleo ya jamii hutokana na jamii kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana kwa urahisi kutokana na demokrasia imara pamoja na utawala bora ambao utaongozwa na katiba ya nchi katika kuweka vipaumbele vinavyoleta maendeleo bila kuathiri maisha ya mwananchi, kutambua majukumu ya viongozi na kutatua kero za wananchi wao, kuhakikisha viongozi wanakuwa na weledi wa kazi na kujua ukomo wa mipaka katika kutimiza majukumu yao pia wananchi kuwajibika katika shughuri za maendeleo, kuheshimu na kutii sheria pamoja na kulinda amani, mshikamano, upendo na usalama wao.

Sheria zichukuliwe kwa utoaji wa taarifa zinazoweza kuleta taharuki, matumizi ya lugha chafu/matusi hasa kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na upande wa wasanii kwani kumekuwa na uchapishaji wa taarifa ambazo sio za kweli mitandaoni na kwenye vituo mbalimbali za habari, sheria hizi zinakuwa zinazingatia matumizi sahihi ya maneno katika tasnia mzima ya Sanaa kwa ajili ya kuboresha na kukuza lugha ya taifa letu.

Uboreshwaji wa mitaala katika ngazi zote za elimu upanue wigo wa elimu na sio kubomoa kwani ubora wa mitaala unaweza kuongeza thamani ya elimu au kuibomoa kabisa na kuonekana haina thamani kutokana na mitaala ulivyo ukiringanishwa na mitaala iliyopita pia wizara ya elimu kuhakikisha mada zote zinafundishwa kwa wakati kupunguza idadi ya mwanafunzi wanaofeli sababu kutokana na kutofundishwa mada zote hivyo kushindwa kuyamudu baadhi ya maswali ambayo hayajafundishwa. Pia maswali ya mifano yaendane na maswali ya mazoezi hasa katika somo la Hisabati kwani watunzi wa vitabu wamekuwa wakitunga mifano rahisi kulinganisha na maswali ya mada husika. Angalau kila shule iwe na walimu wa kutosha ili walimu wapate muda wa kupitia namna wanafunzi wanamudu somo analofundisha tofauti na mwalimu mwenye masomo mengi ni ngumu kupitia kutokana na uwepo wa wanafunzi wengi mashuleni.

Utoaji wa elimu kwa vijana jinsi ya kujiajiri na kuwawezesha inaweza kusaidia na kupunguza kiwango cha vijana kukaa mtaani bila kazi kwa kuwapatia mikopo na kuwapa elimu juu ya uwekezaji kama biashara na kilimo kwa kutoa vitendea kazi kama mbegu, mbolea na dawa. Lakini pia sheria ziwepo kwa ajili ya vijana wanaokwenda kinyume na sheria kwa kufanya uharibifu wa mali na kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na uvutaji wa bangi hali ambayo inaweza kuongeza idadi ya vijana tegemezi na kurudisha nyuma maendeleo ya jamii.

Huimarishwaji wa huduma za afya, gharama za matibabu zisiwe kubwa, elimu itolewe jinsi ya kujikinga na wagonjwa ya milipuko na jinsi ya kujikinga na magonjwa yasiyoyakuambukizwa kama kisukari, shinikizo la damu, selimundu, utoaji wa bima za afya katika jamii ili kupunguza wananchi kushindwa kupata huduma kwa sababu ya kukosa ela kwa ajili ya matibabu. Pia uwepo utaratibu wa utoaji huduma kwa wale wanaotibiwa kwa msamaha kupata vibari maalumu kuepusha usumbufu wa kukosa huduma kwa kukosa vibari vinavyowatambulisha kuwa hawapaswi kulipia gharama za matibabu.

Ni vyema kuomba mungu na kumchunguza na kujiridhisha pindi unapokuwa unatafuta mwenza wa kuwa na mahusiano nae ili kuepuka kuumizwa na kupoteza muda kwa ajili ya mtu asiyekuwa na malengo na wewe pia tujifunze kusameheana, kuheshimiana na kuvumiliana kwenye mahusiano kwani hakuna aliyemkamilifu yaani tusikilizane na tukosoane mtu akienda tofauti na tujifunze jinsi ya kuishi pamoja kwani changamoto ni sehemu ya maisha. Pia vijana wa kiume na like kupunguza vigezo au sifa katika kuchagua mtu wa kuwa nae kwani hakuna mtu ambae anaweza kukidhi vigezo vyote 100% hii ni kutokana na vijana wengi kujiwekea baadhi ya tabia au sifa fulani zitakazomfanya awe na mahusiano na mtu fulani.
 
Back
Top Bottom