Maendeleo ya Chato au popote pale nchini ni maendeleo ya Taifa zima

Njoo wilaya ya Kakonko ujionee hali ilivyo mbaya ndio utastaajabu ya Chato!

Unaenda kujenga uwanja wa mpira wa kimataifa Chato? Kweli inaingia akilini?

Yaani watu wa Kigoma, Rukwa, Kagera na Shinyanga wakafuate huduma ya hospitali ya rufaa Chato? Kweli?

Kuweni na mshipa wa aibu,sio kulamba tu miguu ya watu!

Hata Mobutu alijenga kijijini kwao ambako ni ndani ya DRC!Hali ikoje sasa hivi?
Achana na Mabuto aliyejenga bila kuweka miradi na vitu endelevu na yenye muunganisho!
 
Dhana ya Maendeleo nchi isipotoshwe na watu wachache kwa sababu zao lakini uhalisia ni kwamba maendeleo yanayofanyika Chato yasichukuliwe kuwa ni upendeleo la hasha. Tukumbuke kuwa Taifa hili limejengwa kwa misingi ya umoja tangu kipindi cha awamu ya kwanza ya Mwl. Nyerere hivyo ukiangalia mkao wa nchi hii ni tofauti na majirani zetu.

Mkurya yuko Chato, Mhehe, Mnyamwezi, Mngoni, Mchaga, Mpare,Mmasai, Mhaya nk. Na wote kwa dini na itikadi zao za siasa ni wanufaika wa huduma na uwekezaji wa hapo Chato. Hii ndiyo Tanzania. Chato haijengwi na wanachato wazaliwa pekee. Tanzania Ya Sasa na Utandawazi umeondoa kabisa mipaka ya kiukabila, kiukoo na kifamilia.

Vijiji vya ujamaa navyo viliua mahame. Hii ndiyo modern society iliyojengwa kimchakato muda mrefu. Mfano Wachaga, wahaya, wasukuma wako kila wilaya na vijiji nchi, tumeona wasukuma wako Mbeya, Kigoma, Dar, Pwani huko waliko wakidai maendeleo na kuyatumia. Hivyo kwangu mimi maendeleo ya wilaya au kijiji chochote yanaakisi maendeleo ya nchi na taifa kwa ujumla.

Huu ndiyo mtizamo chanya unaofaa kuwepo. Dodoma kuna watu wa asili mbalimbali wamewekeza na kujenga hapo ni wanufaika wa maendeleo yanayofanyika hapo kwa sasa lakini wengine hatupigi kelele. Mnyamwezi aliyeko chato hawezi kulalamikia maendeleo hayo. Muhimu ukiona hivyo chukua kiwanja hapo na tumia fursa zilizopo kwa faida yako na taifa.

Mh. Rais amejitahidi sana kupeleka maendeleo ya miundo mbinu kila wilaya kwa sasa tunaona na amezingatia Ilani ya uchaguzi 2015. Watanzania tupunguze ulalamishi oh mara maendeleo ya vitu badala ya watu, oh mara maendeleo yana upendeleo wa kimaeneo! Hatumtendei haki Rais na tunamkatisha tamaa. Hakuna nchi yenye maendeleo kila mahali muhimu tuangalie kipaumbele na mantiki ya kupeleka maendeleo mahala je chato haistahili kabisa kupewa maendeleo? Kwanini? Je, siyo sehemu ya Tanzania?

Mimi nimefika Chato ni wilaya iliyokaa kimkakati, ardhi nzuri kwa uwekezaji, imezunguka ziwa na ni tambarare na milima michache, hali ya hewa nzuri iko karibu na Uganda, Rwanda, Burundi, DRC na hata Kenya. Imezungukwa na migodi ya madini, ufugaji, kilimo, misitu, uvuvi na hifadhi ya Rubondo na Burigi Chato. Pia ni satellite district nzuri kwa jiji la Mwanza, Geita, Bukoba na Shinyanga kwa kanda ya ziwa.

Ninaunga mkono waziri wa utalii kuifanya kituo cha utalii. Pengine ili kuifanya iwe na mipango endelevu hivyo nishauri miundo mbinu ya kiutalii ijengwe pale ili kujenga future ya malengo hayo. Ni lazima tusambaze utalii nchi nzima hususani maeneo mapya yanayoiburiwa (diversified -quality tourist designated areas) na hiyo ndiyo sera ya utalii.

Pia tupate wawekezaji pajengwe maduka makubwa ya mall. Tuboreshe pia maeneo yanayozunguka kanda hii mfano kujenga na kuboresha jumba la makumbusho la Bujora liwe la kisasa na kuiingizia taifa fedha kwa kuvutia cultural tourism, kujenga maofisi yanayoeleweka ya TANAPA, TTB na wizara ya utalii,chuo kikuu cha serikali kanda ya ziwa haina, tawi chuo cha madini, tawi la chuo cha utalii, kumbi za mikutano ili ku boost conference tourism, kisiwa cha ukerewe vinaweza ku link vizuri na maeneo mengine ya kanda hii na Ili chato iweze kuwa satellite developed city yenye muunganisho na vivutio vingine vya kanda ya ziwa. Maeneo maalum kama haya yanayoweza kuchagiza maendeleo nchini hayapo.

Tuanzie hapo tuachane na mijadala isiyo na tija.

Mungu ibariki Tanzania.
Chato hakutaendelea hata budget yote ya nchi ikipelekwa huko tatizo ni watu waliopo huko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom