SoC01 Maendeleo na mabadiliko katika jamii si jukumu la viongozi ama watu waliopo madarakani bali ni jukumu la kila mmoja

Stories of Change - 2021 Competition

jjoram

New Member
Aug 23, 2021
4
12
MABADILIKO KATIKA JAMII

UTANGULIZI
Katika jamii yoyote maendeleo na mabadiiko katika Nyanja mbaimbali ndiyo msingi imara na Madhubuti katika kuleta umoja,amani na ushirikiano ili kuendeleza tamaduni na mapokeo mbalimbali toka kizazi hadi kizazi.Yote haya yanachochewa na ustawi wa jamii katika kila sekta inayoifanya kuwa JAMII.
Maendeleo na mabadiliko katika jamii hayawezi kutokea iwapo jamii itabaki kuwa tuli (static) ni lazima ipitie hatua na marejeo mbalimbali ili kuendelea na kuleta mabadiliko.
Zifuatazo ni Nyanja mbalimbali ambazio ndiyo msingi wa maendeleo na mabadiliko katika jamii.

UCHUMI NA BIASHARA
Ili kuchochea mabadiliko katika Nyanja ya uchumi na biashara kuna umuhimu wa kuzingatia vichocheo mbalimbali ambavyo ndio chachu katika msingi wa mabadiliko ama kukua kwa uchumi na biashara.Si vitu vya kuletwa na meli,kununua dukani,kiwandani ama kuagiza ndani na nje ya nchi bali ni vitu ambavyo tuko navyo kila wakati.

i)Ardhi

Ardhi imebeba raslimali mbalimbali ambazo zote kwa ujumla ni msingi imara katika kuleta mabadiliko kwenye uchumi vilevile biashara.Kwa mfano hapa Tanzania ardhi yetu imebeba madini,udongo wenye rutuba kwa kilimo vyanzo mbalimbali vya maji na misitu.Vyote hivi vikitumiwa kwa utaratibu maalumu wenye tija kwa jamii hamna namna lazima yatokee mabadiliko katika uchumi ama biashara maana hivi ndio msingi kwa nchi yoyote duniani katika kukuza uchumi.Kumbuka kilichotokea 1884,Berlin Conference wakati wazungu kutoka nchi mbalimbali walikua wanagombania na kugawana sehemu mbalimbali za Africa zenye raslimali hizi ili kukuza uchumi na biashara katika mataifa yao.Hivyo si vizuri kupuuzia tulivyonavyo wenzetu wanaviona ni mbali.Jiulize tu makampuni ya madini kutoka nje ya nchi yanafanya nini Tanzania (GEITA GOLD MINE NA BARRICK)

ii)Fedha

Fedha pia ni moja ya chachu katika maendeleo.Haipingiki popote duniani kwamba kila nchi iliyo katika njia ya mafanikio ama mabadiliko ya uchumi na biashara inatakiwa iwe na msingi mzuri wa mapato.Kila nchi ina namna yake ya kupata mapato na njia kuu iliyozoeleka ni kodi.Si vyema kutegemea misaada kutoka nje ya nchi,hii inaongeza mzigo kwa taifa na kuzorotesha uchumi na biashara.

Kwa Tanzania tumeona njia mablimbali mpya za mapato(kodi kwa njia ya sim una nyumba kupitia luku) ambazo kama taifa itazitumia vizuri mabadiliko katika uchumi na biashara ambayo ni chanya bila shaka lazima yatokee.

iii)Watu
Watu pia ni msingi mzuri wa mabadiliko katika uchumi na biashara kulingana na yale wanayoyafanya katika mzunguko wa Maisha yao ya kila sku.Mabadiliko katika uchumi na biashara yanategemea watu kwani watu ndio msingi,wateja mna wahanga wa mabadiliko yoyote yanayotokea katika jamii hivyo kila wanachokifanya kinatakiwa kuna na athari chanya ili kuleta mabadiliko katika uchumi na biashara.

iv)Miundombinu na Teknolojia
Huu pia ni msingi imara katika kuleta mabadiliko ya uchumi na biashara kwani uwepo wa miundombinu bora na teknolojia huvutia mabadiliko katika nyaja hizi.Kumbuka tu,kwanini mataifabya ulaya yanaongoza kwa uchumi na biashara jibu linalokuja ni moja tu:toka enzi za utumwa wao walikua na miundombinu na teknolojia bora ambayo ilipelekea uzinduzi wa viwanda hivyo kuchochea mabadiliko ya uchumi na biashara na malighafi za viwanda walikuja kuchukua kwenye ardhi yetu,hivyo basi ili kuleta mabadiliko ya uchumi na biashara miundombinu na teknolojia ni lazima iwe katika hali nzuri itakayokaribisha mabadiliko
Sababu zote hizo tajwa hapo juu zinaweza kutumik pia katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya jamii.

KILIMO
Ili kukuza na kuleta mabadiliko katiko nyanja ya kilimo yafuatayo ni ya kuzingatia
kwanza kutumia njia mbadala ya umwagiliaji kuliko kutegemea mvua za msimu,kutumia mbolea na njia mbalimbali zinazoshauriwa na watalaamu wanaopatikana hapa nchini ili kuboresha kilimo,kuunda vyama mbalimbali vya wakulima ili kutafuta masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi ili kuongeza thamani ya mazao na pato binafsi na la taifa pia ili kupunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji maeneo yatengwe kati ya wakulima na wafugaji na yatambulike kisheria ili kuepusha migogoro kati yao vilevile serikali itoe mchango na iwe karibu na wakulima na wafugaji ili kuchangia pale wanapokwama na kulinda haki zao.Yote haya yakifanyika mabadiliko chanya yatatokea kwenye nyanja ya kilimo

SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Maendeleo katika nchi mbalimbali hapa duniani yamesukumwa na uwepo wa mfumo mzuri wa sayansi na teknologia.Kwa hapa Tanzania ili kuleta mabadiliko katika nyanja hii kama nchi kwanza inatakiwa ipitie nyaraka mbalimbali na mapokeo kutoka sehemu mbalimbali duniani ili kuona ni teknolojia ama sayansi ipi itafaa hapa nchini pili kujenga ushirika na uhusiano mzuri na nchi zilizoendelea ili kupata ujuzi mbalimbali katika maswala ya sayansi na teknolojia tatu,nchi ikishapitia hatua zote hizo inaweza kutazama sasa sayansi na teknolojia iliyopo nchi na kuiweka kwenye mizani na hizo za kigeni ili kuamua kuboresha ama kupokea sayansi na teknolojia kutoka nje kwa maendeleo ya nchi

DEMOKRASIA
uhuru wa watu katika kufanya maamuzi,uhuru wa vyombo vya habari,usawa baini ya watu,mgawanyo wa kazi katika nguzo zinazoiongoza nchi(bunge,mahakama na baraza la mawaziri),uwepo wa katiba inayofatwa na ulinzi wa haki za binadamu ni mambo madogo lakini ni ya msingi katika kujenga na kuimarisha demokrasia na kuleta amani baina ya watu,nchi mbalimabli imeshindwa kuzingatia mambo haya madogo na kuleta amani ambayo imekua ngumu kuirejesha kwa Tanzania tunajitahidi ila ni muhimu kuendelea kuzingatia mambo haya ili kutunza amani iliyopo utawala bora na uwajibikaji pia unaweza kuimarishwa kwa kuzingatia mambo haya

AFYA
zimekuwepo taasisi mbalimbali za afya dunia kama WHO Johns hopkins na zinginezo zikihakikisha afya ya kila mtu iko salama.Hapa Tanzania afya ya kila mmoja iko chini ya serikali maana yenyewe ndiyo inayojenga na kuboresha vituo vya afya mbalimbali ikisaidiana na mashirika binafsi.Ili kuboresha nyanja hii Tanzania inatakiwa iboreshe miundombinu mbalimbali ili kurahisisha ufikaji wa watu kwenye vituo vya afya kama barabara,kujenga vituo vingi kama inavyoendelea kufanyika kupitia makusanyo na kodi kwa njia ya simu,kuweka malengo mbalimbali kama kupunguza vifo vya mama na mtoto na kujitahidi kuyafikia,kuendlea kujenga ushirika na mataifa mbalimbali yaliyoendelea pasipo kuyategemea kwa ni hatari kiuchumi na yote kwa yote kuhakikisha uwepo wa wataalamu wengi katika vituo vya afya nchi ili kuboresha nyanja hii

HAKI ZA BINADAMU
kabla ya kuangalia namna ama njia yoyote ya kuleta mabadiliko kaitka haki za binadamu cha kwanza ni muhimu kuangalia kama haki hizo zipo,watu wanazitambua haki zao,je zinalindwa ndipo lije swala la kuboresha.Kama hayo yote yametiliwa maanani kilichobaki ni kuzilinda.zinalindwaje sasa?kwa kutoa taarifa sehemu husika kama vyombo vya dola kuusu uvunjivu wa haki za binadamu unapotokea,kutoa ushirikiano kwa taasisi zinazohusika na haki na binadam na yote kwa yote kuvitia moyo vyombo mbalimbali na vyama mbalimbali vinavyolinda na kutetea haki za binadamu.

Hitimisho:

Maendeleo na mabadiliko katika jamii si jukumu la viongozi ama watu waliopo madarakani bali ni jukumu la kila mmoja likianzia katika ngazi ya familia chini ya msingi mmoja tu USHIRIKIANO KATIKA KULETA MAENDELEO NA MABADILIKO KATIKA JAMII.

jjoram177
 
Back
Top Bottom