Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,361
- 2,734
Kuna baadhi ya Watanzania wenzangu wananishangaza na kunisikitisha sana. Na hii ni pale wanapo hadaliwa na viongozi wa chama na serikali iliyoko madarakani kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu mwaka 1961 tulipopata Uhuru hadi leo. Utakuta watu wanatoa takwimu za ajabu kwa kuwataja wataalamu wa kada mbalimbali kuwa walikuwa idadi hii - sasa hivi ni idadi hii, mara shule zilikuwa idadi hii- sasa hivi ni idadi hii, mara barabara za lami zilikuwa kadhaa za kilometa kadhaaa- na sasa hivi ni kilometa kadhaaa.
Utakuta Watanzania wenzangu wanatikisa vichwa kwa kukubali kwamba kweli tumesonga mbele. Mwanasiasa mwingine anajivunia maendeleo kwa kueleza idadi ya simu za mchina zilizoko vijijini ambazo zinapiga mziki mzuri na mawasiliano vilevile.
Labda wengine mtanishangaa kwa kudhani kuwa mimi nakataa kwamba hatujasonga mbele. Pamoja na kusonga mbele kunakoonekana mimi sishangai hata kidogo wala sioni Suprise ya kufanya sherehe kubwa eti miaka 50 ya Uhuru. Kwa yeyote anayedanganywa na takwimu za vitu vilivyoongezeka inabidi ajue kwamba ( kwa mujibu wa vitabu vingi zaidi ya 50 nilivyosoma vya sayansi ya jamii) ni kuwa "Any society is dynamic" .Yaani ni kwamba kila jamii ya mwanadamu lazima ishuhudie mabadiliko kadri siku zinavyozidi kwenda mbele. Utake usitake lazima mabadiliko yatokeee. Kwa hiyo vitu vinavyotajwa kuwa ni matunda ya miaka 50 ya Uhuru sio zawadi kwa watanzania bali ni wajibu, watanzania kama jamii mojawapo ya wanadamu kosonga mbele ilikuwa lazima. Ndiyo maana mie nasema sio gift wala suprise kama baadhi ya wanasiasa wanavyotakakuliweka suala hili. Haki ni ya kwako wewe unaandaliwa kupiga makofi.
Pili nauliza swali ambalo mie linaninifanya nichefuke, kuwa raslimali tulizonazo na na maendeleo haya ya miaka 50 tunayotaka kusherekea vinaendana/vinalingana au vinakaribiana? Sisi tuna maji ya kutosha mito, Maziwa Tanganyika, Victoria, Nyasa na mengineyo lakini tunapeta na giza, je unasherekea nini? Angalieni migodi tuliyoisikia tangu enzi hizo kama mwadui , na mingine ambayo kwa mujibu wa the "Tanzania National Website" haya ni majigambo:-
Maliasili Madini – dhahabu, almasi, tanzanite, mawe mengine ya thamani, gesi ya asili, chuma, mkaa wa mawe, maji ya chemchem, nta ya kung'ara, magadi na chumvi. Wanyama na Utalii: Mbuga 12 za wanyama, Eneo la Hifadhi la Ngorongoro, Hifadhi za wanyama 13, Hifadhi maalum za wanyama 38 na sehemu za hifadhi za utamaduni 120.
Uvuvi:Hufanyika kwenye maziwa makuu matatu ambayo ni Victoria, Tanganyika na Nyasa pamoja na mito na pwani ya Bahari ya Hindi. Pato la samaki linaloweza kupatikana kwa mwkaa mzima linakadiriw akuwa tani za metriki 730,000 kwa mwaka, ingawa kwa hivi sasa ni tani 350,000 tu kwa mwaka
Majaliwa ya rasilimali ya madini Almasia, Dhahabu,Metali za besi na kundi la platinamu,Metali za chuma,Bati,Vito,Kaoneti,Makaa ya mawe,Madini ya viwanda. Hapa wamesahau Nikel inayochimbwa huko Ngara maeneo ya Kabanga.
Kabla haya madini na raslimali nyingine hazijaanza kutumika ipasavyo Watanzania walio wengi walisoma bure na hata kupata chakula mashuleni, sasa muda huu kila kwenye madini panachimbwa ,wanyama wanawindwa, watalii wengi, wanafunzi wengi maskini wanakosa mkopo. Mtanzania unasherekea kipi. Mtu anashindwa kutimiza wajibu kisha tunajiandaa kushangilia. Tutashangilia kwa hali tofauti. Wakati wengine wanapiga miayo kwa ajili ya njaa, wengine wanapiga miayo sababu ya shibe. Maana miaka hii 50 wamevuna na wameshiba kwelikweli.Leo hii wauguzi hakuna vijijini, watu wanapoteza maisha, miaka 50 watoto wa shule Watanzania wanaenda shuleni bila viatu, Nyumba za walimu vijijini hata mjini tabuu, maabara hakuna, maji bado shida ila kwenye tovuti ya nchi tunajitapa kuwa tuna raslimali lukuki, maana yake nini? Tulipofika ni wajibu na ilibidi tufike lakini si kwa kiasi kidogo namna hiii. Ndio maana nashindwa nisherekee nini??!!!!
Fedha zilizoko mifukoni kwa watu ambazo ni jasho la watanzania ni nyingi ila sisi tunaleana. Wenye hizo fedha mifukoni wajiandae kusherekea maana wao wamevuna. Na ninaelewa watanzania wachache watakaopewa T-shirt na maji ya kunywa watashangilia lakini wakirudi nyumbani watakutana na giza kama kawaida. Badala ya kujisifu na sifa za kijinga tujiulize. Iweje sisi Watanzania wenye miaka 50 tangu tupate Uhuru bado maskini kiasi hiki wakati tuna raslimali nyingi????!!!!!. Uchumi wa Rwanda uko juu yetu pamoja na matatizo yote yaliyotokea. Sisi rushwa na kulindana tu.Angalieni kibwagizo kutoka tovuti ya taifa " Umasikini: Takriban asilimia 50 ya idadi ya watu wote nchini wanaishi maisha ya ufukara" hii inatajwa bila aibu wala uoga.
Kilimo ndo siwezi kusema, kila mwaka wakurugenzi na watendaji wa vijiji na kata wana kesi mahakamani kwa kuiba mbolea na mbegu za ruzuku, wizi wa pembejeo kila mwaka, power tiller zinatolewa kisiasa siasa tuuu hakuna mpago halisi kwamba tutaachana na jembe la mkono siku moja.Madini ndo yananiuma maana hata ripoti ya Bomani kuhusu
"Taarifa fupi ya kamati ya Rais ya kuishauri Serikali kuhusu Usimamizi wa sekta ya madini JuzuuNa. 2"utakutana na maelezo yanayoonesha kuwa wananchi wote wanasikitishwa na hali hii. Nanukuu:-
"Takwimu zinaonyesha kuwa shughuli za uchimbaji mkubwa wa madini zimeongezeka kwa kuanzishwamigodi mikubwa sita mipya ya dhahabu kati ya mwaka 1997- 2007. Vilevile kumekuwa na ongezeko la shughuli za uchimbaji wa madini ya vito kama almasi na tanzanite. Aidha shughuli za uchimbaji madini zimeongezeka kutoka wachimbaji wenyeleseni wapatao 2,000 mwaka 1997 na kufikia takribani wachimbaji 7,000 mwaka 2007.Takwimu pia zinaonyesha mchango wa sekta ya madini umeongezeka kutoka 1.7%mwaka 1997, na kufikia 3.8% mwaka 2006.
Miongoni mwa malalamiko ya wananchi ni pamoja na hali inayoonekana ya sekta ya madini kutochangia vya kutosha katika maendeleo ya nchi hasa ya kiuchumi na kijamii. Pia imeonekana kuwa mikataba ya madini inapendelea zaidi makampuni makubwa ya uwekezaji katika madini, huku kukiwepo na usiri mkubwa wa mikataba hiyo." Kwa taarifa nzima bofya hapa : http://swahili.policyforum-tz.org/files/ripotiyabomani.pdf
Kwa hili la sherehe ya miaka 50 ni sawa na kibarua aliyepewa kupalilia shamba la hatua 20 kisha akapatiwa chai ya maziwa nzito, maji ya kunywa, Chapati na nyama ili afanye kazi vizuri lakini kuanzia asubuhi saa 12 hadi jioni saa 11 alikuwa kapalilia hatua mbili tu!!! Alipoulizwa kulikoni mtu unapewa kila nyenzo ili ufanye kazi vizuri alijibu " kwani sikupalilia?" ukweli ni kuwa alipalilia lakini vitendea kazi alivyopewa na kazi iliyofanyika ni sifa ipi angepewa huyu bwana. Kazi ilikuwa ni moja kumuachisha kibarua huyo na kumtafuta anyefaa.
Hii ni sawa na sisi Watanzania ambao kwa akili zetu tunamg'ang'ania na kumshangilia kibarua huyo mwenye kula mikate, nyama, maziwa na kushiba lakini akapalilia hatua mbili. Na sisi Watanzania tutashangilia kweli siku hiyo. Kibarua anafaaa? Naomba niwasilishe japo kwa uchungu pale Haki ya mtanzania inapogeuzwa kuwa Gift (zawadi) tena yenye Surprise!!!