Maendeleo Mbadala (Alternative Development)

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
Maendeleo Mbadala (Alternative Development).

Nchi za Afrika tangu zipate Uhuru bado zina imani kubwa kuwa... "bila mikopo kutoka nje haziwezi kuendelea". Ni imani ambayo iko kichwani mwetu Waafrika. Na jambo hili limetupunguzia sana uwezo wa kufikiri tofauti ili kujiletea maendeleo. Kusema Kweli tuliowengi tumedumaa kifikra kama viongozi wetu walio wengi Barani Afrika.

Iran, Korea zote, Taiwan, Libya ya Muamal Ghadafi na nchi nyingi za Asia zilianza kuwaza kitofauti sana namna ya kuleta maendeleo baada ya kuchoshwa na mikopo ya Mashirika makubwa ya kifedha kama Benki Kuu ya Dunia. Wakaamua kujaribu alternative development yaani njia mbadala ya maendeleo. Waliamua kutumia raslimali zao kwa faida kwelikweli na wakaamua kuwa makini na mikopo ya nje Je leo hii wako wapi????. Pia waliwekeza katika TEKNOLOJIA ya kwao na hata ya kuiba pia ambayo ni ngumu na hatari kuifanya. Zaidi wakawa wabunifu katika mambo yao.

Barani Afrika tunatakiwa kufanya mambo yetu kwa kujiamini kabisa,

Mosi, jambo la Msingi kabisa ni kuthubutu na kupunguza lawama nyingi katika jambo ambalo unataka kulifanya zaidi na kuwa na ujasiri wa kusema hili jambo linawezekana kabisa.

Pili, kuwa wabunifu. Ubunifu Barani Afrika katika mambo mengi tunayoyafanya ni mdogo sana. Ubunifu ni chanzo kikubwa cha kujiletea maendeleo tuweni......

Tatu, rushwa tupambane nayo sana kwani ni kubwa kuliko tunavyodhani barani Afrika.

Nne, Migogoro ya kisiasa, ardhi (wakulima na wafugaji) na Ugaidi unatutafuna ipasavyo na bila kuthibiti haya mambo kusema kweli tuna safari ndefu kufikia maendeleo tunayoyataka.

Ujinga, Maradhi, Umasikini ni changamoto ambazo zinalifanya bara letu kudidimia kabisa na bila kuzitatua safari yetu ni ndefu sana ili kuyafikia maendeleo tunayoyataka.

Na tumeona tangu zamani kuwa mambo mawili ni ya Msingi sana katika kuendelea kwetu. Lazima tuwekeze katika, SAYANSI NA TEKNOLOJIA tujikite zaidi katika kuendeleza TEKNOLOJIA ya chini kabisa yaani INDIGENEOUS TECHNOLOJI. India na China zimefanikiwa sana katika dawa za asili kwa sababu ya kuwapa uwezo wabunifu katika mambo ya dawa za asili na kuwasaidia katika kufikia standard ya nchi na Kimataifa.

Jambo la pili ni kukuza uchumi (uchumi wa leo umeshikiliwa na TEKNOLOJIA zaidi). Mnaweza kuwa na kila kitu nchini mwenu lakini kama mpo mpo tu hizo rasilimali haziwezi kuwasaidia kama TEKNOLOJIA na JINSI ya kukuza uchumi ziko chini.

“We build too many walls and not enough bridges,” said Sir Isaac Newton.

Simon Jilala.
 
Back
Top Bottom