MAENDELEO: Kwanini Bukoba hakuna stendi yenye hadhi kama mji wa wasomi?

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Tatizo la Bukoba ni serkali,mchawi wa Kagera ni serkali mbaya wa maendeleo ya Bukoba ni ccm,tangia Nyerere mkoa ulitengwa kuanzie elimu,afya na miundo mbinu hakuna bahati mbaya hii ni mikakati iliyoasisiwa kwa wivu wa maendeleo tuliyokuwa nayo mapema.

Mwaka 1928 mji ulikuwa unakuwa kwa kasi lakini Nyerere akaona wivu ndo ukaandaliwa mkakati wa kudhoofisha Bukoba na Kagera kwa ujumla nakutengeneza sheria za uhujumu uchumi wakataifisha mali za watu watu waliamua kubeba vitu vyao vya thamani na kwenda kuvitelekeza maporini ili visikutwe nyumbani vitu kama mabati,tv,pikipiki,baiskeli ata fedha nyingi zilichimbiwa ardhiri na wengi walisahau walikoziweka.

Nyumba za watu zilichukuliwa na serkali watu wenye pesa zao ambao ndio walikuwa wafanyabiashara wakakimbia nchi wakiogopa kufungwa,wengi walikimbilia Uingereza,Ujerumani,Marekani nakwingineko.

Juhudi za kudidimiza Kagera ziliendelea wawekezaji wengi walitaka kujenga viwanda Kagera lakini walikataliwa na kuelekezwa Mwanza, nataka niwambie Nchii Kagera ina hali ya hewa nzuri ya kuishi kuliko mikoa mingi apa nchini Kagera ina ardhi yenye rutuba kuliko mikoa mingine lakini pia ina ardhi ya kutosha kwaajili ya kilimo cha kibishara.

Upande wa stendi kuu na soko kuu la Bukoba kama walivyosema watangulizi apo juu hakuna kabila la kujenga stendi au soko,hakuna kanuni wala sheria inayotoa nafasi kufanya ivyo swala la stendi nila serkali serkali kushindwa kujenga stendi na soko ni mwendelezo wa kuididimiza Kagera ila katika awamu zote za utawala awamu ya tano imefunga record maana babala ya kupeleka fedha za maendeleo waliamua kubeba ata za misaada mfano mzuri nizile B60 zilizotolewa kwaajili ya wahanga wa TETEMEKO LA ARDHI 2016 tuliambulia B3 tu zilizojenga shule ya Ihyungo japo na penyewe ni utata mtupu maana kuna tetesi kuwa shule ilijengwa na makampuni mawili ndio walitoa hizo B3.

Mvutano uliomshinda Kikwete akiwa Rais alipofika Kagera na kukutana na Kagasheki aliyekuwa Mbunge wakati ule na aliyekuwa Meya wa mji Dr.Amani Rais alishindwa kutatatua mgogoro ule uliokuwa wa kimaslahi kati ya Ccm,Mbunge na Meya soko kuu halikujengwa na stendi pia.

2014 wanaBukoba wakafanya mabadiliko makubwa serkali za mitaa wakafuta wenyeviti wote wa mitaa na wajumbe wake 2015 madiwani 70 wakatoka upinzani na Mbunge iliyopelekea Meya na Naibu wake kutoka upinzani ndio muda Magufuli aliingia madarakani akaelekeza tamisemi waondoe makusanyo yote ya halmashauri kurudi serkali kuu halmashauri nyingi zikadhoofika nyingine zikishindwa kujiendesha nakutishiwa kufutwa lakini Manispaa ya Bukoba ilijibana na kufanikiwa kujenga stendi mpya Kyakairabwa uku wakishindana na serkali kutokana na fedha za ndani chini ya usimamizi makini wa Meya kijana Chief Karumuna na Naibu Meya Jimmy Karugendo walifanya kazi kubwa uku wakiunganisha makundi yaliyokuwa asimu

2019 Mwendazake kamwagaanyanga akachukua wenyeviti wote serkali za mitaa na wajumbe wake 2020 akachukua madiwani,wabunge na Urais chakwanza alielekeza Tamisemi warudishe makusanyo kwenye halmashauri lakini kwa upande wa Bukoba pamoja na kurudishiwa makusanyo wakaanzisha mgogoro mpya wakidai stendi ya Kyakairabwa ikiendelezwa watawainua CHADEMA kwahiyo 2024/25 watabwagwa kwenye UCHAGUZI.

Mungu akiwa fundi mkuu akatwangwa mtu na kufanya utulivu wa muda nchini.
Nimeweka michoro ya Stendi mpya iliyojengwa Kyakairabwa ambayo Kama ingekamilika ingebadili hali ya mji na mkoa kwa ujumla.
Lakini pia nimeweka na picha ya stendi inayotumika sasa ivi na soko kuu la Bukoba ni aibu kwa serkali inayojinasibu na uchumi wa kati.
FB_IMG_1619767559216.jpg
FB_IMG_1619767549377.jpg
FB_IMG_1619767566487.jpg
IMG_20210410_135017_067.jpg

IMG_20210410_135138_351.jpg
 
Mnakaa kulalamika badala muungane mjenge bukoba yenu. mnajisifia kuwa wasomi kumbe hopeless
Yaani elimu yenu yoote hadi mnajiita nshomile ndo mmefika hapa, kuishia kulalamika
Kuweni kama wachaga. Huyu alikuwa katibu kwa mwezi mmoja si wa kwenu, huyo karamagi si wa kwenu, Prof wa visenti vya mboga naye si wa kwenu.
Check yule mrombo alivyong'arisha kwao kwa lami
Stupid kabisa nyie
Mie ni mtani wenu ila niyoandika siyo utani
 
Afadhali ule mpango wa ujenzi wa sitendi mpya ulikwama,utajengaje sitendi porini kyakairabwa ?
 
Akili zimukutoka kweli kweli aisee! Hivi hata kutunga uongo wa kuwaubaisha watu hujui? Kwa mfano hizo TV zilizotupwa porini miaka ya Mwl Nyerere zilikuwa zinarushwa na kituo gani, maana TV zimeingia Tanzania miaka ya 90 na kituo cha kwana kilikuwa kinaitwa CTN, kikajafuatiwa na ITV! Sijui kama kumbukumbu zako za kitoenda shule zinakuangazia kuwa miaka hiyo Rais alikuwa Nyerere! Kwa taarifa yako Mwl Nyerere alistaafu 1985. Wadsnganye wajinga kama wewe, lakini siyo watu werevu kama mimi hapa!
 
Uongo Mtupu

Kagera haiendelei kwasababu moja tu :

Wahaya hawapapendi kwao, hawawekezi kwao kama ilivyo kwa watu wa kanda ya Kaskazini.

Huo ni ukanda wa kiikweta, mvua za kutosha, Ardhi nzuri, Wamekuwa na wasomi wengi kuliko jamii zingine nchini kabla na baada tu ya Uhuru, ila wahaya wanajazana mjini na kuwekeza kisha wanasahau kurudi nyumbani kwao.

Nyerere mnamsingizia tu, mbona mlipotaka kudhulumiwa na Dikteta IDD AMIN aliwatetea sana kwa kuita jeshi lenye makabila yote nchini liwapiganie?

That's it mengine ni maneno tu
 
Jamaa mwongo anajitetea tu
 
Mbona wanyakyusa miaka ya 2015 kama sikosei waliungana na kuijenga mbeya yao nyie mnasubiri mbeya inajengwa na wana mbeya wanatumia nguvu na kuungana pambaneni
 
Afadhali ule mpango wa ujenzi wa sitendi mpya ulikwama,utajengaje sitendi porini kyakairabwa ?
Mara ya mwisho kwenda bukoba ni lini. Mji wa bukoba umepanuka na kufika katoma. Kyakairabwa sio porini tena. Baada ya watu kusikia stendi inaamia kule ujenzi unaofanywa unaweza kimbia.
 
Yaan Bukoba hiyo ndio huwa inafananishwa na Moshi?? Duh kwel dunia haiishi vituko
 
Mnakaa kulalamika badala muungane mjenge bukoba yenu. mnajisifia kuwa wasomi kumbe hopeless
Yaani elimu yenu yoote hadi mnajiita nshomile ndo mmefika hapa, kuishia kulalamika
Kuweni kama wachaga. Huyu alikuwa katibu kwa mwezi mmoja si wa kwenu, huyo karamagi si wa kwenu, Prof wa visenti vya mboga naye si wa kwenu.
Check yule mrombo alivyong'arisha kwao kwa lami
Stupid kabisa nyie
Mie ni mtani wenu ila niyoandika siyo utani
Mbona ume comment kwa hasira namna hii mkuu, kulikoni?
 
Yaan Bukoba hiyo ndio huwa inafananishwa na Moshi?? Duh kwel dunia haiishi vituko
Kinachofananishwa ni vijijini mzee bukoba rular yaan muleba,misenyi na karagwe huko ndo kumepiga gap nyumba za huko hata bukoba mjini huzipati.

Mji wa bukoba changamoto yake ni miundombinu hasa stendi
 
Mara ya mwisho kwenda bukoba ni lini. Mji wa bukoba umepanuka na kufika katoma. Kyakairabwa sio porini tena. Baada ya watu kusikia stendi inaamia kule ujenzi unaofanywa unaweza kimbia.
Nipo hata leo,sitendi ilitakiwa iwe pembeni mwa barabala kuu,na siyo uchochoroni.
 
Tatizo la Bukoba ni serkali,mchawi wa Kagera ni serkali mbaya wa maendeleo ya Bukoba ni ccm,tangia Nyerere mkoa ulitengwa kuanzie elimu,afya na miundo mbinu hakuna bahati mbaya hii ni mikakati iliyoasisiwa kwa wivu wa maendeleo tuliyokuwa nayo mapema.

Mwaka 1928 mji ulikuwa unakuwa kwa kasi lakini Nyerere akaona wivu ndo ukaandaliwa mkakati wa kudhoofisha Bukoba na Kagera kwa ujumla nakutengeneza sheria za uhujumu uchumi wakataifisha mali za watu watu waliamua kubeba vitu vyao vya thamani na kwenda kuvitelekeza maporini ili visikutwe nyumbani vitu kama mabati,tv,pikipiki,baiskeli ata fedha nyingi zilichimbiwa ardhiri na wengi walisahau walikoziweka.

Nyumba za watu zilichukuliwa na serkali watu wenye pesa zao ambao ndio walikuwa wafanyabiashara wakakimbia nchi wakiogopa kufungwa,wengi walikimbilia Uingereza,Ujerumani,Marekani nakwingineko.

Juhudi za kudidimiza Kagera ziliendelea wawekezaji wengi walitaka kujenga viwanda Kagera lakini walikataliwa na kuelekezwa Mwanza, nataka niwambie Nchii Kagera ina hali ya hewa nzuri ya kuishi kuliko mikoa mingi apa nchini Kagera ina ardhi yenye rutuba kuliko mikoa mingine lakini pia ina ardhi ya kutosha kwaajili ya kilimo cha kibishara.

Upande wa stendi kuu na soko kuu la Bukoba kama walivyosema watangulizi apo juu hakuna kabila la kujenga stendi au soko,hakuna kanuni wala sheria inayotoa nafasi kufanya ivyo swala la stendi nila serkali serkali kushindwa kujenga stendi na soko ni mwendelezo wa kuididimiza Kagera ila katika awamu zote za utawala awamu ya tano imefunga record maana babala ya kupeleka fedha za maendeleo waliamua kubeba ata za misaada mfano mzuri nizile B60 zilizotolewa kwaajili ya wahanga wa TETEMEKO LA ARDHI 2016 tuliambulia B3 tu zilizojenga shule ya Ihyungo japo na penyewe ni utata mtupu maana kuna tetesi kuwa shule ilijengwa na makampuni mawili ndio walitoa hizo B3.

Mvutano uliomshinda Kikwete akiwa Rais alipofika Kagera na kukutana na Kagasheki aliyekuwa Mbunge wakati ule na aliyekuwa Meya wa mji Dr.Amani Rais alishindwa kutatatua mgogoro ule uliokuwa wa kimaslahi kati ya Ccm,Mbunge na Meya soko kuu halikujengwa na stendi pia.

2014 wanaBukoba wakafanya mabadiliko makubwa serkali za mitaa wakafuta wenyeviti wote wa mitaa na wajumbe wake 2015 madiwani 70 wakatoka upinzani na Mbunge iliyopelekea Meya na Naibu wake kutoka upinzani ndio muda Magufuli aliingia madarakani akaelekeza tamisemi waondoe makusanyo yote ya halmashauri kurudi serkali kuu halmashauri nyingi zikadhoofika nyingine zikishindwa kujiendesha nakutishiwa kufutwa lakini Manispaa ya Bukoba ilijibana na kufanikiwa kujenga stendi mpya Kyakairabwa uku wakishindana na serkali kutokana na fedha za ndani chini ya usimamizi makini wa Meya kijana Chief Karumuna na Naibu Meya Jimmy Karugendo walifanya kazi kubwa uku wakiunganisha makundi yaliyokuwa asimu

2019 Mwendazake kamwagaanyanga akachukua wenyeviti wote serkali za mitaa na wajumbe wake 2020 akachukua madiwani,wabunge na Urais chakwanza alielekeza Tamisemi warudishe makusanyo kwenye halmashauri lakini kwa upande wa Bukoba pamoja na kurudishiwa makusanyo wakaanzisha mgogoro mpya wakidai stendi ya Kyakairabwa ikiendelezwa watawainua CHADEMA kwahiyo 2024/25 watabwagwa kwenye UCHAGUZI.

Mungu akiwa fundi mkuu akatwangwa mtu na kufanya utulivu wa muda nchini.
Nimeweka michoro ya Stendi mpya iliyojengwa Kyakairabwa ambayo Kama ingekamilika ingebadili hali ya mji na mkoa kwa ujumla.
Lakini pia nimeweka na picha ya stendi inayotumika sasa ivi na soko kuu la Bukoba ni aibu kwa serkali inayojinasibu na uchumi wa kati.View attachment 1768711View attachment 1768713View attachment 1768715View attachment 1768740

View attachment 1768739
Mmejaa Ujuaji Mwingi Sana
 
Uongo Mtupu

Kagera haiendelei kwasababu moja tu :

Wahaya hawapapendi kwao, hawawekezi kwao kama ilivyo kwa watu wa kanda ya Kaskazini.

Huo ni ukanda wa kiikweta, mvua za kutosha, Ardhi nzuri, Wamekuwa na wasomi wengi kuliko jamii zingine nchini kabla na baada tu ya Uhuru, ila wahaya wanajazana mjini na kuwekeza kisha wanasahau kurudi nyumbani kwao.

Nyerere mnamsingizia tu, mbona mlipotaka kudhulumiwa na Dikteta IDD AMIN aliwatetea sana kwa kuita jeshi lenye makabila yote nchini liwapiganie?

That's it mengine ni maneno tu
Kagera imepiga hatua kubwa upande wa makazi vijijini sawa na Kilimanjaro tatizo umasikini wa kipato na ukosefu wa elimu wa wananchi wake wengi walioko vijijini. Pili kuna ukosefu mkubwa sana wa exposure na viongozi wao wabovu na wezi.

Manispaa ya Bukoba ni tatizo zaidi ambako najiuliza kuanzia wateule mpaka viongozi wa kuchaguliwa kama wanaelewa wapo ktk moja ya miji mibovu kabisa Tanzania. Mji mchafu hakuna barabara za maana na mitaa michafu. Wananchi wengi ktkt ya manispaa ya Bukoba ni wachafu.

Toka uwanja wa ndege kuingia ktkt ya mji unashuhudia mji mbovu na bila shaka wenye viongozi wabovu kabisa. Nyumba chafu mpaka za shirika letu la nyumba NHC ambazo sijui mara ya mwisho kupakwa rangi. Magenge ya kahawa na majungu ktkt ya mji. Unajiuliza kwa nini uongozi hauchukui hatua kwa wananchi hawa wazembe waliojazana mjini. Wakati miji mingine imechukua hatua ya kuondoa wamachinga barabarani Bukoba hiyo amri haitekelezwi!!

Manispaa hakuna Stand wala Soko la maana shughuli zinaendelea ktk maeneo machafu!! Hakuna hata uwekezaji wa serikali ktk majengo ya ofisi na biashara. Wala hakuna hatua ya manispaa kusimamia mpango mji wa manispaa ya Bukoba. Nimuombee Rais Samia achukue hatua maalumu ya kuirudisha Bukoba ktk enzi yake ya miaka 1970's. Bukoba imeangamizwa na ujinga na uongozi mbovu!
 
Tatizo la Bukoba ni serkali,mchawi wa Kagera ni serkali mbaya wa maendeleo ya Bukoba ni ccm,tangia Nyerere mkoa ulitengwa kuanzie elimu,afya na miundo mbinu hakuna bahati mbaya hii ni mikakati iliyoasisiwa kwa wivu wa maendeleo tuliyokuwa nayo mapema.

Mwaka 1928 mji ulikuwa unakuwa kwa kasi lakini Nyerere akaona wivu ndo ukaandaliwa mkakati wa kudhoofisha Bukoba na Kagera kwa ujumla nakutengeneza sheria za uhujumu uchumi wakataifisha mali za watu watu waliamua kubeba vitu vyao vya thamani na kwenda kuvitelekeza maporini ili visikutwe nyumbani vitu kama mabati,tv,pikipiki,baiskeli ata fedha nyingi zilichimbiwa ardhiri na wengi walisahau walikoziweka.

Nyumba za watu zilichukuliwa na serkali watu wenye pesa zao ambao ndio walikuwa wafanyabiashara wakakimbia nchi wakiogopa kufungwa,wengi walikimbilia Uingereza,Ujerumani,Marekani nakwingineko.

Juhudi za kudidimiza Kagera ziliendelea wawekezaji wengi walitaka kujenga viwanda Kagera lakini walikataliwa na kuelekezwa Mwanza, nataka niwambie Nchii Kagera ina hali ya hewa nzuri ya kuishi kuliko mikoa mingi apa nchini Kagera ina ardhi yenye rutuba kuliko mikoa mingine lakini pia ina ardhi ya kutosha kwaajili ya kilimo cha kibishara.

Upande wa stendi kuu na soko kuu la Bukoba kama walivyosema watangulizi apo juu hakuna kabila la kujenga stendi au soko,hakuna kanuni wala sheria inayotoa nafasi kufanya ivyo swala la stendi nila serkali serkali kushindwa kujenga stendi na soko ni mwendelezo wa kuididimiza Kagera ila katika awamu zote za utawala awamu ya tano imefunga record maana babala ya kupeleka fedha za maendeleo waliamua kubeba ata za misaada mfano mzuri nizile B60 zilizotolewa kwaajili ya wahanga wa TETEMEKO LA ARDHI 2016 tuliambulia B3 tu zilizojenga shule ya Ihyungo japo na penyewe ni utata mtupu maana kuna tetesi kuwa shule ilijengwa na makampuni mawili ndio walitoa hizo B3.

Mvutano uliomshinda Kikwete akiwa Rais alipofika Kagera na kukutana na Kagasheki aliyekuwa Mbunge wakati ule na aliyekuwa Meya wa mji Dr.Amani Rais alishindwa kutatatua mgogoro ule uliokuwa wa kimaslahi kati ya Ccm,Mbunge na Meya soko kuu halikujengwa na stendi pia.

2014 wanaBukoba wakafanya mabadiliko makubwa serkali za mitaa wakafuta wenyeviti wote wa mitaa na wajumbe wake 2015 madiwani 70 wakatoka upinzani na Mbunge iliyopelekea Meya na Naibu wake kutoka upinzani ndio muda Magufuli aliingia madarakani akaelekeza tamisemi waondoe makusanyo yote ya halmashauri kurudi serkali kuu halmashauri nyingi zikadhoofika nyingine zikishindwa kujiendesha nakutishiwa kufutwa lakini Manispaa ya Bukoba ilijibana na kufanikiwa kujenga stendi mpya Kyakairabwa uku wakishindana na serkali kutokana na fedha za ndani chini ya usimamizi makini wa Meya kijana Chief Karumuna na Naibu Meya Jimmy Karugendo walifanya kazi kubwa uku wakiunganisha makundi yaliyokuwa asimu

2019 Mwendazake kamwagaanyanga akachukua wenyeviti wote serkali za mitaa na wajumbe wake 2020 akachukua madiwani,wabunge na Urais chakwanza alielekeza Tamisemi warudishe makusanyo kwenye halmashauri lakini kwa upande wa Bukoba pamoja na kurudishiwa makusanyo wakaanzisha mgogoro mpya wakidai stendi ya Kyakairabwa ikiendelezwa watawainua CHADEMA kwahiyo 2024/25 watabwagwa kwenye UCHAGUZI.

Mungu akiwa fundi mkuu akatwangwa mtu na kufanya utulivu wa muda nchini.
Nimeweka michoro ya Stendi mpya iliyojengwa Kyakairabwa ambayo Kama ingekamilika ingebadili hali ya mji na mkoa kwa ujumla.
Lakini pia nimeweka na picha ya stendi inayotumika sasa ivi na soko kuu la Bukoba ni aibu kwa serkali inayojinasibu na uchumi wa kati.View attachment 1768711View attachment 1768713View attachment 1768715View attachment 1768740

View attachment 1768739
Tukiachilia mbali porojo na kejeri mada yako ina point ya msingi na inahitaji kuangaliwa kwa jicho pevu japo ktk kipengere cha elimu sio kweli mmetengwa ila mengine yote serikali inapaswa ijitathimin km wenye dhamana

Sent from my TECNO BC2c using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom